Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Taarifa kutoka kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan

kwa Al-Burhan na kwa Watu Wetu nchini Sudan
(Imetafsiriwa)

Baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa vuta nikuvute na mtihani wa nguvu tangu mapinduzi ya Al-Burhan mnamo 25/10/2021, na baada ya mzozo huo kujitokeza wazi kati ya Marekani, ambayo inamdhibiti Al-Burhan, naibu wake na kundi lake kwa upande mmoja, na kati ya Uhuru na Mabadiliko, na vyama vilivyoshirikiana nacho kutoka kwa vibaraka na wafuasi wa Uingereza kwa upande mwingine, kwa sababu hakuna hata moja ya pande hizi mbili (Amerika au Uingereza) iliweza kupanua ushawishi wake katika upande wa kijeshi na upande wa kiraia (walipokuwa wakifanya kazi) kwa pamoja, kwa hiyo walirudi kwenye makubaliano ya muda, kwa kutia saini Muundo wa Makubaliano ambao uliandaliwa na kafiri Volker chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Wamarekani na Waingereza. Al-Burhan anafanya kazi kwa bidii siku hizi kuzifanya kambi za kisiasa zinazokataa makubaliano hayo zijiunge nayo, ili kuunda serikali ya kiraia!

Muundo wa Makubaliano hayo unabainisha kuwa: “Sudan ni nchi yenye tamaduni, makabila na dini nyingi,” na huu ni uongo, kwa sababu karibu 98% ya watu wa Sudan ni Waislamu, na kwa hiyo Dini yao ni moja, ambayo ni Uislamu, na utamaduni wao ni mmoja, ambao ni utamaduni wa Kiislamu, na maandishi haya ni hila tu ya kuuweka Uislamu mbali na mifumo ya maisha na sheria. Muundo wa Makubaliano hayo pia yanabainisha kuwa: “Sudan ni nchi ya kiraia, kidemokrasia, kifederali, kibunge, ambayo kwayo ubwana ni wa watu na wao ndio chimbuko la mamlaka,” yote haya ni kinyume na Uislamu, kwani dola ya kiraia ni dola ya kisekula ambayo hutenganisha dini na maisha, na demokrasia hufanya haki ya kutunga sheria kuwa ya wanadamu, kwani haizingatii hukmu za Shariah, na kwa sababu ubwana ndani yake sio kwa Shariah; Quran na Sunnah na yaliyoongozwa kwazo. Ufederali huifanya dola kuwa chini ya mgawanyiko kwa sababu inamaanisha wingi wa watawala wanaopata mamlaka yao wenyewe kutoka kwa maeneo yao. Pia inamaanisha wingi wa sheria, kwani kila jimbo lina katiba na sheria zake.

Hii ni ncha ya tu ya mlima wa ukafiri kwamba muundo wa makubaliano hayo yanatoka, na inatosha kwa kila Muislamu mwenye shauku juu ya Dini yake kuyakataa, kwa mujibu wa kauli ya Mteule (saw): «مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ» “Mtu yeyote mwenye kuingiza katika amri yetu hili (Uislamu) jambo lisilotokana nao, basi linakataliwa.”

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunamkumbusha Al-Burhan na watiaji saini wa muundo wa makubaliano hayo, ambao walichukuliwa na balozi za Magharibi, kutumikia miradi yao, na kufanya uharibifu kwa watu wao, ili kuzunguka pambizoni mwa viti vibovu vya utawala, tunawakumbusha mambo yafuatayo:

Kwanza: Watu wa Sudan ni Waislamu, wanaikumbatia Dini tukufu ya Uislamu, kwani ndio kitambulisho chao na utamaduni wao, na ndio msingi wa maisha yao, na msingi wa dola yao, wao ni sehemu ya Umma mtukufu ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameuleta kwa ajili ya watu wote, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.”. [Aal-i-Imran: 110].

Waislamu na watu wa Sudan ni miongoni mwao, ni Ummah uliotolewa kuwatawala watu kwa hukmu za Mola Mlezi wa walimwengu wote, basi vipi watawaliwe na wale ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia “wale ambao wamepandisha hasira [Yako]” (maghdoub a’laihim), na wapotofu (dhallin) ambao hawajui?!

Pili: Uislamu mtukufu ni imani na mifumo ya maisha, yaani, ni Dini na kutokana nayo ni dola, na kazi ya yeyote anayeketi kwenye kiti cha serikali ni kutabikisha Uislamu kikamilifu na kijumla. Bwana wa viumbe vyote amehutubiwa kwa hili, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma’ida: 49].

Mwenyezi Mungu (swt) ameonya dhidi ya kuwapa njia waumini makafiri juu ya Waislamu:

(وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً)

“...wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini. [An-Nisa: 141].

Kisha, vipi kuhusu yule anayezipiga vita hukmu na mifumo ya Uislamu, na kusalimisha matukufu ya watu na mali ya nchi kwa kafiri mkoloni, zana zao, na mashirika yao!!

Tatu: Ni Uislamu mtukufu pamoja na hukmu zake ndio unaoikomboa nchi kutokana na ukoloni unaotuandama vifua vyetu. Ndiyo inaokomesha upuuzi huu. Kutokana na kutawaliwa na balozi za Magharibi, UNITAMS, na mashirika mengine ya Kimagharibi yanayoeneza ufisadi katika nchi zetu, na ni Uislamu ndio unaokifukuza kituo hiki cha kisiasa ambacho ni wakala wa ukoloni, na kuwaleta watu ambao ni watiifu kwa itikadi na Umma wao.

Nne: muundo wa makubaliano hayo hayatatatua mgogoro usioweza kusuluhishwa wa utawala nchini, ambao ni mzozo kati ya jeshi na pande za kisiasa, kwa sababu kwa kweli mzozo huo ni mapambano kati ya vibaraka juu ya viti vya madaraka kwa niaba ya dola kubwa (Amerika na Uingereza). Na kwa sababu yalikuwa ni makubaliano ambayo yaliegemezwa kwenye msingi batili; kutenganisha dini na maisha, dola, na jamii, na kwa sababu ni suluhu ya upatanishi ya muda baina ya nguvu zisizo na ikhlasi, na kwa sababu kila chama kinapanga njama dhidi ya kingine, mgogoro wa utawala utabakia, na ni hukmu za Uislamu pekee ndizo zitakazoutatua.

Tano: Muundo wa makubaliano hayo hautasuluhisha mgogoro wa kiuchumi ambao kwao watu waliasi, kwa sababu pande za Makubaliano hayo zimeunganishwa na nguvu za nje, na hufikiria kwa msingi wa mfumo wa kibepari katika uchumi, ambao ni mfumo wa hukmu za kikafiri. unaowafanya masikini kuzidi kuwa masikini na matajiri kuzidi kuwa matajiri, na kuwawezesha wakoloni makafiri kupora mali ya nchi zetu tajiri baada ya kuzifunga minyororo kwa mikopo yenye riba.

Tunakuelezea mambo haya ili uregee kwenye fahamu zako, na uachane na upotofu wako, ili utambue kwamba siasa sio himaya yako, na kwamba kutawala na kuchunga mambo ya watu sio taaluma yako, kwa sababu wewe hubebi fahamu ya kimfumo ya ulimwengu, mwanadamu na uhai, kutoka kwa Mpole, Mtaalamu (swt), kwa msingi wa imani ya Ummah juu ya jinsi ya kuchunga mambo, na jinsi ya kukabiliana na matatizo na migogoro ili utambue kupitia hilo hatari ya kuingia katika medani ya siasa ambayo si kwa mujibu wa mfumo wa Uislamu, ambapo utakanganyikiwa kati ya adui na rafiki, na utaongozwa kwenye kifo chako kwa mikono yako mwenyewe, hadi kufikia hatua ya mtawala halisi wa nchi yako, kuwa ni adui mkoloni kafiri!!

Ewe Al-Burhan, mtawala halisi wa Sudan: Itakapokufikia taarifa yetu hii ya kutuondolea lawama mbele ya Mola wako Mlezi na pengine huenda ukamcha Yeye, basi jua kwamba wewe bado uko katika upana wa maisha, hivyo basi patiliza fursa yake kwa kutubia kwa Mwenyezi Mungu,

تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحاً) “...Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli!” [At-Tahrim: 8] na uachane na kutekeleza hukmu za kikafiri na mifumo yake. Hiyo ni kwa kupitia tu kutoa Nusra (msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir, inayoufahamu mfumo mtukufu wa Uislamu, na jinsi unavyotekelezwa, na inafahamu uhalisia wa mzozo wa kimataifa, na jinsi ya kushughulika nao. Twakuombea uwe kama wale wa kwanza,

(وَالسَّابِقُونَ الأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ)

“Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye” [At-Tawba: 100].

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, tunawahamasisha watu wote wenye nguvu na ulinzi wenye ikhlasi, kuipa Nusra Hizb ut Tahrir ili Uislamu ufike kwa usafi wake katika utawala, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili kung’oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka katika nchi yetu, na kisha utajua na watu watajua watu wa dola ni kina nani, na fahamu za fahari na izza maana yake ni nini.

(إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ)

“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbiya: 106]

H. 15 Jumada II 1444
M. : Jumapili, 08 Januari 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.