Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Bajeti Mpya ya Misri ni Kati ya Tarakimu Zinazopotosha na Ukweli Usiokuwepo
(Imetafsiriwa)

Na: Ustadh Mahmoud Al-Laithi*

Mnamo tarehe 16 Juni 2025, Mbunge wa Misri Diaa El-Din Dawood alipinga rasimu ya bajeti kuu ya mwaka wa fedha wa 2025/2026, akionyesha kuwa serikali inadai kupunguza deni la umma, wakati takwimu zinaonyesha kinyume chake. Alibainisha kuwa deni la ndani na nje limeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2018, na kufikia jumla ya pauni trilioni 11.5 za Misri mwezi Juni 2024. Alieleza kuwa mikataba iliyotangazwa na serikali haitafsiri matokeo yanayoonekana kwa wananchi, akikosoa kuendelea kwa matumizi ya sera hizo hizo za kiuchumi. Pia alieleza kuwa mapato ya deni na malipo ya awamu pekee katika bajeti mpya yanafikia karibu pauni bilioni 4,382.6 za Misri.

Katika kikao cha hadhara cha bunge la Misri, mbunge Diaa El-Din Dawoud alitoa kauli muhimu alipokuwa akipinga kwa uthabiti bajeti kuu mpya ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026. Alifichua mkanganyiko mkubwa kati ya madai ya serikali ya kupunguza deni la umma na takwimu rasmi, ambazo zinaonyesha kupanda kwa hatari kwa deni la ndani na nje, na jumla ya deni la umma kufikia karibu pauni trilioni 11.5 za Misri. Dawoud alielezea kinaya kinachoumiza kwamba Wamisri hawaoni mabadiliko, licha ya mazungumzo ya mara kwa mara ya mikataba na uwekezaji.

Licha ya umuhimu wa misimamo hii, inabakia tu katika uchunguzi wa juu juu wa dalili za ugonjwa, bila kushughulikia mzizi wa ugonjwa, kupinga tu sera bila kuhoji mfumo wa kibepari unaozalisha bajeti hizi nzito kwanza. Kwa hiyo, ni faradhi ya Kisharia kwa Ummah kuwasilisha ruwaza ya kimsingi ya Kiislamu ya kushughulikia fedha za umma, upangaji bajeti, na deni la umma ili kutofautisha haki na batili, na masuluhisho ya kweli kutoka kwa masuluhisho ya viraka tu.

Bajeti ya Misri inatokana na mtindo wa kibepari kikamilifu, unaosimamiwa na makubaliano na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, ambapo serikali inakuwa chini ya maagizo ya nje kwa kisingizio cha "mageuzi ya kiuchumi." Katika mtindo huu, bajeti inageuka kuwa chombo cha kukusanya kodi na kulipa madeni, badala ya kujali mambo ya watu, kuhakikisha haki zao, na kutimiza mahitaji yao.

Mapato ya kodi yanachukua zaidi ya 85% ya jumla ya mapato ya umma, ambayo ni njia isiyo halali ya ukusanyaji kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu, kwani haitokani na hukmu za Shariah kuhusu vyanzo vya fedha vya dola.

Gharama za deni pekee hutumia zaidi ya 65% ya bajeti katika mfumo wa malipo ya awamu na mapato ya riba. Hii ina maana kwamba serikali inafanya kazi kama mpatanishi wa kulipa mikopo ya riba, badala ya kuwa mlinzi wa mambo ya watu.

Muundo huu unaonyesha kuwa dola ya Misri haitekelezi utawala wa kweli, lakini badala yake inafanya kazi kama wakala mtendaji kwa maslahi ya wakopeshaji wa kigeni chini ya kivuli cha mageuzi, wakati maskini wanazidi kuwa maskini na rasilimali za watu zinaporwa chini ya bendera ya uwekezaji.

Serikali ilidai kuwa inaelekea kupunguza uwiano wa deni kwa Pato la Taifa, lakini takwimu zinakinzana na dai hilo. Deni la ndani lilipanda kutoka trilioni 3.4 hadi pauni trilioni 8.7 za Misri katika miaka sita, na deni la nje kutoka pauni bilioni 844 hadi pauni trilioni 3.7, sawa na ongezeko la karibu mara tatu la jumla ya deni. Hali hii haiakisi tu usimamizi mbaya wa fedha, bali pia ukosefu kamili wa kuzingatia kanuni za Kiislamu. Riba imeharamishwa kimsingi katika nususi za Kiislamu, na kukopa kutoka kwa makafiri ni haramu sio tu kwa sababu inahusisha riba, bali kwa sababu inaiweka dola katika utiifu wa kisiasa na kiuchumi, ambao umeharamishwa katika Uislamu, kwani unajumuisha kuwategemea makafiri kwa njia inayopelekea kutawala kwao.

Dawoud alikosoa mikataba iliyotangazwa na serikali kwa kukosa matokeo yanayoonekana na yuko sahihi. Hata hivyo, kiuhalisia, hii si mikataba ya kimaendeleo; badala yake, ni ubadilishanaji ubwana unaofuja mali ya serikali kwa kisingizio cha uwekezaji. Kubinafsisha makampuni ya umma yenye faida kama vile Kampuni ya Heliopolis, Arabian Cement, Banque du Caire, pamoja na maeneo ya gesi na maeneo ya pwani kwa bei nafuu kunakiuka hukmu za Shariah ya Kiislamu zinazoharamisha ubinafsishaji wa mali ya umma, kwani ni mali ya Umma. Mtume (saw) amesema,

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: فِي الْمَاءِ، وَالْكَلَأِ، وَالنَّارِ»

Waislamu ni washirika katika umiliki wa vitu vitatu: maji, malisho, na moto,” na hii inajumuisha madini, rasilimali za nishati, na huduma za umma. Mikataba hii sio suluhisho la mgogoro; ni ya kubomoa kwa utaratibu muundo wa uchumi wa serikali kwa ajili ya mabepari wa ndani na nje.

Suluhisho haliko katika kuandaa bajeti mpya ndani ya mfumo wa kibepari, wala katika kurekebisha uwiano wa mapato au matumizi. Badala yake, liko katika kung'oa mfumo huu kabisa na kusimamisha Khilafah Rashida ambayo inatekeleza mfumo wa kiuchumi wa Uislamu. Chini ya Dola ya Kiislamu, kodi hazitozwi kwa watu ili kufidia nakisi; badala yake, dola inategemea vyanzo vya mapato ya Shariah. Hakuna ukopaji kwa msingi wa riba, wala mikataba yoyote na wakoloni, taasisi zenye riba kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa au benki za Kimagharibi.

Dola itafanya kazi ya kufutilia mbali deni lote la umma lenye msingi wa riba, kwa kuwa msingi wake ni batili katika Sharia; haitambuliwi wala kupitishwa kwa Ummah. Badala yake, waliohusika na madeni hayo watawajibishwa. Khilafah pia itasimamia rasilimali, huduma za umma, maji, nishati, na migodi kama mali ya umma ambayo haiwezi kuuzwa au kubinafsishwa. Rasilimali hizi lazima zitumike kushughulikia mambo ya watu, sio kuwahudumia wakopeshaji.

Dawoud alionyesha maumivu ya halisi, lakini hakusonga zaidi ya ukosoaji wa hali ya juu hadi utambuzi wa kina, wa kimsingi. Sisi kama Waislamu, ni wajibu wetu katika Shariah kutangaza kwamba tatizo haliko kwenye tarakimu, wala si kwa nani anatawala, bali ni jinsi wanavyotawala. Leo, utawala haujengwa juu ya Uislamu, bali unatokana na mfumo wa kibepari wa kisekula, ambao huzalisha umaskini, madeni, ubinafsishaji na ufisadi. Hakuna wokovu kwa Misri au kwa nchi nyengine yoyote ya Kiislamu isipokuwa kupitia kwa Khilafah Rashida, ambayo inasimamia Dini, inatekeleza mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu, na kuregesha mamlaka ya Ummah juu ya rasilimali zake.

Enyi wanajeshi wa Misri, enyi kizazi cha ‘Amr ibn al-‘As (ra)

Nyinyi ni ngao na upanga wa Ummah, ngome yake yenye nguvu wakati wa shida, na walinzi waangalifu wa Dini yake, usalama, na adhama yake.

Nyinyi ni wana wa Umma huu, nyama yake na damu yake, na juu ya mabega yenu kuna amana kubwa na jukumu zito: kuilinda Dini, kutetea matukufu ya Waislamu, na kuzuia utawala na udhibiti wa maadui juu ya ardhi na rasilimali zenu.

Kile ambacho Misri inapitia leo, kuzorota, kuporomoka, na utiifu wake wa kudhalilisha kwa taasisi na fedha za Magharibi sio hatima iliyokusudiwa. Badala yake, ni matokeo ya moja kwa moja ya kukosekana kwa utawala wa Kiislamu, na kujisalimisha kwa nchi kwa mfumo wa kibepari katili ambao haujui lolote isipokuwa unyonyaji wa watu na uporaji wa rasilimali zao.

Enyi wanajeshi wa Misri, msiwe ngao kwa wale ambao wamesaliti na kuuza. Msiwe upanga mikononi mwa wale walioweka nchi na watu wake rehani kwa wakopeshaji wa kigeni. Msiwe mlinzi wa wale ambao wamekiuka mali na riziki za watu, chini ya pazia la mageuzi na uundaji bajeti.

Msiruhusu silaha zenu zitumike katika kuimarisha batili hii. Msichafue heshima yenu kwa kutetea mfumo unaotumikia tu maslahi ya maadui. Badala yake, kuweni vile Mwenyezi Mungu (swt) alivyokukusudieni kuwa: walinzi wa Ummah wenu, mkijitahidi kwa ikhlasi kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume; dola ambayo inatawala kwa Sharia ya Mwenyezi Mungu (swt), inaukomboa Ummah kutokana na kutawaliwa, inarudisha mali na rasilimali kwa wamiliki wao halali, inajali kikweli mambo ya watu, na inaubeba Uislamu kama ujumbe wa uongofu na nuru kwa ulimwengu.

Enyi askari wa Misri,

Nusrah (msaada wa kijeshi), ambayo Mwenyezi Mungu (swt) anaingoja kutoka kwenu, sio kunusuru bendera au mipaka. Badala yake, ni nusrah kwa Dini, nusrah kwa ulinganizi wa haki, na nusrah kwa mradi mkubwa wa hadhara ya Kiislamu. Basi kuweni watu wake, na msikose fursa kubwa zaidi ya kuandika majina yenu katika daftari la milele la matendo mema, kuulinda Uislamu na dola yake, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kuisimamisha na akufanyeni enyi wanajeshi wa Misri kuwa Answari (wasaidizi) wake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal 24]

* Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.