Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utafutaji Haki wa Süleyman Soylu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Majadiliano kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Süleyman Soylu, na Waziri wa Haki, Abdulhamit Gül, yalitia muhuri kwenye ajenda ya kisiasa ya Uturuki. Soylu alijibu kwenye Twitter kuhusu kuachiliwa kwa mtu aliyemtukana mamake kwenye mitandao ya kijamii. “Mamangu amekuwa hospitalini kwa siku 45. Mlaani huyo muovu chini ya picha yangu na mamangu akiwa alisimama mbele ya korti na kuachiliwa kwa dhamana. Nifanye nini? Je! Inabadilisha nini kwamba mimi ni waziri? Wakati unapambana na maswala ya nchi na serikali, inamaanisha nini kutoweza kulinda heshima ya mama yake? Nitachukulia kama uchochezi ikiwa atachukuliwa tena na tweet yangu.” Waziri wa Haki Abdulhamit Gül alijibu tweet ya Soylu kwa taarifa hii wakati wa hotuba yake katika "Mkutano wa Tathmini wa Mahakama za Rufaa katika Mwaka wao wa 5." "Ninatoa wito kwa wale ambao wananiamuru kukamata kila siku kutoka katika mitandao ya kijamii. Wale ambao hawafurahishwi na utaratibu huu wanaweza kutumia haki yao ya kukata rufaa lakini hakuna mtu anayeweza kutikisa vidole vyao kwa mahakama." (Mashirika ya habari)

Maoni:

Ajenda nchini Uturuki inabadilika kwa haraka sana hivi kwamba wakati mwingine inakuwa vigumu kufuatilia. Mara kwa mara, mambo yanakuja moja baada ya moja kama mvua kubwa. Sehemu ya mazungumzo ya siku za hivi karibuni ni mzozo kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Süleyman Soylu na Waziri wa Haki, Abdulhamit Gül. Süleyman Soylu aliyetuma tweet hiyo hapo juu baada ya kushambuliwa kwenye Twitter kwa maoni ya matusi alipokuwa akisambaza picha yake na mama yake, ambaye amekuwa akipokea matibabu hospitalini kwa siku 45 kwa sababu ya virusi vya korona. Kwa kuziangalia sentensi za Soylu hapo juu, inaonekana jinsi gani anavyo papatika kutokana na sheria zilizopo na njia yake za utekelezaji, ingawa anabeba jukumu mojawapo ya majukumu muhimu zaidi katika utaratibu wa kiidara wa nchi.

Kufuatia taarifa hizi zilizotumiwa na Soylu na Gül, suala hili lilijadiliwa katika vyombo vikuu vya habari. Katika hotuba hizo, walitaja kwamba sheria, ambazo zinafanya kazi kwa sasa, haziwezi kuwaadhibu wale wanaofanya uhalifu ikiwa ni pamoja na kutukana, sheria hazitoshelezi, mahakama zinatoa maamuzi kulingana na ukosoaji kwenye mitandao ya kijamii, kukamatwa hakuwezi kufanywa kwa vifungo vya miaka miwili au chini yake kulingana na sheria ya sasa ya utekelezaji na maswala mengine mengi pia yalitajwa. Kuhusu masuala haya yote, tungependa kusema yafuatayo.

a- Bila shaka, sheria ambazo zinatumika sasa ni sheria zisizokuwa za Kiislamu na kuzitekeleza na kuwahukumu watu nazo ni haram kwa mujibu wa Sharia. Utekelezaji wa sheria hizi hautatoa haki na amani kwa njia yoyote ile.

b- Kama ilivyo kwa mfano wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Soylu, watekelezaji wa nidhamu ya kikafiri wa ya kidemokrasia hulia wakati matokeo dhidi yao yanapotokea kama natija ya utekelezaji wa sheria zilizopo. Lakini, watekelezaji wawa hawa hawahisi vibaya kamwe kwa sababu ya adhabu za kidhalimu na haramu dhidi ya wale wanaobeba Da'wah ya Kiislamu, badala yake wanaunga mkono utekelezaji huu na wanafurahishwa nao. Kwa kweli, yeye ndiye mkuu wa wakala wa utekelezaji wa sheria ambapo hiyo ndio hatua ya kwanza na muhimu zaidi katika kutekeleza sheria za kikafiri za kidemokrasia.

c- Süleyman Soylu anapaswa kujua vizuri kabisa kwamba asingelalamika juu ya jambo kama hilo lau kama angefanya kazi kwa ajili ya utekelezaji na ulinzi wa sheria zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu badala ya kumsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume kwa kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya utekelezaji wa sheria za kikafiri za kidemokrasia.. Kwa sababu aina hizi za uhalifu huchukuliwa kama jinai ya ta'zir, katika hali kama hiyo, kwa kuzingatia ushahidi, Qadhi hutoa adhabu ya mboko kwa mtu aliyefanya uhalifu huo na kutoa kifungo iwapo ataona kinafaa. Kwa kweli, Hizb ut Tahrir imefafanua haya katika vitabu vyote viwili vinavyoitwa Nidhamu ya Kuadhibu katika Uislamu na Utangulizi wa Katiba na kufafanua adhabu. Pia, adhabu zilizowekwa kulingana na Uislamu haziwezi kupunguzwa kwa sababu kama vile kupunguzwa kutokana na sababu kama vile upunguzaji wa utekelezaji, kifungo cha nje, kuachiliwa kwa dhamana nk. Lengo la adhabu hizi ni kuwakomesha watu kufanya uhalifu sio kuwashajiisha kufanya uhalifu kama ilivyo katika sheria za jinai zinazotekelezwa hivi sasa nchini Uturuki.

d- Sheria zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu zitatabikishwa katika Dola ya Khilafah Rashida ambayo itasimamishwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Haki itasimamishwa kwa hali halisi kwa utekelezaji wa sheria hizi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammet Hanefi YAĞMUR

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu