Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 21/10/2020

Vichwa vya Habari:

Uturuki Yaanza Kuvunjavunja Nafasi za Syria

Amerika Kuiondoa Sudan kutoka kwa Orodha ya Dola Fadhili za Ugaidi

Mchumba wa Mwandishi wa Habari Amshtaki Mfalme Mtarajiwa wa Saudi

Maelezo:

Uturuki Yaanza Kuvunjavunja Nafasi za Syria

Jeshi la Uturuki limeanza kujiondoa kutoka kwa kituo cha uchunguzi cha Morek mjini Idlib, Syria. Walikianzisha kituo hicho mnamo 2018 na wamekiimarisha, ikiondoa dhana kwamba kamwe halitaachana nacho. Maafisa sasa wanasema hakina thamani ya kijeshi na kwamba wanaivunja kambi hiyo. Hiki kilikuwa moja ya vituo 12 ambavyo vilikusudiwa kuwasaidia waasi wa Siria mjini Idlib. Maafisa wengine wa Uturuki wanaripoti kwamba vituo vinne vya uchunguzi na kambi mbili za kijeshi mjini Idlib zitaondoka. Kambi hizo zinasemekana kuwa vigumu kuhami, na zina faida chache kwa waasi. Jeshi la Uturuki limekanusha kujiondoa kwenye nafasi hizo, lakini maafisa wengine wanathibitisha hili. Sasa kwa kuwa uasi wa Syria umetibuliwa na vikundi tofauti tofauti ima vimeshindwa au kuunganishwa katika mazungumzo yanayoongozwa na Magharibi mchoro uliotumiwa kufanikisha hii haufai tena kwani kusudi lake limepatikana. Uturuki, Saudi Arabia, Qatar na Jordan zote zilikuwa sehemu ya mkakati huu wa kuyageuza na kuyatibua mapinduzi, ambayo sasa yote yako wazi.

Amerika Kuiondoa Sudan kutoka kwa Orodha ya Dola Fadhili za Ugaidi

Rais wa Amerika Donald Trump alitangaza kwenye mtandao wa Twitter kwamba Amerika itaiondoa Sudan kutoka kwa orodha yake ya dola wadhamini wa ugaidi baada ya Khartoum kulipa dolari milioni 335 kwa wahasiriwa na familia za ugaidi wa Amerika.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alimshukuru Rais Trump kwenye Twitter. “Asante sana, Rais Trump! Tunatarajia sana kutangazwa rasmi na Bunge la Congress kuliondoa jina la Sudan kama dola mdhamini wa ugaidi, ambayo imeigharimu sana Sudan, ” aliandika. Kuondolewa kwa Sudan kwenye orodha ya ugaidi kunaaminika kuwa chanzo cha nchi hiyo ya Kiafrika kusawazisha mahusiano na 'Israeli', baada ya Imarati na Bahrain. Maafisa wawili wa Amerika ambao hawakutajwa majina waliiambia The New York Times kwamba Sudan huenda ikasawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi ndani ya siku chache baada ya maelezo ya kuondolewa kwa Sudan kwenye orodha ya ugaidi kufanyiwa kazi. Bunge la Congress linahitaji kuidhinisha kuondolewa baada ya kuarifiwa rasmi na rais. Dolari milioni 335 zinatarajiwa kulipwa kwa familia za wahanga wa mashambulizi ya al-Qaeda ya mwaka 1998 dhidi ya balozi za Amerika nchini Kenya na Tanzania. Amerika ilijibu bomu la ubalozi huo kwa kufyatua makombora kwenye kiwanda cha kutengeneza dawa jijini Khartoum. Amerika ilidai wakati huo kwamba kiwanda cha dawa cha Al Shifa kilikuwa kinatumiwa kutengeneza gesi ya neva kwa al-Qaeda, lakini hakuna ushahidi uliowahi kuthibitisha madai hayo. Kiwanda hicho kiliharibiwa katika shambulizi hilo. Kwa kuwa Al Shifa inazalisha nusu ya dawa nchini, uharibifu wake ulisababisha athari mbaya kwa raia wa Sudan.

Mchumba wa Mwandishi wa Habari Amshtaki Mfalme Mtarajiwa wa Saudi

Mchumba wa mwandishi wa habari wa Saudi Arabia aliyeuawa Jamal Khashoggi amewasilisha kesi dhidi ya mfalme mtarajiwa wa Saudi Arabia, akimtuhumu kuagiza mauaji hayo. Hatice Cengiz na kikundi kupigania haki kilichoundwa na Khashoggi kabla ya kifo chake wanamfuatilia Mohammed bin Salman na wengine zaidi ya 20 kwa uharibifu ambao haujafafanuliwa. Khashoggi aliuawa na timu ya mawakala wa Saudi wakati wa ziara ya ubalozi mdogo wa ufalme huo jijini Istanbul, Uturuki, mnamo 2018. Mfalme huyo mtarajiwa amekataa kuagiza mauaji hayo. Khashoggi alikuwa mkosoaji mashuhuri wa serikali ya Saudi na alikuwa akiishi katika uhamisho wa kibinafsi nchini Amerika, akiliandikia gazeti la Washington Post mara kwa mara. Suala zima limezifichua Amerika pamoja na Saudia. Mauaji ya kinyama ya Saudia na kubadilisha hadithi mara kwa mara na Donald Trump kutangaza waziwazi kuwa Amerika inahitaji mauzo ya ulinzi ya Saudi yanaonyesha kuwa mataifa haya hayana maadili na maisha ya mwanadamu ni njia tu ya kufikia lengo.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.