Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Msafara wa Uthabiti kati ya Khiyana ya Utawala wa Misri na Wajibu wa Jeshi lake kuchukua Hatua

(Imetafsiriwa)

Na: Ustadh Said Fadil*

Huku kukiwa na mikutano tasa na makongamano ya uhadaifu, msafara maarufu unaojiita "Msafara wa Uthabiti" ulitoka Tunisia, Algeria, na Morocco, kuelekea Gaza kupitia Libya na Misri, kwa lengo la kuvunja mzingiro na kusaidia watu wa Ukanda wa Gaza, ambao wamekuwa chini ya vikwazo kwa zaidi ya miezi kumi na nane. Msafara huo uliwabeba wanaume na wanawake wa rika zote, waliounganishwa kwa lengo moja: kuvunja mzingiro huu uliowekwa na umbile la Kiyahudi kwa watu wa Gaza, kwa ushirika na ushiriki wa moja kwa moja wa tawala zilizo jirani, hasa unaoshikilia bendera kati yao utawala wa Misri.

Hata hivyo, mara tu msafara ulipokaribia mpaka wa Misri, ukweli mchungu ulifichuka kwa mara nyengine tena. Utawala wa Misri sio lango la wokovu, lakini ni mshirika katika uhalifu. Ulizuia msafara huo kuingia Misri, uliwaweka kizuizini washiriki wake nchini Libya, kuwanyang'anya simu, kuzuia mawasiliano na kuwalazimisha baadhi ya washiriki kurudi. Ni tabia inayomstahiki adui pekee. Kwa hivyo, matukio hayo yalijirudia, yakithibitisha kwamba Gaza sio tu inazingirwa na umbile la Kiyahudi, bali pia imezingirwa na tawala za Kiarabu, chini ya dhamira rasmi ya kisiasa, uratibu wa kufedhehesha wa usalama, na ushirikiano usioyumba wa kimataifa.

Msafara huo haukuwa umebeba silaha wala kurusha roketi. Ulikuwa ni mpango maarufu unaoashiria uungwaji mkono kwa watu waliozingirwa wa Gaza. Hata hivyo utawala wa Misri uliuchukulia kana kwamba ni tishio kubwa la usalama! Je, kuinusuru Palestina, hata kwa maneno, imekuwa ni uhalifu? Je, kuonyesha mshikamano na Gaza imekuwa ni kosa linalohitaji ukandamizaji na kuwekwa kizuizini?!

Kilichotokea kwa Msafara wa Uthabiti bado ni jinai nyengine iliyoongezwa kwenye rekodi rasmi ya usaliti wa tawala za Kiarabu, unaoshika bendera miongoni mwao ni utawala wa Sisi nchini Misri, ambao hauachi kutangaza ahadi yake kwa usalama wa Mayahudi. Unajivunia uhusiano wake na uongozi wa uvamizi huo, huku ikikabiliana na mtu yeyote anayesubutu kunyosha mkono wa msaada kwa Gaza na watu wake.

Msimamo wa kweli hupimwa uwanjani, sio kwa kauli mbiu. Uwanjani, uhalisia ni kwamba hakuna mpaka unaofunguliwa, hakuna askari anayepelekwa, na hakuna mzingiro unaovunjwa isipokuwa kwa amri ya Washington.

Hapana shaka kwamba Msafara wa Uthabiti unaakisi hali ya ikhlasi ya kweli ya watu, na unathibitisha kwamba kadhia ya Palestina ni kiini cha Umma. Ni sababu ya Ummah na inabaki hai moyoni mwake. Hata hivyo, ukweli ambao lazima usemwe wazi ni kwamba misafara ya misaada ya kibinadamu, haijalishi ni mikubwa kiasi gani, hailing'oi umbile linalokalia kwa mabavu, haikomboi ardhi, haisitishi milipuko ya mabomu, na haiondoi mzingiro.

Uislamu umebainisha wazi kwamba kuwanusuru wanaodhulumiwa ni faradhi ya Shariah kwa wale wenye uwezo na nguvu, sio juu ya wale ambao hawana chochote isipokuwa kauli mbiu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto…” [Surah An-Nisa 4:75]

Kwa hivyo ni nani anayezungumziwa katika ayah hii tukufu? Ni watu wenye nguvu na uwezo: jeshi la Misri, jeshi la Jordan, jeshi la Uturuki, jeshi la Pakistan, na majeshi yote ya Waislamu, askari zaidi ya milioni 5, wakiwa na silaha za kutosha kuangamiza umbile la Kiyahudi ndani ya muda wa siku chache, laiti kungekuwa na uongozi wa kweli.

Hata hivyo, badala ya kuelekea Al-Quds, tunaona majeshi haya yakiwazingira watu wao wenyewe, yakikandamiza misafara, na kulinda mipaka ya umbile la Kiyahudi dhidi ya hasira za watu wengi.   

Kinachotokea leo ni kielelezo wazi cha ushirika wa tawala na muungano wao na uvamizi huo. Badala ya Misri kuwa lango la nusra na kuondoa mzingiro, imekuwa mlinzi wa gereza kwa niaba ya uvamizi. Badala ya jeshi la Misri kuwa upanga dhidi ya Mayahudi, limekuwa ulinzi wa mipaka yao na msaidizi katika kutekeleza mzingiro wa Gaza.

Enyi wanajeshi wa Misri, enyi watu wenye nguvu na uwezo:

Je, Gaza haistahili kuinuka kwa ajili yake?

Je! damu ya mashahidi wake na vilio vya mama zake waliofiwa, wajane, watoto na wazee wake havikuitini?

Je, Palestina si imani juu ya mabega yenu? Je! watu wake sio ndugu zenu, na nusra kwao sio wajibu juu yenu?

Je, amri za Mwenyezi Mungu (swt) haziko juu ya amri za wakubwa zenu?!

Kuinusuru Palestina hakuhitaji kauli. Kunahitaji vifaru.

Hakuhitaji shutma. Kunahitaji maamuzi kufungua njia.

Hakuhitaji kivuko cha mpaka kufunguliwa kwa siku moja au mbili. Kunahitaji vita kamili na vipana vya ukombozi (tahrir).

Nyinyi ndio mnaoitwa leo kuunusuru Umma, kuwaondoa watawala wa khiyana, na kubeba mradi wa Ummah, Khilafah, kusimamisha utawala wa Uislamu, kukusanya majeshi, na kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt).

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi …” [Surah An-Nur 24:55]

Msafara wa Uthabiti, licha ya yote yaliyotokea, ni kofi usoni mwa tawala. Ni uthibitisho mpya kwamba sababu ya Palestina ingali hai katika nyoyo za Ummah. Aidha, pia ni wito wa kuamsha. Wakati umefika kwa Waislamu kuvuka hatua ya “huruma” na kuingia katika hatua ya utendaji mkali: kubadili tawala, kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu, kuhamasisha majeshi, kuvunja mzingiro, na kukomboa ardhi.

Kwa hivyo musiache damu ya mashahidi, vilio vya kina mama, au mayowe ya watoto yapotee kwenye korido za makongamano, au katika njia ya kuomba omba kutoka kwa serikali za khiyana. Badala yake, ufanyeni Msafara wa Uthabiti kuwa cheche ya mabadiliko ya kweli, ukombozi (tahrir) wa Palestina, na kusimamishwa kwa Khilafah.

Ee Mwenyezi Mungu (swt), tusimamishie dola ya Kiislamu bila ya kuchelewa, dola itakayoikomboa Al-Masjid Al-Aqsa, kuvunja msiko wa Mayahudi, na kuwaunganisha Waislamu chini ya bendera ya Uislamu, chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah An-Anfal 8:24]

* Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Gazeti la Ar-Rayah Toleo Na. 552

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.