Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bado Demokrasia Ingali Inahamasishwa?

Habari:

Rais Recep Tayyip Erdogan alihudhuria Mkutano wa 7 wa Kawaida wa Mkoa wa Kars na Karaman kutoka Ukumbi wa Vahdettin kupitia njia ya matangazo ya moja kwa moja. Wakati wa hotuba yake, Erdogan alisema "Tunachukua hatua madhubuti ambazo zitaiweka nchi yetu katika nafasi inayostahili katika mpangilio wa kiulimwengu, kisiasa na kiuchumi ambayo itabadilishwa upya baada ya janga hili. Tunazindua uhamasishaji mpya kabisa katika uchumi, mahakama na demokrasia. Tumeunda upya usimamizi wa uchumi. Tunakusudia kutekeleza haraka hatua ambazo zitatufanya tufikie malengo yetu '. (AA 14.11.2020)

Maoni:

Watawala ambao taarifa zao hazina tija, ambao maneno yao hayana maana, ambao ushauri wao hauna maana na ambao hawapati funzo kutokana na shida na misiba, ingawa hujifanya kama askari wa jeshi walioapa katika kuikokota jamii kwenye maafa. Wale ambao wamesahau kuwa wadhifa wao na cheo chao ni vya muda mfupi na ambao hawana habari kuwa watahesabiwa kwa Mwenyezi Mungu, wale ambao wanaona kila njia inaruhusiwa kwao kwa ajili ya kufikia maslahi rahisi ya kiulimwengu, kwa bahati mbaya ndio wanaowatawala watu. Ukweli ni kwamba Chama cha AK, ambacho kiko madarakani kwa takriban miaka 20, na kiongozi wake Rais Erdogan wangali wanazungumzia juu ya uhamasishaji katika uchumi, mahakama na demokrasia, wanapaswa kuwa na wasiwasi na mtu yeyote ambaye ana Imani, utambuzi na mazingatio. Tunasema wanapaswa kuwa na wasiwasi, kwa sababu walichokifanya ni kumbukumbu ya watakachokifanya.

Tunapoangalia mchakato ambapo Chama cha AK kiliingia madarakani nchini Uturuki, tunajua kwamba waliingia madarakani na siasa zao za kutatua shida za nchi ambayo ilipitia mgogoro mkubwa wa kifedha na ilikuwa na ripoti mbaya katika sheria na haki. Lakini wakati umeonyesha kuwa jamii inazungukwa na demokrasia, safu ya upendeleo ya kijamhuri ya mara kwa mara, rushwa, maslahi, utovu wa aibu, udhalimu, demokrasia iliyo endelea. Ubinafsishaji wa bidhaa zinazomilikiwa na umma zenye thamani ya makumi ya mabilioni ya dolari katika siku za mwanzo za uchumi. Kueneza riba ya kiwango cha chini kwa jamii. Ingawa pesa za kuvutia zinazotoka ng'ambo kwa miaka mingi zilifufua masoko na kuleta afueni kwa uchumi, tulisema kuwa puto hili litalipuka kama si sasa ni sasa hivi. Kuamini kwamba mpangilio wa kirasilimali, uliojengwa juu ya msingi wa unyonyaji na mgogoro, utaokolewa kupitia uhamasishaji, ni upungufu wa akili. Ni kujitenga na ukweli.

Gari ya moshi hii ambayo njia yake ni ya kimakosa, ambayo lengo lake ni imani ya kirongo, ambayo fundi wake anaitii Magharibi, ambayo viongozi wake ni wajinga, ambayo mabehewa yake yamejaa haramu na madhambi, haingefika salama kamwe. Si kichwa cha gari ya moshi wala reli ingeweza kuvumilia treni hii ya madhambi na haramu. Tayari haziwezi. Tunazungumza juu ya sheria ambapo hata Waziri wa Sheria analalamika juu ya haki, hakuna mtu anayekubali uamuzi aliopewa, wale ambao ni dhaifu lakini walio sahihi wanakuwa wakosefu, wale walio na nguvu lakini wakosefu wanaamiliwa kwa heshima, haki inaonekana kulingana na athari za mitandao ya kijamii. Je! Kutakuwa na tofauti yoyote kuzindua harakati katika mfumo wa sheria ambapo kwa sababu ya mawazo yao maelfu ya Waislamu wamefungwa bila haki, ambapo maelfu ya wanaume wanaadhibiwa kwa kuchukua ushuhuda wa wanawake kama msingi, ambapo maelfu ya vijana wamefungwa ambao walioa katika umri mdogo? Ukweli kwamba uhamasishaji katika eneo hili utatumikia ukandamizaji na dhuluma zaidi, ni dhahiri kama mchana.

 Ingawa kazi ya Rais Erdogan, juhudi, mapambano juu ya demokrasia na demokrasia iliyo endelea ni imani ya kirongo, hakuna shaka kwamba ina sura ya mafanikio na uthabiti zaidi. Kiasi ya kuwa miradi yote iliyofungua kwa upana mlango wa haram wakati ilikuwa imefunguliwa nusu mlango kupitia demokrasia iliyo endele, ambayo ilikubali makubaliano ambayo yalidhalilisha familia na jamii, ambayo hupeana haki kwa wapotovu wa LGBT kwa kutunga sheria na ambazo huangamiza familia na uchochezi wa usawa wa kijinsia, zilikuwa kwa ajili ya demokrasia iliyo endelea. Na kutenda kwa ujasiri zaidi katika njia hii kuliko makafiri wa Magharibi hakika ni uchungu sana. Hiyo inamaanisha haram na uhalifu katika maeneo haya yanaonekana kutotosha, mapya yataongezwa kwayo kupitia kuhamasishwa demokrasia.

Ulikuwa ukimtafuta Umar wa kila mji, lakini utawala wako na vitendo vyako vinafanana na mpangilio wa Abu Jahl. Kuwa Umar kunamaanisha kuwa na uwezo wa kusema sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu pindi alipopata jibu, 'Tutakurekebisha kwa panga zetu' kwa swali lake, 'Je! mtafanya nini nitakapopotoka?' Ni kuwa na hamu ya kutekeleza dini ya Mwenyezi Mungu. Ni kuweza kusema, 'Sitakunywa isipokuwa watu wangu wanywe hii' kuhusiana na sharubati iliyoletwa kwake. Sio kuishi  kifahari wakati mamilioni ya watu wanang'ang'ana chini ya mstari wa njaa kupitia kila aina ya kodi na utozaji.

Uhamasishaji gani unaweza kutatua ukweli kwamba wewe ni kiziwi kwa sauti ya haki ya mamilioni ya watu? Ungali unahamasisha demokrasia wakati kila aina ya haram na fedheha zinafanywa kuwa halali kupitia mikono yako? Je! Ukweli kwamba unajaribu kuwadanganya Waislamu kupitia nidhamu hii ya imani ya kirongo, wakati sababu halisi ya shida hizi na zaidi ni nidhamu ya sasa ya kirasilimali ya kidemokrasia, sio uhamasishaji dhidi ya Mwenyezi Mungu na dini yake?

Ikiwa kweli ulitaka kuwa na utaratibu ambapo kila mtu atapata amani na furaha, ungezindua uhamasishaji wa Khilafah kwa njia ya Utume ambayo ni nidhamu ya utawala ya Uislamu na sio kwa demokrasia. Kwa njia hii, ungekuwa miongoni mwa washindi katika ulimwengu huu na vilevile kesho Akhera. Tuseme nini; kile mtu alinacho akilini mwake hujitokeza katika mazungumzo yake...

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ahmet SAPA

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 27 Novemba 2020 17:20
Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.