Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Nafasi Muhimu katika Siasa za Kimataifa
Kwa: Abdulrahman al-Ziuod
(Imetafsiriwa)

Swali

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Mwenyezi Mungu Mtukufu akusaidie ubebe kheri mikononi mwako na mwetu, na Mwenyezi Mungu atukirimu kwa Khilafah ya pili na atufanye sisi mojawapo ya mashahidi na wanajeshi wake.

Mada: Nafasi Muhimu katika Siasa za Kimataifa

Mtendaji na dola kuu hufafanua upeo wa kazi ambao wanaupa kipaumbele katika kupata maslahi yao, ambao huitwa "Nafasi Muhimu", vilevile chama hiki hufafanua uwanja wa kazi yake katika nchi moja au nchi kadhaa hadi imakinike barabara ndani yake na Dola ya Kiislamu iasisiwe. 

Swali: "Je, Khalifah anaye kuja, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, anapaswa kuunda nafasi muhimu kwa ajili ya Dola ya Kiislamu ambayo ataipa kipaumbele ili kueneza Uislamu duniani kupitia Da'wah na Jihad?" Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Jibu

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Mwenyezi Mungu akubariki kwa dua zako nzuri, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akubariki kwa kheri.

Ile uliyoiita "nafasi muhimu" katika maana ambayo umeiashiria katika swali lako ni muhimu mno kwa dola yoyote yenye ushawishi katika jukwaa la kimataifa … Dola ya Khilafah ni dola ya kimfumo, dola ya kiulimwengu, na sio dola ya kieneo pekee: kwa sababu itikadi yake ni itikadi ya kiulimwengu, kwa kuwa ni itikadi ya mwanadamu, na nidhamu yake ni nidhamu ya kiulimwengu kwa kuwa ni nidhamu ya mwanadamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

 (وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِلنَّاسِ بَشِيراً وَنَذِيراً)

“Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji.” [Saba: 28]. Al-Bukhari narrated from Jaber ibn Abdullah, the Prophet (saw) said:

«أُعْطِيتُ خَمْساً لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ مِنْ الْأَنْبِيَاءِ قَبْلِي نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ وَجُعِلَتْ لِي الْأَرْضُ مَسْجِداً وَطَهُوراً وَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلَاةُ فَلْيُصَلِّ وَأُحِلَّتْ لِي الْغَنَائِمُ وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ كَافَّةً وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ»...

“Nimepewa mambo matano ambayo hayakupewa nabii mwengine yeyote kabla yangu. -1. Nimepewa ushindi kwa utisho (kupitia Mwenyezi Mungu kuwatia hofu maadui zangu) kwa masafa ya muda wa mwezi mmoja. -2. Ardhi imejaaliwa kwangu kuwa ni msikiti na tohara, hivyo basi yeyote katika Ummah wangu itakapomfikia swala popote na aswali. -3. Na nimehalalishiwa ngawira. -4. Na alikuwa kila Mtume akitumilizwa kwa watu wake pekee lakini mimi nimetumilizwa kwa wanadamu wote. -5. Na nimepewa haki ya kuwashufaiya watu (Siku ya Kiyama).”

Ingawa Dola ya Khilafah huitazama dunia nzima na kuifanya dunia nzima uwanja wa sera zake na amali zake kama ilivyo onyeshwa katika hadith iliyo simuliwa na Ibn Majah katika Sunnah yake kutoka kwa Thawban (ra) aliyesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«زُوِيَتْ لِي الْأَرْضُ حَتَّى رَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الْأَصْفَرَ أَوْ الْأَحْمَرَ وَالْأَبْيَضَ يَعْنِي الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَقِيلَ لِي إِنَّ مُلْكَكَ إِلَى حَيْثُ زُوِيَ لَكَ...»

“Ardhi ilikunjuliwa kwangu mpaka nikaiona mashariki yake na magharibi yake, na nikapewa hazina mbili, ya manjano au nyekundu na nyeupe – akimaanisha dhahabu na fedha. Na nikaambiwa: ‘Hakika ufalme wako utapanuka kwa kadri ya vile ulivyo kunjuliwa.’...”

Lakini, hii haimaanishi kuwa mipango iliyo wekwa na Dola ya Khilafah katika sera ya kigeni iko sawa kwa dola zote, wala haimaanishi kuwa nchi zote na maeneo yote ulimwenguni yatapokea umakinifu sawa kutoka kwa Dola ya Khilafah, bali, Dola ya Khilafah huunda nafasi muhimu kwa ajili yake kwa mujibu wa manufaa ya Da'wah ya Kiislamu na maalumati ya kisiasa, kiuchumi na kijeshi yaliyopo, na kutafuta zaidi kunali sera zake na kwa namna angavu zaidi katika nafasi muhimu ambayo imejifafanulia… Nafasi muhimu hiyo hubadilika kwa kutegemea kupatikana kwa malengo, kubadilika kwa uhalisia na maslahi ya Da'wah, na kadhalika.

Kwa kufuatilia sera ya Mtume (saw) na maswahaba wake watukufu, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, ni wazi kuwa Mtume (saw) alilifanya Bara Arabu kuwa ndio nafasi muhimu ya dola baada ya yeye (saw) kuiasisi mjini Madina. Na kisha muda mfupi baada ya kupata ushindi mwingi katika Bara Arabu, alipanua nafasi muhimu ya dola hiyo kujumuisha mipaka ya Ash-Sham na Iraq. Kisha Makhalifah waliokuja baada yake wakapanua nafasi muhimu ya dola baada ya ukombozi mwingi na kujumuisha Syria, Iraq, Fursi, Misri, Afrika Kaskazini, na kwengineko… Hivyo basi, nafasi muhimu ya Khilafah ilibadilika na kupanuka kwa mujibu wa ushindi uliopatikana na dola hiyo na mabadiliko ya maalumati na dhurufu.

Hivyo basi, pindi Dola ya Khilafah ya Pili itakapo simama, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itarudisha urithi wa dola ya kwanza ya Uislamu, ipendapo Mwenyezi Mungu. Itaunda mipango na kuchora mikakati inayostahili na kubuni nafasi muhimu inayo afikiana na maslahi ya Da'wah, maalumati na takwimu… Na itachukua hatua na mbinu muwafaka ili kuubeba Uislamu na kuueneza ulimwenguni ikizingatia nafasi muhimu iliyojiundia, na itaitathmini nafasi hii muhimu kwa mujibu wa maslahi ya Da'wah na mabadiliko ya takwimu zinazojiri, Mwenyezi Mungu akipenda. Kitabu cha Dola ya Kiislamu kinaeleza katika mlango: “Sera ya Kigeni ya Dola ya Kiislamu,” katika uzingatiaji wa dola wa takwimu zilizoko katika kuunda kwake mipango na mbinu ili kunali sera zake:    

 [Hivyo basi, fikra ya kisiasa ambayo kwayo uhusiano wa Dola na dola nyenginezo hujengwa juu yake ni kueneza Uislamu miongoni mwao na kubeba Risala hiyo kwao. Njia ambayo inapaswa kufuatwa ni Jihad. Lakini, kuna mbinu nyingi na mipango mingi ambayo Dola huanzisha au kutabanni. Kwa mfano huenda ikatia saini mkataba wa ujirani mwema na baadhi ya maadui na kupigana na wengine. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliidhinisha hatua kama hizi tangu kuwasili kwake (saw) mjini Madina. Dola yaweza kutangaza vita dhidi ya maadui zake wote kwa pamoja. Abu Bakr alifanya hivyo alipoyatuma majeshi hadi Iraq na al-Sham kwa wakati mmoja. Dola yaweza kukubali mikataba ya muda tu, ili kuiwezesha kuunda rai jumla kwa matokeo fulani yanayo hitajika. Hivyo ndivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyo fanya wakati yeye (saw) alipotia saini mkataba wa Hudaybiyah… Dola pia yaweza kutia saini mikataba ya kiuchumi na baadhi ya nchi, huku wakati huo huo ikikosa kuwa na mahusiano ya kibiashara na nyenginezo, ikizingatia maslahi ya Da'wah kwa Uislamu. Yaweza kuwa na mahusiano ya kidiplomasia na baadhi ya nchi, na kukosa kuwa nayo kwa nyenginezo. Hii itakuwa kwa mujibu wa mpango ulioundwa kwa uangalifu ili kuipeleka Da'wah katika mwelekeo mzuri. Dola yaweza kuchagua propaganda na matangazo ili kueneza Da'wah, au yaweza kutumia njia ya kufichua njama za maadui na mbinu za vita baridi. Upangaji wa Dola utakuwa kwa mujibu wa maumbile ya kazi itakayostahili kufanywa na kuendeshwa kufikia manufaa ya Da'wah ya Kiislamu… Lakini yote haya ni kwa lengo la kueneza Uislamu kupitia njia isiyo badilika, ambayo ni Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu.] Mwisho.  

Hivyo basi, uundaji nafasi muhimu ya dola haiko tofauti sana na yale yaliyo nukuliwa hapa kutoka katika kitabu cha Dola ya Kiislamu.

Tafadhali pokea salamu zangu.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

25 Dhul Hijjah 1440 H

26/08/2019 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu