Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  15 Safar 1442 Na: 1442/06
M.  Ijumaa, 02 Oktoba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali NchiniTunisia Inaendelea katika Sera ya Kugandamiza Dhidi ya Shughuli za Hizb ut-Tahrir "Wala msikae katika kila njia mkitisha watu, na kuwazuilia na Njia ya Mwenyezi Mungu wale wenye kumuamini, na mkataka njia ipotoke." [Al-A'raaf: 86]

Kabla ya kikao cha majadiliano kilichoandaliwa na jarida la Al-Tahrir mnamo Alhamisi 01 Oktoba 2020 saa kumi jioni katika makao makuu ya Hizb ut-Tahrir yaliyo katika makutano ya Soukra-Ariana chini ya anwani: "Uhalifu nchini Tunisia, jambo la dharura au janga la serikali?", Wageni wa kikao hicho walishangazwa ghafla na nukta ya usalama iliyofunga njia ya pekee ya kuelekea katika makao makuu ya Hizb.

Na pindi walipoulizwa kuondoka mahali hapo ili wageni na vyombo vya habari vijiunge na kikao hicho, maafisa wa usalama walikataa, wakidai kwamba hatua hii ya usalama ilikuwa imepangwa kabla na haiwezi kuvunjwa bila kushauriana na idara, na Baada ya mabishano kati yao na wanachama wa Hizb ut-Tahrir, waliondoka mahali hapo baada ya kusababisha kuchelewesha kwa matangazo ya moja kwa moja kwa nusu saa.

Hakika sisi, katika Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia, tunapinga kuendelea kwa serikali nchini Tunisia na washirika wake kutekeleza sera ya Rais wa zamani Beji Caid Essebsi kuzuia shughuli za Hizb ut-Tahrir kwa kutumia njia mbaya zinazotukumbusha polisi wa kisiasa wa Rais aliyeng'olewa Ben Ali, na tunasisitiza kuwa njia kama hizo duni hazitaidhoofisha Hizb ut Tahrir kutokana na kuendelea na shughuli zake Ili kutimiza lengo lake la kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo ndani yake matakwa ya Waislamu nchini Tunisia yatatimizwa kupitia kutabikisha mfumo wa Uislamu kwa Waislamu katika nchi zao za Kiislamu, ili kuwawezesha kurudisha ubwana, usalama na utajiri wao baada ya ukoloni katili ambao umeangamiza kilimo na kizazi na kutawala juu ya utajiri wa nchi na riziki za watu.

﴿وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ﴾

"Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka." [Ash-Shu'araa: 227]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.