Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 23/05/2021

Vichwa Vya Habari:

Wapatanishi wa Misri wanajaribu kushawishi kusitisha mapigano kati ya ‘Israel’na Hamas

Pakistan Yahitaji Mafungamano ya Kimkakati, Mapana, Watunga Sheria wa Amerika Waambiwa

Katika Vitendo Viovu Zaidi Tangu Msikiti wa Babri Kuvunjwa, Waislamu wa India Wanahofu Huku Msikiti Mwingine Ukichomwa.

Maelezo:

Wapatanishi wa Misri wanajaribu kushawishi kusitisha mapigano kati ya ‘Israel’na Hamas

Wawakilishi wa Misri waweka juhudi zaidi katika kurefusha muda wa kusitisisha mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina Jumamosi hii, na maafisa wa misaada wametaka uwepo wa hali ya utulivu ili waweze kukabiliana na mzozo wa kibinadamu ulioikumba Gaza baada ya siku 11 za mapigano.  Usitishaji wa mapigano, ambao ulianza kabla ya jua kuzama mnamo siku ya Ijumaa, ulikuwa ukiendelea hadi siku ya Jumamosi jioni, umewawezesha maafisa kuanza kufanya tathmini ya madhara na uharibu uliotokea. Pamoja na makabiliano kati ya askari polisi wa Israel na waandamanaji wa Kipalestina katika eneo takatifu la Al-Qudsi Ijumaa hii, hakukuwa na taarifa yoyote ya urushwaji wa roketi za Hamas kutoka Gaza au shambulizi la anga kutoka Israel katika muda wote wa usiku au Jumamosi. Roketi ambazo huvurumishwa na Hamas na baadhi ya makundi mengine ya jihad zimedhoofisha miji ya kusini mwa Israel wakati wa mapigano, na kusababisha taharuki, lakini hazikuwa na madhara makubwa ikilinganisha na mabomu ya Israeli yanayovurumisha katika Ukanda wa Gaza. Maafisa wa Palestina wameweka gharama ya ujenzi mpya wa Gaza kufikia dolari milioni kumi, wakati huo huo maafisa wa afya wanasema watu 248 walikufa katika mapigano. Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuongezeka kwa hali mbaya ya kiafya na taharuki kubwa kufuatia kuharibiwa kwa miundombinu msingi kama nyumba, barabara, na mahospitali "kila mtu atulie na kutojiingiza katika vitendo vya kichikozi," Lynn Hastings, msimamizi mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu shughuli za kibinadamu katika mipaka ya wapelestina, aliyasema hayo alipokuwa eneo maalumu la jiji la Gaza alipokuwa akiongea na manusura. Misri baada ya kusimamia usitishaji wa mapigano, kwa msaada wa Amerika, imetuma ujumbe au uwakilishi maalumu kwenda Israel siku ya Ijumaa kujadili njia ya uimarishaji wa usitishaji mapigano, ikiwa ni pamoja na misaada kwa wapelistina wa Gaza, afisa wa Hamas aliliambia shirika la habari la Reuters. Ujumbe huo umekuwa ukifanya hivyo tangu kusitiswa mapigano kati ya Israel na Palestina, na siku ya Jumamosi ujumbe huo ulikutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas  katika jiji la Ramallah liliopo katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi, hayo yalisemwa na msemaji wa kiongozi wa Wapalestina. Chanzo kimoja kimesema kwamba Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Amerika Antony Blinken atatembelea Israel na eneo Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatano na Alhamisi, akitazamia kuwezesha usitishaji wa mapigano. Mahmoud, pamoja na kwamba anaushawishi mdogo katika eneo la Gaza, eneo linaloongozwa na Hamas. Raisi wa Amerika Joe Biden alisema siku ya Alhamisi kwamba Washington itafanya kazi pamoja na Umoja wa Mataifa kupeleka misaada ya kibinadamu na kusaidia kuijenga upya Gaza, na kwa usalama dhidi ya mifuko ya kifedha inayotumika kuimarisha Hamas kijeshi, ambayo hupelekea kuundwa kwa vikundi vya kigaidi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi lilitoa wito wa "Kushikana kamili" katika kusitisha mapigano na kutilia mkazo katika uwasilishwaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Palestina. [chanzo: Reuters]

Usitishaji wa mapigano hautatui tatizo la Palestina. Kinachohitajika ni majeshi ya Waislamu kuikomboa Palestina yote kufuatia ukaliaji haramu wa kimabavu unaofanywa na taifa la Kizayuni. Hili litawezekana tu kupitia nguvu ya kijeshi kupitia maafisa imara wa majeshi ya Kiislamu dunia nzima.

Pakistan Yahitaji Mafungamano ya Kimkakati, Mapana, Watunga Sheria wa Amerika Waambiwa

Siku ya Jumamosi Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi aliwaambia watunga sheria wa Amerika kwamba Pakistan ilikuwa ikitafuta msingi mzuri, urafiki wa kimkakati na Amerika, ambao ungesaidia pia Afghanistan. Katika mkutano maalumu na wanachama wa nyumba ya uwakilishi na maseneta, Waziri wa Mambo ya Kigeni alilialika kundi la watunga sheria wa Amerika kutembelea Pakistani 15 Juni kwa ajili ya mashauriano na uwakilishi wa Pakisatan kuona namna ya kuboresha uhusiano wao. Wakati wa kikao chake na wanachama wa bunge dogo la uwakilishi Asia na Pasifiki, Bw. Qureshi alisisitiza umuhimu wa “mpango msingi na mkubwa wa kimkakati wa kiurafiki” ambao utatizamia maslahi ya nchi zote, kauli ilithibitisha hayo baada ya kikao. “urafiki huo utaimarisha mahuisano ya nchi hizo pia utalinda maslahi ya pamoja katika ukanda wa Asia ya Kati,” alisema. Uimarishaji wa ukanda wa biashara na Maendeleo pia itakuwa ni jambo zuri kwa mshikamano wa kati ya Amerika na Pakistan, aliongezea. Waziri wa Mambo ya Kigeni aliongezea, juhudi za Pakistan za kutaka “uimara wa Amani ya kisiasa” nchini Afghan­istan. “Amani ya Afghanistan ni jukumu la wote makundi ya Afghan na wadau muhimu wa nje” alisema. Wanachama wa jumba ndogo la uwakilishi wameridhishwa na juhudi za Amani za Pakistan nchini Afghanistan na kuonyesha ukubwa wa nafasi ya kamati kati ya Pakistani na Amerika katika juhudi zake za kuimarisha uhusiano wa Amerika na Pakistan, kauli nyingine ilithibitisha hayo baada ya kikao. Katika kikao tofauti na kundi lingine la Watunga Sheria, Waziri wa Mambo ya Kigeni alijadili kuhusu umuhimu wa Amani ya kanda na usalama kusini mwa Asia na kushauri uimarishaji wa mahusiano ya watu na Amerika. Baadaye, Waziri wa Mambo ya Kigeni aliwaambia waandishi wa habari kwamba alijadili kuhusu hali ya Virusi vya Korona na watunga sheria wa Amerika, aliwaambia kwamba Nchi ina chanjo za kutosha kwa sasa lakini zitahitajika zaidi kwa ajili ya kupambana na mlipuko wa Virusi hivyo. Bw Qureshi ameshauri kudumisha kutembeleana mara kwa mara na kuzidi kuwajululisha hali ya kanda inavyo kwenda, haswa maendeleo ya Afghanistan. Kikao cha Waziri wa Mambo ya Kigeni na watunga sheria hao kilifuatia baada ya kusikilizwa ujumbe maalumu wa Afghanistan kulikofanyika Washington mwishoni mwa wiki. Wakati wa kusikilizwa, baadhi ya watunga sheria wa Amerika na mpatanishi mkuu wa Amerika nchini Afghanistan, Balozi Zalmay Khalilzad, ikijadili jukumu la Pakistan kuhusu mchakato wa Amani ya Afghan. Pia wamejadili malalamiko ya Rais wa Ashraf Ghani kwamba mchakato wa uletaji Amani nchini Afghanistan hivi sasa ulikuwa “mwanzoni na baadaye ni mpango wa kuipata Pakistan” kwa kuwa upunguzaji wa vikosi vya Amerika ungepunguza ushawishi wa Amerika katika nchi hiyo. “hivi sasa Amerika imejipunguzia jukumu. Jambo la Amani au uadi lipo katika mikono ya Pakistan hivi sasa,” Bw Ghani alisema. Mbunge  wa kike wa Congress Sara Jacobs, kutoka California kupitia chama cha Democrat, wakati wa kusikilizwa kwake alimnukuu  Bw Ghani na akamuuliza Balozi Khalilzad “ni kipi haswa unachofanya kuhakikisha” kwamba Pakistan itaendelea kuunga mkono mpango wa Amani wa Amerika? “nafahamu ndani ya Pakistan kuna changamoto, lakini naamini kwamba safari ya Jenerali Qamar Javed Bajwa kutembelea Kabul ilikuwa ina malengo mazuri. Walijadili hatua kadhaa ambazo pande mbili zinaweza kuzichukua… kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa nchi zote mbili…,” alisema. Mbunge wa Congress Ted Lieu, mwakilishi mwingine kutoka California kupitia chama cha Democrat mwanajeshi wa zamani wa jeshi la anga la Amerika mwenye cheo cha kanali, aliuliza kama Pakistan kulikuwa kuna umuhimu wa kufanikiwa mchakato wa Amani wa Afghan, kwa nini haukutiliwa maanani. “ni kutokuwa na heshima kutokumualika kiongozi wa  Pakistan katika mkutano mkuu wa kujadili hali ya hewa (uliofanyika Washington mapema mwaka huu) wakati ambapo viongozi wa India na Bangladesh walialikwa,” alisema. “ni kweli, upo sahihi. Pakistan ni nchi muhimu. Tumeshirikiana kwa kiwango kikubwa sana na Pakistan. Na Pakistan ina jukumu kubwa sana la kufanya nchini Afghanistan ili kuweza kuendelea na mambo mengine,” Balozi Khalilzad alijibu. [chanzo: Dawn]

Kwa kuzingatia ni mara ngapi Amerika imeisaliti Pakistan katika kila namna, ni aibu kubwa kiasi gani kisiasa kuendelea kutaka mpango mkakati wa pamoja. Tofauti na hivyo, Pakistan ni lazima uhusiano wake na Amerika na kushughulikia uhuru wa kiuchumi na sera za mambo ya nje.

Katika Vitendo Viovu Zaidi Tangu Msikiti wa Babri Kuvunjwa, Waislamu wa India Wanahofu Huku Msikiti Mwingine Ukichomwa.

Hofu imetanda katika jamii ya Waislamu wa kaskazini ya India baada serikali ya eneo hilo kukataa agizo la mahakama na kuvunja msikiti mkongwe wa karne katika eneo la Uttar Pradesh. Ubomoaji wa msikiti wenye umri wa miaka 112 katika mji wa Ram Sanehi Ghat wilaya ya Barabanki ilikuwa ni moja ya vitendo viovu dhidi ya jamii ya Kiislamu tangu kuvunjwa msikiti wa Babri Masjid karne ya 16 uliovunjwa na genge la kutoka mji wa jirani wa Mabaniani Ayodhya mwaka 1992. Hata ingawa agizo la mahakama limesimamisha mchakato wa ubomoaji mpaka tarehe 31 Mei, serikali ya eneo hilo ilivunja majengo siku ya Jumatatu baada ya kudai kwamba serikali ya mtaa ililivunja jengo hilo mnamo Jumatatu baada kutangaza kuwa "ni ujenzi ulio kinyume cha sheria." “huu ni msikiti ambao watu wamekuwa wakiutumia kwa ajili ya ibada kwa miongo kadhaa, na ubomoaji huo umepelekea hofu miongoni mwa watu kwa kuhofia kukamatwa kutokana na kupinga kwao,” mmoja wa wanakamati wa msikiti, Mohammed Nasim, “ilikuwa kuna umuhimu gani wa kuuvunja wakati ambapo nchi nzima ipo katika mapambano dhidi ya mripuko? alisema. Uttar Pradesh, ndio mji mkubwa na wenye umaarufu zaidi India, unaotawaliwa na Yogi Adityanath, mwanasiasa kutoka chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP), anayefahamika kwa chuki zake dhidi ya Uislamu. Serikali ya mtaa imepinga kutokea kwa uovu wowote, nimesema hakuna msikiti wowote uliobomolewa katika eneo hilo. “sifahamu kama kuna msikiti wowote uliobomolewa,” jaji wa wilaya ya Barabanki Dkt. Adarsh Singh aliiambia Arab News. “ilikuwa ni jengo lililojengwa kinyume na sheria.” Lakini Zufar Farooqui, mwenyekiti wa bodi ya waqfu wa wasunni eneo la kati la Uttar Pradesh, aliuliza akiwa anatoa malalamiko yake kwa jaji: “msikiti umekuwepo mbele ya mkaazi jaji mdogo wa wilaya kwa miaka mingi. Hili halipingiki. Vipi msikiti uwe ni jengo haramu? Wakati ulisajiliwa na bodi ya Sunni Waqf.” Tarehe 15 Machi, uongozi wa wilaya uliiuliza kamati ya msikiti ili kuthibitisha umiliki wake. Kamati ilisema imewasilisha nyaraka zote na siku hiyo hiyo ikaenda mahakama kuu kwa kuhofia msikiti “utabomolewa.” Mahakama ilisema uongozi wa wilaya ulikuwa bado una tafuta nyaraka. Kulingana na mchambuzi wa siasa anaye egemea kwa Lucknow Asad Rizvi, ubomoaji ulikuwa “shambulizi la kupingwa dhidi ya msikiti,” kwa sababu Ayodhya na Barabanki ni wilaya jirani. [chanzo: Arab News]

Serikali ya Modi ya BJP inatizamia kupunguza ushawishi wa Waislamu India kwa kufuta misikiti na kufanya maisha ya Waislamu nchini India kuwa magumu. Viongozi wa Kiislamu wa India hawafanyii maovu Mabaniani waliokuwa wengi kama wao wanavyofanyiwa.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.