Afisi ya Habari
H. 13 Ramadan 1446 | Na: |
M. Alhamisi, 13 Machi 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Doria ya Pamoja ya 'CORPAT' na Adui India na Zoezi la Pande Mbili 'Bangosagar' Inathibitisha kuwa Vibaraka wa Marekani-India Wanacheza na Ubwana wa Nchi kwa Maslahi ya Mabwana zao Wakoloni
(Imetafsiriwa)
Moja ya sababu zilizomfanya msaliti Hasina kupinduliwa na watu ni kwamba alitekeleza njama ya India kule Pilkhana na mara kwa mara alifanya majaribio mabaya yote ya kuweka udhibiti wa India juu ya jeshi la nchi hiyo. Wakati ambapo wananchi wanapaza sauti kudai haki kwa mkasa wa Pilkhana, doria ya pamoja 'CORPAT' na zoezi la pande mbili 'Bangosagar' lililofanyika katika Ghuba ya Bengal kwa kushirikisha jeshi la wanamaji la Bangladesh na India imewashtua watu. Kwa kweli, vibaraka wa Marekani-India wamedhamiria kulinda maslahi ya kijiografia ya wakoloni wao hata kwa gharama ya ubwana wa nchi. Inafaa kutaja kwamba wakati matabaka ya kisiasa ya kisekula ya nchi hayakupaza sauti yake dhidi ya njama hiyo ya Pilkhana, ni Hizb ut Tahrir pekee ndiyo iliyofichua njama hiyo mbele ya taifa hilo kwa ushujaa na kupinga njama hiyo dhidi ya ubwana wa nchi hii. Na kwa sababu hii, serikali ya wahaini ya Hasina ilikipiga marufuku chama hiki cha ukweli na haki, na chenye nidhamu ya hali ya juu, ikikitaja kuwa ni tishio kwa kile kinachoitwa usalama wa umma. Na sasa ni wazi kama mchana, wakati wanacheza na ubwana wa nchi, vibaraka wa sasa wa Marekani-India wanafuata nyayo zile zile za Hasina aliyeanguka na kujaribu kunyamazisha sauti ya Hizb ut Tahrir. Mtume (saw) ametuonya kuhusu watawala hao wapumbavu. Mtume (saw) amesema,
«سَيَأْتِي عَلَى النَّاسِ سَنَوَاتٌ خَدَّاعَاتُ يُصَدَّقُ فِيهَا الْكَاذِبُ وَيُكَذَّبُ فِيهَا الصَّادِقُ وَيُؤْتَمَنُ فِيهَا الْخَائِنُ وَيُخَوَّنُ فِيهَا الْأَمِينُ وَيَنْطِقُ فِيهَا الرُّوَيْبِضَةُ قِيلَ وَمَا الرُّوَيْبِضَةُ قَالَ الرَّجُلُ التَّافِهُ فِي أَمْرِ الْعَامَّةِ»
“Itakuja kwa watu miaka ya khiyana, ambapo muongo atasadikiwa, na mkweli atakadhibishwa; msaliti atachukuliwa kuwa mwaminifu, na mtu mwaminifu atachukuliwa kuwa msaliti; na Ruwaibidha ndio wataamua mambo.’ Ikasemwa: ‘Ruwaibidha ni nani?’ Akasema: ‘Ni Mtu muovu na mnyonge anayetawala mambo ya watu.” [Ibn Majah].
Ni lazima watu wawawajibishe watawala hawa vibaraka wasaliti. Kwa sababu vibaraka hawa wanafichua siri za jeshi la Waislamu kwa maadui kupitia mazoezi ya pamoja ya kijeshi na kuuweka utawala wa nchi hatarini.
Enyi Maafisa wenye Ikhalsi katika Jeshi! Enyi walinzi makini wa kulinda uhuru na ubwana wa nchi! Uhadaifu wa vibaraka wa Marekani-India sasa uko wazi mithili ya muanga wa mchana. Kwa kuwa wao ni vibaraka, wamejitolea kulinda maslahi ya mabwana zao wa Magharibi huku wakipuuza maslahi ya watu, hivyo hawana imani na nguvu ya watu. Nyoyo zenu bado zinavuja damu kutokana na kuuwawa kwa wenzenu kule Pilkhana.
Hata hivyo, ni usaliti mkubwa ulioje ambao umefanywa na kipote cha watawala hawa vibaraka kwa kuandaa zoezi hili na wale ambao mikono yao imejaa damu ya ndugu zenu! Mumeshuhudia jinsi watu kwa umoja walivyocheza dori ya ushirikiano pamoja nanyi katika kukabiliana na uvamizi wa mpaka. Jinsi kizazi cha vijana kilivyotikisa barabara kwa umoja na kauli mbiu "Delhi au Dhaka, Dhaka Dhaka" na kulazimisha serikali ya wasaliti ya Hasina kuanguka. Hata hivyo ni jinsi gani kipote cha watawala vibaraka wauwaji wenye uchu wa madaraka ambao hawasiti kuiba "dhahabu ya sikio la mama yao", hawasiti kuwagawanya kwa ajili ya mabwana zao wa Magharibi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
«وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imaam (Khalifa) ni ngao ambayo mnapigana nyuma yake na mnajilinda kwaye” [Sahih Muslim]. Kwa hiyo, lazima muregeshe mfumo halisi wa usimamizi wa Khilafah ili kulinda ubwana wa nchi. Kama munavyojua, katika mpango wa “Matembezi ya Khilafah” watu wametaka Nusrah (nguvu) kwa ajili ya Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa kilichojitolea kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.
Insha’Allah, chini ya Khilafah pekee, watu wataungana na kukabiliana na utawala wa wakoloni makafiri wa Magharibi na kiongozi wao wa kieneo India.
[إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah At-Tawbah: 39]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari |
Address & Website Tel: |