Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Kikao cha Kadhia za Ummah

Usaidizi wa Bidhaa na Huduma Baina ya Ukusanyaji na Uchungaji

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya kikao chake cha kila mara cha Kadhia za Umma kwa anwani "Usaidizi wa Bidhaa na Huduma Baina ya Ukusanyaji na Uchungaji" mnamo Jumamosi, 1 Rabi' Al-Awwal 1442 H sawia na 17/10/2020 – saa tano asubuhi.

Waraka wake wa kwanza kwa anwani: "'Kuondoa Msaada na Ulevi wa Kushindwa", Iliwasilishwa na Dkt. Ahmed Abdel-Fadil, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, ambaye alisisitiza kupitia waraka wake kwamba serikali imelevywa na kushindwa katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kijamii na mambo mengine ya maisha.

Halafu Profesa Khaled Abdullah, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, alizungumza juu ya masuluhisho, akionyesha kwamba sababu ya migogoro hii ni kuasisiwa kwa serikali kwa msingi mwingine usiokuwa Uislamu. Dola ya Uislamu, ambayo msingi wake ni itikadi ya Kiislamu, inakataza sababu za gharama kubwa zinazowakilishwa katika forodha, kodi na ukiritimba, na hizi zote hupandisha bei za bidhaa na huduma, na utukufu wa kila moja ya miamala hii unathibitishwa na andiko la Sharia linayoyaharamisha.

Watoaji maoni katika kikao hiki ni pamoja na:

  1. Ustaadh Mohamed Mabrouk – mwandishi habari maarufu.
  2. Saad Ahmed Saad – Mwanachama wa Chama cha Wanachuoni Sudan.
  3. Muhammad Osman Saleh – Mwenyekiti wa Chama cha Wanachuoni wa Sudan.
  4. Ustaadh Abdullah Imam – Mtafiti wa Historia.

Kwa kuhitimisha, Mh. Ahmed Saad Al-Hussein, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir na afisa wa mwendeshaji wa kikao, aliwashukuru waliohudhuria ukumbini na waliofuatilia kikao kupitia vyombo vya habari kwa ushiriki wao na ufuatiliaji.

Jumamosi, 1 Rabi’ Al-Awwal 1442 H sawia 17 Oktoba 2020 M

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 21 Oktoba 2020 13:35
Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.