Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  12 Rajab 1441 Na: 1441/06
M.  Jumamosi, 07 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Kumbukumbu ya miaka 99 ya Kuvunjwa kwa Khilafah,
Enyi Waislamu, Isimamisheni, ambayo kwayo ni Izza, na kupitia kwayo Tunarudisha Hadhi yetu Miongoni mwa Watu na Mataifa
(Imetafsiriwa)

Kumbukumbu ya maumivu inapita siku hizi, ambayo ni kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah kupitia mhalifu wa karne hii, Mustafa Kemal, tarehe ishirini na nane Rajab 1342 H, sawia na Machi 3, 1924 M. Kuvunjwa kwa Khilafah ilikuwa ni janga liso kifani ambapo biladi za Kiislamu zilitikisika kwalo, na kiongozi wa malenga, Ahmed Shawqi aliiomboleza kwa mashairi ya huzuni yanayo tona damu, ambayo alisema:

Ulivishwa sanda usiku wa harusi, na ukazikwa alfajiri
Minara na majukwaa yalipiga kelele kwa ajili yako, na falume na waombolezaji walilia kwa ajili yako India iliomboleza sana, na Misri inahuzunika, zinakulilia kwa machozi

Tunaukumbusha Ummah juu ya mateso haya makubwa na tukio lenye uchungu ambalo limewakumba na kuwafanya waporwaji na maadui zake bila ya mchungaji wa kweli kuzuia maovu yao, bila ya Khalifah msafi mchamungu, ambaye nyuma yake mnapigana na kujihami, hadi tulipokuwa mayatima kwenye meza ya mabwana walafi, na mataifa yalikusanyika dhidi yetu kama vile watu wanavyoitwa kwenye karamu, hivyo Palestina ilipotea na kwa hivyo dada zake, na mambo yetu yalikabidhiwa Ruwaibidat wachache (watawala wajinga wasio na uwezo), ambao hawazingatii ahadi wala heshima yoyote kwetu sisi, ni wenye nguvu dhidi yetu, wanyenyekevu kwa Makafiri. Tunapo ukumbusha Ummah kuvunjwa kwa Khilafah yao, pia tunawakumbusha kuwa kurudi kwake ni moja ya faradhi kubwa, na kujiweka mbali nayo ni moja ya madhambi makubwa. Muislamu katu haepuki dhambi hilo isipokuwa kwa kufanya kazi kwa bidii kulisimamisha taji lililopotea la faradhi zote: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Kinachowatishia Wamagharibi na vibaraka wao ni Ummah kurudi katika Uislamu wake, kwani Ummah umechochewa na kulemaa kwake na umevunja kizuizi cha uoga, kuasi dhidi ya watawala wake ambao wamewekwa na Wamagharibi kwenye shingo zao, na ambao wamewatesa kwa mateso mabaya zaidi, na kwamba ingawa Wamagharibi wameweza kuyadhibiti mapenduzi mengi yaliyo ibuka katika biladi za Waislamu na kuyazunguka na kisha kuyatibua, lakini Ummah umeanza kuhisi njia ya Uamsho wake, na haitachukua muda mrefu kurudilia zamu nyengine tena ili kuziangusha zile serikali za kisekula za kikafiri na kuwatupa watawala hawa sehemu ya mbali.

Muundo ambao taifa hili litaufuata katika njia ya uamsho wake ni muundo wa Khilafah Rashida, sio tu kwa sababu ilipata mafanikio yaso kifani katika nyanja zote za kiuchumi, kisayansi na umoja, lakini pia kwa sababu imejengwa juu ya itikadi ya kiakili na kisiasa ambayo kwayo nidhamu imechimbuka, na kabla ya hilo kwa sababu ndio nidhamu ambayo Mola wa Walimwengu wote ameiridhia kwa Ummah huu, muundo ambao ulianzishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye alithibitisha ufaradhi wake kupitia Hadithi sahihi, na Maswahaba zake, radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie, walikubaliana kwa pamoja juu yake, na kisha wakaufuata, kwa hivyo waliifanya dola hii, kuwa dola ya kwanza ulimwenguni katika rekodi ya kipindi cha muda mrefu katika zama za kuunda mataifa.

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ)

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya akhera ni chache ” [At-Tawba: 38]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Misri

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.