Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 21/08/2021

Amerika na Serikali Yake Kibaraka ya Kabul Zashindwa nchini Afghanistan

Kwa kasi ya kushangaza, mujahidina wa Afghanistan waliifagia nchi hiyo na kulazimisha kuporomoka kwa serikali ya Kabul, huku rais wake akikimbia kimya kimya, ingawa, kulingana na Rais wa Amerika Joe Biden akizungumza mnamo Jumatatu, Waamerika walikuwa "wamelipa mafunzo imara na kulihami jeshi la Afghanistan la Wanajeshi 300,000 - wenye zana za kutosha – jeshi  kubwa zaidi kiidadi kuliko majeshi ya washirika wetu wengi wa NATO." Serikali ya Kabul ilianguka haraka mno kwa sababu ilikuwa ni mamlaka bandia yaliyoundwa tu kuficha mamlaka halisi, ambayo ni Amerika. Na yale yanayoitwa majeshi ya Afghanistan yaliporomoka haraka sana kwa sababu wao pia walikuwa ni jeshi bandia, lililoundwa kama nyongeza, kama pazia, kwa wanajeshi vamizi wa Amerika. Swali halisi basi sio kwa nini serikali bandia ya Kabul au vikosi bandia vya jeshi la Afghanistan vilianguka bali kwa nini Waamerika walilazimishwa kuachana na uvamizi wao wa kijeshi.

Katika kuviondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan, Amerika imeshindwa vibaya zaidi tangu ilipopanda wadhifa wa dola kuu yenye nguvu zaidi duniani baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Nchini Vietnam, Amerika bado iliweza kupata malengo makuu ya kimkakati katika maridhiano yake na China, hata kama haikuweza kufanikiwa kijeshi ndani ya Vietnam yenyewe. Lakini hakuna njia ya kuisifia kampeni yake ya Afghanistan isipokuwa kushindwa kubaya kiutendaji pamoja na kimkakati, kijeshi na kisiasa. Amerika imejua hili tangu muhula wa pili wa George W. Bush, rais ambaye ndiye aliyeamuru uvamizi huo, lakini Amerika iliendelea kuakhirisha kujiondoa kwa sababu ya fedheha ya kushindwa kwake, ikitumaini kwamba njia fulani huenda ingeweza kupatikana ili kufanikisha kwa namna fulani mafanikio kutoka kwake.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mnamo Ijumaa, Biden alikuwa bado anajaribu kutetea kujiondoa huko kwa watu wa Amerika walioshangazwa ambao walikuwa wameongozwa kuamini kutoshindwa kwa Amerika, dola kubwa zaidi na yenye nguvu zaidi, kwa kuregelea sababu iliyotajwa hadharani ya kwenda Afghanistan, "Kuna hatari kubwa kutoka ISIS na al-Qaida na washirika hawa wote katika nchi zengine - mno - kuliko ilivyo nchini Afghanistan. Tutabakisha uwezo wa upeo wa juu ambao ikiwa wataweza kurudi tena - tutaweza kuwatoa, kwa ustadi. ... Kwa hivyo hapa ndipo tunapaswa kuwa, hii ni kuhusu Amerika kuongoza ulimwengu, na washirika wetu wote wamekubaliana na hilo." Lakini uhalisia ni kwamba Amerika haikwenda Afghanistan kwa sababu ya kile Biden alichokiita "tishio kutoka kwa ugaidi". Ukweli ni kwamba, Amerika iliingia Afghanistan kwa sababu inatoa manufaa ya kipekee ya kistratejia, eneo la kipekee la kijeshi lililoinuka juu lililozungukwa na milima, ngome ya mwamba ya kimaumbile angani, yenye kuziona Asia Magharibi, Kati na Kusini huku pia ikitoa msingi imara dhidi ya mahasimu wote wa kimikakati wa Magharibi, Urusi pamoja na China. Afghanistan, au Khurasan kama inavyoitwa katika hadith ya Mtume (saw), inawakilisha moja ya zawadi kubwa kabisa za siasa ya kieneo lakini ambayo Amerika katika karne ya 21, mithili ya Muungano wa Kisovyeti katika Karne ya 20 na Uingereza katika Karne ya 19, imeshindwa kabisa kushikilia.

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu utainuka hivi karibuni na kusimamisha tena Dola yao ya Kiislamu la Khilafah kwa njia ya Mtume (saw), kama ilivyotabiriwa katika hadith sahih, ambayo itaunganisha ardhi zote za Waislamu, ikiwemo ile ya Afghanistan, itakomboa maeneo yaliyosalia yaliyokaliwa, itatabikisha Sharia ya Kiislamu, kurejesha mfumo kamili wa maisha ya Kiisilamu, na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima.

Kiongozi wa Taliban Akataa Demokrasia, Kanda Yajibu Mapinduzi Hayo

Huku Taliban wakiwa wangali katika harakati za kuimarisha udhibiti wa nchi, na bado hawajatoa maelezo kuhusu utawala wa Afghanistan, wameweka wazi kuwa wanakusudia huo uwe Sharia ya Kiislamu. Mmoja wa Makamanda wao, katika mahojiano na Reuters pia aliweka wazi kuwa Taliban hawatatabikisha demokrasia. Taarifa hizi zinapaswa kukaribishwa, hata kama Taliban bado hawajatoa ahadi yoyote ya kusimamisha Dola ya Khilafah. Hii ni kwa sababu demokrasia ni falsafa ya kigeni ya kikafiri ambayo hata Wakristo wa Magharibi walikuwa wameikataa na walilazimishwa tu kuibeba katika maridhiano na waasi wa kimada wa kikafiri, kama yale yaliyoonekana katika Mapinduzi ya Kifaransa na mapinduzi ya baadaye barani Ulaya mnamo 1830 na 1848, na ambayo yakawa maarufu kwa sababu ya unyonyaji wa raia wa kipote cha watawala wa Magharibi. Demokrasia inamtaka mwanadamu atunge sheria katika maisha yake, huku dini ya haki ikimtaka mwanadamu kuishi maisha yake kulingana na amri za Muumba wake. Fauka ya hayo, kipote cha watawala wa Magharibi waligundua kwa haraka kuwa demokrasia halisi ni jambo lisilowezekana kwa kuwa sheria ni mada ya kina na maalum ambayo idadi ya watu jumla haiwezi kuchangia kwa njia ya kisawasawa; kipote hicho cha Wamagharibi kwa hivyo kiliweza kuendelea kulinda maslahi yao na utawala wao wa jamii ya Magharibi chini ya kile wanachokiita 'Demokrasia ya Uwakilishi'. Demokrasia wala demokrasia ya uwakilishi kamwe hazihusiani na Uislamu, na ni Sharia ya Kiislamu pekee ndiyo inayopaswa kutabikishwa katika nchi za Waislamu. Taliban lazima iungwe mkono kwa kujitolea kwa hili. Lakini wakati huo huo, ni muhimu kuelewa kuwa tatizo la kimsingi la Umma wa Kiislamu katika zama hizi sio tu ukombozi wa maeneo yake yaliyokaliwa au utabikishaji wa ndani wa Sharia ya Kiislamu bali ni kutokuwepo kwa Dola ya Khilafah, na uwepo wa uongozi jumla kwa Waislamu wote, ambao wameamrishwa kuahidi utii kwa Khalifah mmoja. Mtume (saw) amesema,

«وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» 

Hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujilinda kwaye” na yeye (saw) amesema,  «إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ فَاقْتُلُوا الآخِرَ مِنْهُمَا»Wanapopewa ahadi ya utiifu (Bay'ah) makhalifa wawili muuweni yule wa pili kati yao”. Ni wabeberu makafiri ndio waliopatiliza fursa ya kugatuliwa kwa mamlaka kutoka katika mamlaka makuu ndani ya Ummah wa Kiislamu kutuzidi nguvu na kutugawanya kuwa mafungu ya vijidola vya kitaifa kwa muundo wa Westphalia wa Ulaya. Ummah wa Kiislamu ni lazima ukatae migawanyiko miongoni mwetu, na kuunda Dola moja ya Khilafah ambayo, kuanzia kusimamishwa kwake, itaingia katika safu za dola kuu kwa sababu ya ukubwa wake, idadi kubwa ya watu wake, wingi wa rasilimali zake, uwepo wa eneo lake la siasa za kijografia na mfumo wenye nguvu wa Kiislamu.

China pamoja na Urusi zimejitokeza kujaza ombwe lililoachwa na kujiondoa kwa Amerika. Kulingana na New York Times, China ilitoa taarifa mnamo Jumatatu, ikisema kwamba "inaheshimu haki ya watu wa Afghanistan kuamua kwa hiari hatima yao" na itaendeleza "uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na Afghanistan". Wakati huo huo balozi wa Urusi jijini Kabul alisema mnamo Ijumaa, "Kulikuwa na utawala mbaya ambao umepotea na watu wana matumaini. Wanasema hauwezi kuwa mbaya zaidi kwa hivyo unapaswa kuwa bora." China pamoja na Urusi zinafaidika na kushindwa kwa Amerika lakini wakati huo huo zinaogopa kwamba Afghanistan inaweza kuwa msingi wa jihad dhidi yao pia. China inaendelea kuikalia kwa nguvu Turkestan Mashariki, huku Urusi ikiendelea kutawala nchi za Asia ya Kati, ambazo hapo awali zilikuwa zinakaliwa na Umoja wa Kisovieti. Amerika pia inatafuta kuziingiza China na Urusi, ili kutoa udhibiti zaidi dhidi ya mwamko wowote wa Uislamu, na pia kuongeza uhasama wa China na Urusi kwa kila mmoja. Amerika itaendelea kusaidiwa kwa nguvu katika uingiliaji wake katika eneo hili kupitia Pakistan, ambayo inaendelea kufanya kazi kama msaidizi kwa sera ya kigeni ya Amerika. Ni Pakistan ndio iliyoiwezesha Amerika kuingia Afghanistan, na ni Pakistan ndio iliyoiwezesha Amerika kutoka kwa kutia shinikizo kubwa lisilohimilika kwa uongozi wa Taliban ili kuwalazimisha kuanza mazungumzo na Amerika. Ilikuwa ni shinikizo kutoka Pakistan, kwa maagizo ya Amerika, ndilo lililoilazimisha Taliban kujizuia kuingia Kabul kwa ushindi, wakitafuta badala yake "suluhu ya kisiasa" pamoja na chembechembe za iliyokuwa serikali ya vibaraka iliyoshindwa. Mnamo siku ya Jumanne, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan na Mkuu wa Jeshi Qamar Javed Bajwa waliuhakikishia ujumbe uliokuwa ziarani wa viongozi kutoka kwa serikali ya zamani ya Afghanistan, waliowasili siku hiyo hiyo ambayo Taliban iliichukua Kabul, kwamba Pakistan ingefanya kila kitu kwa ajili ya "suluhu ya pamoja". Suala la Afghanistan halitatatuliwa kikamilifu wakati Pakistan ikiendelea kutekeleza ajenda ya Amerika. Waislamu wa Pakistan lazima wanyanyuke na kuwapindua watawala wao vibaraka na urithi wa mifumo ya kikoloni ya Kiingereza na kusimamisha mahali pao kiini cha Khilafah ya Kiislamu ambayo itaunganisha kwake ardhi za Afghanistan na Asia ya Kati, ikomboe Turkestan Mashariki na Kashmir, na ipanuke hadi ulimwengu mzima wa Kiislamu, ikitoa uongozi mmoja jumla pekee kwa Umma mzima wa Kiislamu.

    أفغانستان#         #Afghanistan           #Afganistan

        

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu