Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan Maoni ya Habari
19 Aprili 2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni Demokrasia... Simamisheni Khilafah

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Amin.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 28 Ramadhan al Mubarak 1444 H sawia na 19 Aprili 2023 M

Mipaka ya Kitaifa baina ya Waislamu ni Ala ya Kiloni

Pindi Waislamu wanapodai kuhamasika kwa vikosi vyao vya kijeshi ili kuzikomboa Ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu, watawala husisitiza kuheshimiwa kwa mipaka ya kitaifa. Baada ya kuivunja Khilafah, wakoloni waliweka mipaka ya kitaifa baina ya Waislamu. Waliwagawanya na kuwadhoofisha Waislamu, ili kuhakikisha ukaliaji kimabavu wa ardhi zao. Katika Uislamu, hakuna mipaka ya kitaifa kati ya Ardhi za Waislamu. Khilafah ni dola moja kwa Waislamu wote, kuanzia Srinagar hadi Al-Quds. Itaikomboa Kashmir Inayokaliwa kwa mabavu na Msikiti wa Al-Aqsa.

Alhamisi, 22 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 13 Aprili 2023 M

Pakistan Yahitaji Katiba Iliyovuliwa kutokana na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume

Miaka 50 ya katiba ya 1973 imethibitisha kuwa katiba, iliyojengwa juu ya msingi wa hawaa na matamanio ya bunge, imefeli. Makundi yenye nguvu yanaitumia sheria ili kupata maslahi yao, kwa gharama ya watu. Ni wakati sasa wa kutabikisha katiba ambayo mfumo wake na kila kifungu chake kinatokana na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Ndiyo njia pekee ya uhuru, kuhakikisha kuwa katiba haina urithi na ushawishi wowote wa wakoloni.

Ijumaa, 23 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 14 Aprili 2023 M

Ripoti ya Ikulu ya White House kuhusu Kujiondoa kwa Fedheha kutoka Afghanistan Inafichua Udhaifu

Mnamo tarehe 6 Aprili 2023, Ikulu ya White House ilitangaza kutolewa kwa ripoti yake "Kujiondoa kwa Marekani kutoka Afghanistan." Katika ripoti hiyo, serikali ya Kidemokrasia iliituhumu serikali iliyopita ya Republican kwa "miaka minne ya mapuuza." Ripoti hiyo ni ukumbusho wa mgawanyiko mkali wa vyama viwili nchini Marekani, pamoja na uthibitisho kwamba Jeshi la Marekani limelemazwa na uoga. Badala ya kudumisha mivutano na Afghanistan, Khilafah itafanya kazi ya kuziunganisha dola zote za sasa za Waislamu kuwa dola moja yenye nguvu, ili kukabiliana na maadui wa kweli wa Umma wa Kiislamu.

Jumamosi, 24 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 15 Aprili 2023 M

Ni Wakati sasa wa Kuepukana na Jumuiya ya Kimataifa na UN Kikamilifu

Kwa kukubali kuhudhuria mikutano ya G-20 huko Srinagar na Leh, dola za Kimagharibi na jumuiya ya kimataifa zimeidhinisha ukaliaji kimabavu wa India wa Kashmir kinyume cha sheria. Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikiunga mkono tawala zinazokalia kwa mabavu dhidi ya Waislamu, iwe ni Palestina au Kashmir. Ni wakati wa kuachanana kabisa na Umoja wa Mataifa. Waislamu lazima wamtegemee Mwenyezi Mungu tu na nguvu zao wenyewe. Ni Khilafah ndiyo itakayoikomboa Palestina na Kashmir zinazokaliwa kwa mabavu, kupitia Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ﷻ kupitia majeshi ya Waislamu.

Jumapili, 25 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 16 Aprili 2023 M

Kuna Fursa kwani Marekani Imeelekeza Macho Yake Mbali na Ulimwengu wa Kiislamu

Mnamo tarehe 11 Aprili 2023, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan, alimwita Mfalme Mtarajiwa wa Saudia. Taarifa kwa vyombo vya habari ya ikulu ya White House ilisema wito huo ulilenga "mwenendo mpana wa kupunguza mizozo katika eneo hilo." Amerika inajaribu kutuliza mizozo katika Mashariki ya Kati, huku ikielekeza macho yake kwa China na Urusi. Inatafuta msaada kutoka kwa vibaraka wake katika Ulimwengu wa Kiislamu katika mizozo yake mipya. Badala ya kutumiwa na Marekani tena, ni wakati wa kuchukua fursa hiyo na kusimamisha tena Khilafah.

Jumatatu, 26 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 17 Aprili 2023 M

Kinachoitwa kuwa Uchafu Hubainishwa na Wahyi wa Mwenyezi Mungu , Sio Mwanadamu!

Katika kujibu malalamiko ya umma dhidi ya tamthilia ya "Jalan," mnamo tarehe 13 Aprili 2023, Mahakama ya Upeo ilitangaza kwamba uchafu ni kile ambacho "kinaharibu viwango vinavyokubalika vya adabu." Kwa hivyo, uchafu, ambao vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali huufanya kuwa kawaida, utakubalika. Katika Uislamu, uchafu ni kwa mujibu wa yale ambayo Wahyi wa Mwenyezi Mungu umekataza, na sio yale ambayo matamanio ya mwanadamu yameruhusu. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume pekee ndiyo itakayomaliza utumwa wa akili ya mwanadamu, kupitia kuweka utumwa kwa Mwenyezi Mungu ﷻ.

Jumanne, 27 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 18 Aprili 2023 M

Mgogoro Halisi wa Kimahakama ni Uwepo wa Sheria ya Anglo-Saxon na Kukosekana kwa Sheria ya Kiislamu

Kile ambacho kipote cha watawala wanakielezea kama mgogoro wa kimahakama ni mvutano juu ya mamlaka. Matokeo yake ni kuamua kibaraka mpya wa ukoloni wa Marekani. Ni matunda uchungu ya urithi wa sheria ya wakoloni wa Uingereza. Mgogoro halisi wa mahakama ni kwamba haukujengwa juu ya sheria za Kiislamu, hivyo kutotawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ﷻ. Ni idara ya mahakama ya Khilafah ndiyo itakayohakikisha uadilifu wa haraka na uwajibikaji wa Khalifa mwenyewe na kila mtawala anayemteua.

Jumatano, 28 Ramadhan al Mubarak 1444 H - 19 Aprili 2023 M

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.