Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bajeti ya Uturuki ya 2023

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kufuatia kuwasilishwa kwa Pendekezo la Sheria ya Bajeti ya Serikali Kuu ya 2023 iliyoandaliwa na Uongozi wa Mkakati na Bajeti kwa Bunge Kuu la Kitaifa la Uturuki kwa utiaji saini wa Rais Erdogan, majadiliano ya bajeti yanaendelea katika Tume ya Mipango na Bajeti.

Maoni:

Katika Bajeti ya Serikali Kuu ya Uturuki ya 2023, gharama zinakadiriwa kuwa TL 4 trilioni 469 bilioni na mapato ya TL 3 trilioni 810 bilioni. Katika hali hii, bajeti ya 2023 inatarajiwa kuwa na upungufu wa TL 659 bilioni. Pindi vipengee vya matumizi ya bajeti hiyo vinapochunguzwa, ugawaji wa TL 565 bilioni kama gharama za riba ni suala muhimu la kutiliwa mkazo.

Upungufu wa Bajeti unaojitokeza katika hali ambapo mapato hayawezi kulipia gharama hufikiwa na mauzo ya bili za hazina zenye riba kubwa na bondi za serikali kwa ukopaji wa ndani unaofanywa na Wizara ya Hazina na Fedha.

Miswada hii ya hazina na bondi za serikali hununuliwa na benki na wamiliki matajiri wa mitaji. Kwa maana nyengine, ili kukidhi nakisi ya bajeti, serikali hukopa kutoka benki na wamiliki matajiri wa mitaji kwa riba kubwa.

Benki nyingi nchini Uturuki ni za wamiliki matajiri wa mitaji. Kupitia benki hizi, wamiliki wa mitaji hupata mapato ya riba kubwa kwa kukopesha amana za watu ambazo sio mali yao kwa serikali kwa badali ya riba kubwa.

Ikizingatiwa kuwa kutakuwa na gharama za riba za TL bilioni 565 (takriban dolari bilioni 30) katika bajeti ya 2023, itaonekana kuwa serikali inahamisha kiasi kikubwa cha pesa kutoka kwa bajeti, ambazo ni pesa za watu, kwenda kwa mabenki na wamiliki wa mitaji.

Ukweli kwamba Rais Erdogan, ambaye anasema yuko dhidi ya riba, alihamisha kiasi kikubwa sana cha fedha kama vile takriban dolari bilioni 600 juu ya bajeti ya wananchi kwenda kwa wamiliki matajiri wa mitaji na benki kama gharama za riba katika utawala wake wa miaka 20 unamkanusha Erdogan asemaye anapinga riba na kufichua ametumikia nani katika kipindi chote cha utawala wake wa miaka 20.

Ikizingatiwa kuwa takriban nyumba/ghorofa milioni 12 au magari milioni 24 yanaweza kununuliwa kwa dolari bilioni 600, kiwango cha pesa zinazohamishwa na serikali kwa wamiliki matajiri wa mitaji kupitia bajeti pekee kitaeleweka vyema.

Kwa ufupi, bajeti ya 2023, pamoja na shughuli nyingi za kiuchumi na vitendo vya serikali vilivyo jengwa juu ya msingi wa uchumi wa kibepari, zinapelekea kuzidi kuwatajirisha matajiri, kuzidi kuwafukarisha maskini, na kusababisha dhulma kubwa katika mgawanyo wa mapato.

Mhusika mkuu wa vitendo hivi, vinavyoleta matokeo hasi na uchungu kwa watu nchini Uturuki na duniani kote, ni mfumo fisadi wa kiuchumi wa kibepari na serikali ya miaka 20 ya chama cha AK ambayo haijakata tamaa katika kutabikisha mfumo huu fisadi wa kiuchumi wa kibepari.

Hapana shaka kwamba urasilimali umetangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw) na wanadamu wote, na ni mfumo potovu fisadi ambao lazima ukataliwe na kuangamizwa. Na pia hapana shaka kwamba wanadamu wanaweza tu kuachwa huru kutokana na dhulma katika mgawanyo wa mapato na kupata ustawi kwa Khilafah Rashida, itakayo tabikisha hukmu zinazohusiana na uchumi za uongofu wa Kiislamu uliotumwa na Mwenyezi Mungu (swt), Mola Mlezi wa walimwengu wote.

(كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ)  

“ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Al-Hashr 7].

(أَلَيْسَ اللّٰهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِم۪ينَ)  

“Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?” [At-Tin 8].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi Ozer – Wilayah Uturuki

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.