Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Muharram 1444 Na: 1444 H / 005
M.  Jumamosi, 27 Agosti 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amerika, Urusi, China na Wafuasi Wao Wanacheza na Moto Na Hakuna Yeyote kati yao Aliyeko kwa ajili ya Manufaa ya Dunia
(Imetafsiriwa)

Imekuwa dhahiri kuwa Utawala wa Biden, una nia mbaya kama watangulizi wake. Katika kipindi cha miezi michache tu, umethibitisha kwamba katika madhumuni ya kudumisha ubabe wake juu ya uchumi wa dunia hauna tatizo lolote katika kuleta hali yoyote ya kisiasa duniani kwenye njia panda.

Mapema mwezi huu, katika jaribio lake la kufufua viwango vya uidhinishaji vilivyofifia vya Chama cha Democtrats kabla ya uchaguzi ujao wa bunge la seneti, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi aliikasirisha China ambayo tayari imechukizwa, kwa ziara yake nchini Taiwan.

Ulimwengu bado haujasahau jinsi mwezi Februari mwaka jana Rais wa Marekani Joe Biden alivyofanya kazi kubwa kuchochea mzozo kati ya Urusi na Ukraine kupitia mara kwa mara kuhakikisha kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamua kuivamia Ukraine, katika kile ambacho kilikuwa mbinu ya wazi ya kumnasa!

Hatimaye, Biden alifanikiwa katika uchochezi wake, na sasa ulimwengu unapaswa kukabiliana na janga la Urusi-Ukraine na athari za kiulimwengu juu ya usalama wa chakula, ustawi wa kiuchumi, na wasiwasi wa kijamii kutokana na swali linalojirudia mara kwa mara kuhusu uwezekano wa kipupwe cha nyuklia.

Sasa ni zamu ya China kutumbukia katika kina kirefu cha njama ya Marekani na hiyo ni kuwasha duara la moto katika maeneo ynayoizunguka China, moto wa kutosha ambao hatimaye utailazimisha kuanza kupunguza uwepo wake katika uchumi wa kiulimwengu.

Swali kubwa ni, "Yote hayo kwa ajili ya nini?", serikali hizi zinaahidi ulimwengu wa aina gani? Si Amerika wala China inatoa tumaini la kujenga ulimwengu ulio bora zaidi, unaowafaa wanadamu.

Lau tungeunganisha methali mbili za Kiingereza, tungesema umefika wakati wa kumhutubia “Ndovu Mweupe ndani ya Chuma” yaani ni wakati wa ulimwengu kuacha kuikwepa hofu ya kukiri ukweli kwamba urasilimali na kila imani nyengine iliyotungwa na wanadamu ni batili na yenye majanga na kwamba imekuwa zimwi ghali kuliweka nyumbani, huku gharama ikilipwa kwa riziki za wanadamu.

Uislamu umetabikishwa, na kwa milenia moja uliwafurahisha mabilioni ya watu, wakati wote huku ukihimiza haki sawa, na maendeleo ya mwanadamu katika nyanja zote za maisha, na kwa hili tunachagua mifano miwili ya haraka ...

Ni Sharia ya Kiislamu ndiyo ya kwanza iliyoweka msingi wa mchakato wa mahakama, na ni Khilafah katika Baghdad ya karne ya 8, ndiyo iliyoanzisha Nyumba ya Hekima, mahali pa kuzaliwa kwa sayansi nyingi mojawapo ikiwa ni mlingano wa hisabati yaani "Al- Jabr" uliowawezesha idadi kadhaa ya wanazuoni wa Kimagharibi baadaye kufikia uvumbuzi wao kupitia kwayo.

Kwa mara nyingine tena tunawaalika wanafikra wa Kiislamu, wanachuoni, washawishi wa vyombo vya habari kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kuwashinikiza watu wenye nguvu (Nusra) walete kuibuka mara ya pili kwa Ummah wa Kiislamu kupitia kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah iliyoahidiwa kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُم]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.