Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 07/10/2020

Vichwa vya Habari:

Upinzani Wachukua Mamlaka Nchini Kyrgyzstan

Mwisho wa Upendeleo Mkubwa wa Dolari

Kiwango cha Vifo Chaongezeka Eneo la Nagorno-Karabakh

Maelezo:

Upinzani Wachukua Mamlaka Nchini Kyrgyzstan

Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan Kubatbek Boronov amejiuzulu baada ya Tume Kuu ya Uchaguzi kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa bunge wa hivi karibuni kujibu tuhuma za wizi wa kura. Boronov na Dastan Jumabekov, spika wa bunge la nchi hiyo, waliwasilisha barua zao za kujiuzulu katika mkutano wa wabunge katika mji mkuu Bishkek mnamo 6 Oktoba. Maelfu waliandamana katika uwanja wa Ala-Too mnamo 5 Oktoba kupinga udanganyifu wa uchaguzi. Ghasia zilizotokea zilishuhudia huduma za usalama zikijibu kwa mabomu ya machozi, risasi za mpira na maguruneti ya mshtuko dhidi ya waandamanaji, na kumuua mtoto mmoja wa miaka 19 na kujeruhi 590. Baadaye siku hiyo, waandamanaji walivamia jumba la White House, ambalo ndilo lenye afisi za rais wa nchi hiyo na bunge. Kundi la vyama 13 vya upinzani siku ya Jumanne liliunda Baraza la Kuratibu ambalo kwa muda limechukua jukumu kamili la kutafuta njia ya kukabiliana na mkwamo wa sasa. Kyrgyzstan si ngeni kwa machafuko ya kisiasa. Katika miaka 15 iliyopita, nchi hiyo ilikabiliwa na mapinduzi mawili - mnamo 2005 na 2010 na Amerika na Urusi zikilipigania taifa hili la Asia ya Kati.

Mwisho wa Upendeleo Mkubwa wa Dolari

Stephen Roach, Profesa wa Yale na mwenyekiti wa zamani wa Morgan Stanley Asia aliyeinishwa katika gazeti la Financial Times upendeleo wa dolari unakaribia kuondolewa. Kuna uwezekano wa kuanguka kwa dolari na inaweza kuanguka kwa asilimia 35 kufikia mwisho wa 2021. Sababu: mwingiliano mbaya kati ya kushuka kwa kiwango cha uhifadhi wa ndani na upungufu wa akaunti uliopo sasa. Kwa mlipuko unaohusiana na Covid katika upungufu wa serikali ya shirikisho ndio chanzo cha kwanza cha tatizo hili, hii ni ajali iliyokuwa inasubiri kutokea. Kuingia kwenye janga hili, kiwango halisi cha uhifadhi wa nyumbani kilikuwa wastani wa asilimia 2.9 tu ya pato la taifa kutoka 2011 hadi 2019, chini ya nusu ya asilimia 7 ya wastani kutoka 1960 hadi 2005. Hifadhi hii nyembamba iliiacha Amerika katika hatari ya mshtuko wowote, achilia mbali Covid. Pamoja na Amerika kujikamua zaidi baada ya miongo miwili ya vita, huku nguvu yake laini ikiwa magofu, dolari inasalia kuwa faida yake ya mwisho, ambayo sasa inaporomoka kwa kasi.

Kiwango cha Vifo Chaongezeka Eneo la Nagorno-Karabakh

Mapigano makali yanaendelea katika eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh kati ya majeshi ya Armenia na Azerbajan huku pande zote zikituhumiana kushambulia maeneo ya raia. Mnamo tarehe 5 Oktoba, maafisa wa jeshi la Armenia waliituhumu Azerbajan kwa kuilipua Stepanakert, mji mkuu wa Nagorno-Karabakh. Maafisa wa Azeri waliituhumu Armenia kwa kushambulia miji kadhaa, pamoja na miji miwili mikubwa, Ganja na Mingachevir. Karibu watu 250 wameripotiwa kuuawa katika mapigano hayo, lakini idadi halisi inatarajiwa kuwa kubwa zaidi kwani Azerbajan haijaelezea majeruhi wake wa kijeshi. Mapigano hayaonyeshi ishara ya kupungua, na Azerbajan inatoa wito kwa vikosi vyote vya Armenia kujiondoa katika eneo lake. Kimuundo Nagorno-Karabakh iko ndani ya mipaka inayotambuliwa kimataifa ya Azerbajan. Mzozo huo uligeuka kuwa wa ghasia kwa kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, na makumi ya maelfu waliuawa wakati wa mapigano mwanzoni mwa miaka ya 1990. Tangu kusitisha mapigano kutangazwa mnamo 1994, kiuhalisia Nagorno-Karabakh imefanya kazi kama serikali huru kwa msaada wa Kiarmenia. “Nagorno-Karabakh ni ardhi yetu. Tunapaswa kurudi huko, na tunafanya hivyo sasa,” Rais wa Azeri Ilham Aliyev alisema katika hotuba kali mnamo Jumapili. “Huu ndio mwisho. Tuliwaonyesha sisi ni kina nani. Tunawafukuza kama mbwa.”

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 08 Oktoba 2020 12:34
Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.