Jumanne, 09 Ramadan 1445 | 2024/03/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Swala la Kashmir Linahitaji Ukombozi Kupitia Vikosi vya Kijeshi vya Pakistan, Wala Sio Ramani Mpya ya Kisiasa

Na: Mhandisi Moez – Pakistan*

Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, alizindua “ramani mpya ya kisiasa” ya Pakistan ambayo pia inajumuisha Kashmir Iliyokaliwa, siku moja kabla ya maadhimisho ya kwanza ya maamuzi ya India kukomesha kujitawala kwa eneo hilo. Tangu Modi kuiambatanisha Kashmir mnamo tarehe 5 Agosti 2019, utawala mseto wa kiraia na kijeshi wa Pakistan umekumbwa na shinikizo la raia la kuirudi Dola ya Kibaniani kwa namna ya kivita. Serikali imejaribu kuitikia shinikizo hilo la raia, kupitia vipimo vya kiishara kama vile; kuadhimisha Agosti 5 kama siku ya ukandamizaji, kampeni ya kiuhusiano wa Ummah juu ya Kashmir ikielezea madhila ya Waislamu wa Kashmir, wakidunisha uhusiano wa kidiplomasia na Dola ya Kibaniani na  kutoa wito kwa Raisi wa Amerika Donald Trump kushinikiza India juu ya Kashmir na kuomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuandaa kura ya maoni ndani ya Kashmir kupeana kwa Waislamu wa Kashmir haki yao ya kuchagua  kati ya kujiunga na India ama Pakistan, suluhu ambayo ina mizizi ndani ya kugawa kusikoisha kwa bara dogo la Hindi.

Suluhu zote hizi za kiishara zimekataliwa na Waislamu wengi ndani ya Pakistan. Waislamu wa Pakistan wanaufahamu wa kisiasa na wimbi la ufufuo wa Uislamu linalofagia katika ulimwengu wa Kiislamu kwa nguvu limeathiri jamii ya Pakistan. Sasa jamii ya Pakistan inatizama maslahi yake mengi na maswala katika mtizamo wa Kimfumo wa Uislamu, wakitafuta suluhu kutoka kwa Uislamu. Kile kinachoongeza matatizo kwa watawala wasaliti wa Pakistan, ni nafasi maalum na mapenzi ambayo Waislamu wa Pakistan wako nayo juu ya Kashmir. Huku Azad (iliyokombolewa) Kashmir ikiunganishwa kikamilifu na Pakistan kuu, maumivu ya Kashmir na mateso ya watu wake yanahisika moja kwa moja na Wapakistan wengi. Waislamu wa Pakistan wamevuja damu zao kwa ajili ya Kashmir, kwa furaha wakipeana watoto wao kwa Jihad ya Kashmir ya miaka ya 1990, na hiki ndicho chanzo cha ufahari na heshima kwao wao. Mawazo ya kuikomboa Kashmir kupitia Jihad yamekita ndani ya jamii ya Pakistan. Tangu Modi alipoiunganisha Kashmir, jamii ya Pakistan imepinga kwa hasira kutochukua hatua kwa serikali ya Pakistan juu ya Kashmir. Watu maarufu ndani ya Pakistan wametoa wito waziwazi wa kutumiwa nguvu za kijeshi katika kuikomboa Kashmir.

Swala la Kashmir pia liko na umuhimu maalum kwa Vikosi vya Kijeshi vya Pakistan ambavyo vinaiona India kuwa adui wa kishirikina ambaye ni adui wa daima wa taifa linalo amini Tawhid. Uadui huu wa miongo mingi umemakinika juu ya mzozo wa kijeshi juu ya Kashmir. Kashmir ni zaidi ya swala la ardhi ya Waislamu kunyakuliwa bali ni swala la heshima na la kujisifia kwa wanajeshi wa Pakistan. Kuunganishwa  kwa Kashmir na Modi mnamo tarehe 5 Agosti 2019 na kutochukua hatua yoyote kwa serikali ya Bajwa-Imran na kukataa wazi kujibu uchokozi wa Dola ya Kibaniani kwa kutumia vikosi vya kijeshi kumewakasirisha wanajeshi wa Pakistan ambao wanahisi kudhalilika kwa kushughulikiwa vibaya kwa adui wanaomdharau kama mwengine yeyote. Hasira hizi hazijaisha na zinawaogopesha watawala wa Pakistan ambao wanajaribu kutafuta njia nzuri ya kuwafanya wajinga na kuwadanganya Waislamu wa Pakistan na Vikosi vya Majeshi juu ya kadhia ya Kashmir.

Ramani mpya iliotolewa na serikali ya Pakistan ni jaribio jengine la kujifanyisha kama mlinzi wa hatma ya Kashmir. Ikishuhudiwa hasira na udhalilifu uliohisika nchini India pale bunge la Nepal lilipopitisha ramani, inayoonesha maeneo ya mipakani inayozozania pamoja na India kama yake, serikali ya Pakistan imeitabanni wazo hilo kutoka Nepal, katika matumaini kwamba hili litaonesha uzito wa swala la Kashmir na kujilinda na hasira za Umma. Hata hivyo matendo ya serikali ya Nepal yalitengeneza mawimbi ya kieneo kwa sababu Nepal kiasili inatizamwa kama nchi dhaifu kusimama dhidi ya India na imekuwa ikivuka laini ya India. Hivyo pindi serikali ya Nepal ilipo pambana, kwa usaidizi wa Uchina, na India kisiasa kwa kuzindua ramani mpya ya kisiasa, ilionekana kana kwamba Nepal inajikomboa kutokana na hali zilizopita na kuipinga India kwa niaba ya Uchina. Hili limeonekana kama tukio muhimu sana kwa sababu Uchina, Nepal na India zinaushirika katika mpaka wenye mzozo na hatua ya Nepal ilimaanisha inatafuta msaada wa Uchina ili kulinda maslahi yake. Pakistan kwa upande mwingine ni nguvu za kieneo ambazo kihistoria zinaonekana kuwa sawa na India. Taifa lililojihami kinyuklia lenye nguvu za kijeshi na historia ya makabiliano ya kijeshi na Dola ya Kibaniani. Hivyo, pindi serikali ya Pakistan ilipozindua ramani ya kisiasa ya Pakistan inayoonesha Kashmir Iliyokaliwa kama sehemu ya Pakistan, huku ikitangaza wazi kuwa haitatumia nguvu za kijeshi kutilia nguvu ramani yake ya kisiasa, serikali ya Pakistan ilidhihakiwa. Ilikuwa ni lengo la kuendeleza dharau kwa Ummah, kejeli na kashfakwa kujihusisha na hatua za kijanja na za kimapambo, ambazo hazina athari kwenye uwanja halisi au mizani ya nguvu za kieneo. Huu ndio uwazi wa jamii ya Pakistan na kile kinachostahili kufanyika Kashmir kutatua swala hilo, ni Jihad kwa vikosi vya kijeshi vya Pakistan.

Kuzinduliwa kwa ramani mpya na serikali ya Pakistan, na kukataliwa kwake na Waislamu wa Pakistan, ni ishara nyingine kwamba pengo kati ya jamii ya Pakistan na watawala wa sasa liko katika upana mrefu kabisa. Waislamu wa Pakistan wanaupenda Uislamu wao na wanataka kutawaliwa na sharia za Mwenyezi Mungu. Wanataka kuiona Dola ya Uislamu, Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itahukumu kwa yale yote yaliyoteremsha na Mwenyezi Mungu (swt), ikitabikisha suluhu za Kiislamu katika matatizo yetu na kuhamasisha vikosi vya kijeshi yetu kuikomboa Kashmir na Palestina.

فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ } فَعَسَى اللَّهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْأَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ

“Utaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Surat Al-Maida 5:52].

* Imeandikwa kwa  Ar-Rayah Newspaper – Toleo la 301

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 18 Septemba 2020 18:18

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu