Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 14/07/2021

Vichwa vya habari:

Erdogan Awasiliana na Umbile la Kizayuni

Taliban Wameshinda Vita vya Silaha Je, Sasa Watashindwa Vita vya Kisiasa

Mradi wa Ulaya wa Ukanda na Barabara

Maelezo:

Erdogan Awasiliana na Umbile la Kizayuni

Rais wa Uturuki  Recep Tayyip Erdogan amewasiliana na kiongozi mpya mwenza wa ‘Israel’, akimpongeza kwa kuingia madarakani na  kumkumbusha umuhimu wa uhusiano wao wa pande mbili. Erdogan alizungumza na Raisi mpya aliyeapishwa wa ‘Israel’ Yitzak Hertzog kupitia njia ya simu mnamo Jumatatu, 12 Julai. Wakati wa maongezi hayo ya simu, Rais wa Uturuki alisema alimsisitiza dori muhimu ambazo ‘Israel’ na Uturuki zinacheza katika kuhakikisha usalama na utulivu Mashariki ya Kati. Wawili hao pia walizungumzia kuhusu uwezekano wa "ushirikiano mkubwa" katika nyanja za kawii, utalii na teknolojia, Erdogan alisema baada ya maongezi hayo ya simu.  Hertzog alithibisha simu hiyo kupitia mtandao wa tweeter baadaye mnamo Jumatatu, akisema viongozi wote wawili "wamesisitiza kwamba ‘uhusiano kati ya 'Israeli’ na uturuki una umuhimu mkubwa kwa ajili ya usalama na utulivu Mashariki ya Kati" na kwamba " wamekubaliana kuendelea na mazungumzo ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo". Alikiri kwamba wakati uliopita kulikuwa hakuna mahusiano mazuri, Erdogan alisema mawasiliano kati Israel na Uturuki ni lazima yadumishwe bila kujali mzozo wowote utakaoweza kutokea siku za usoni. Akizungumzia kuhusu uhusiano wa Uturuki kwa ‘Israel’ mnamo Disemba, Erdogan alisisitiza kwamba kadhia hizo ziko katika orodha ya juu ya serikali hizo.

Taliban Wameshinda Vita vya Silaha Je, Sasa Watashindwa Vita vya Kisiasa

Huku Taliban ikichukua tena sehemu kubwa ya Afghanistan sera zake za kisiasa zinaanza kuonyesha umbile lake na kuonyesha dunia namna inavyopanga mahusiano na nchi zinazoizunguka na zile zilizo na maslahi nchini Afghanistan. Msemaji wa Taliban Suhail Shaheen alisema: “Tunawakaribisha (China). Kama wanataka kuwekeza na tunawahakikishia usalama wao. Usalama wao ni muhimu kwetu,” akiongea na gazeti la Morning Post la China ya Kusini. “Mara nyingi tumekuwa nchini China na tuna uhusiano mzuri na wao,” alisema. “China ni nchi ya kirafiki ambayo tunaikaribisha katika kuijenga upya na kuleta maendeleo Afghanistan.” Pia msemaji huyo waTaliban alisema kundi lake halitaruhusu "kundi lolote tenganishi, ikiwa ni pamoja na Harakati ya Kiislamu ya Turkistan Mashariki, kuendesha operesheni zake nchini Afghanistan. “Ndio, haitaruhusiwa. Watu kutoka nchi nyengine wanaotaka kuitumia Afghanistan kama eneo la (kuanzisha mashambulizi) dhidi ya nchi zengine, tumejizatiti kwamba hatutawaruhusu hata ikiwa ni mtu mmoja mmoa au kikundi cha watu dhidi ya nchi yoyote ikiwemo China. Huu ndio msimamo wetu chini ya makubaliano ya Doha. Tunashikamana na kauli hiyo.” Taliban imefanikiwa sana katika uwanja wa kivita, lakini siasa zao daima zinakosa kufahamu kuhusu mipango ya dola kuu za kiulimwengu na vibaraka wake kama Pakistan na Saudi Arabia. Maoni kuhusu China yanaacha maswali mengi, lakini Taliban wanatakiwa kuhakikisha hawashindwi vita ya kisiasa baada ya kushinda vita ya kijeshi.

Ukanda wa Ulaya na Mradi wa Barabara

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Muungano wa Ulaya wamepitisha  na kuendeleza mpango mkakati wa uwekezaji wa kilimwengu kwa mradi wa China wa Ukanda na Barabara. Mpango mkakati huo mpya uliotangazwa unaoitwa "Ulaya Iliyounganishwa na Ulimwengu", unahamasisha uwekezaji katika miradi inayoonekana kuiunganisha Ulaya na ulimwengu kuanzia 2022. "Una malengo makubwa ya kuweka kiunganishi katikati ya sera zetu za nje," Mwanadiplomasia mkubwa wa Muungano wa Ulaya Josep Borrell alisema wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mnamo Jumatatu, 12 Julai. "Tulianza kufanya hili miaka miwili iliyopita kupitia makubaliano yetu na  Japan. "Lakini inaonekana kana kwamba hivi sasa ni muhimu zaidi kwetu kutizama matatizo ya kuungana kwa upana zaidi na Mashariki ya Kati na kuzitarajia Asia ya Kati na China, lakini sio kwa mwelekeo huu huu na madhumuni haya haya iliyo nayo Chinakwa Mradi wa Ukanda na Barabara." Uunganishaji bora maana yake ni upanuzi wa silsila za thamani na upunguzaji wa utegemezi wa kimkakati kwa Muungano huo na washirika wake. Kwa muda mrefu Amerika imekuwa ikitaka kupambana na mipango ya kiuchumi ya China kwa kuwataka washirika wake kujenga miradi yao wenyewe ya kupambana nayo.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 08 Septemba 2021 16:42

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu