Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  2 Rabi' I 1447 Na: 1447 / 04
M.  Jumatatu, 25 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ubwana Uliopotea na Vyama Vikipigania Nyadhifa Huku Uchungaji wa Ummah ukiwa Sio Miongoni mwa Hamu Zao
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo vyama tawala vinajiandaa kushindana katika uchaguzi na ngawira zake zilizopangwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu, vikosi maalum, vifaru, na magari ya kivita, alfajiri ya Ijumaa, 22/08/2025, vilizingira Hoteli ya Lalezar katikati ya Sulaymaniyah na kuivamia, ili kutekeleza operesheni ya kumkamata mkuu wa Chama cha Jabhat Ash-Sha’ab, Lahur Sheikh Jangi. Baada ya mapigano makali ya silaha yaliyodumu kwa masaa mengi kati ya Vikosi vya Kupambana na Ugaidi na Vikosi Maalum (Commandos) na “Asayish,” vikosi vya usalama vilivyounganishwa na Muungano wa Uzalendo wa Kurdistan upande mmoja, na walinzi wa Sheikh Jangi upande mwengine, yalimalizika kwa kukamatwa kwa Lahur na kaka yake Pulad, na kusababisha vifo na majeraha.

Operesheni hii haikuwa ya kwanza, kwani ilitanguliwa na operesheni zengine zinazofanana na hii; Mnamo tarehe 12/08/2025, vitengo vya “Asayish” vilifanya operesheni ya kuwakamata viongozi mashuhuri wa mkondo wa upizani kiliberali wa kiraia, hasa Shaswar Abdullah, kiongozi wa Harakati ya Kizazi Kipya. Wakati huo huo, operesheni za ukamataji pia ziliathiri raia mithili ya hao baada ya kibali cha mahakama cha kukamatwa kutolewa kwa kisingizio cha “kuvuruga usalama” na mahakama ya Sulaymaniyah.

Yalichotokea Sulaymaniyah yanatokea kote Iraq, na chanzo chake ni mzozo na ung’ang’aniaji nyadhifa baada ya kula pesa haramu, kutumia rasilimali za nchi kwa maslahi yao binafsi, kwa lengo la kudhoofisha, kuzima, au hata kuwatenga na kuwaangamiza wapinzani. Kila siku, majina ya wale waliofanywa watumwa hutangazwa kutoka kwa uchaguzi chini ya kisingizio cha Sheria ya Kuondoa Ubaathi, faili za ufisadi, na visingizio vyengine, kama ilivyotokea—kwa mfano, lakini sio pekee—kwa Abdul Ghani Al-Asadi, ambaye alishikilia wadhifa wa Gavana wa Dhi Qar, na wadhifa wa Mkuu wa Huduma ya Usalama wa Kitaifa, pamoja na kufanya kazi kama Kamanda wa Vikosi vya Kupambana na Ugaidi. Kwa hivyo sheria hii ilikuwa wapi alipochukua nyadhifa hizi zote?!

Na haya yote yanatokea huku Iraq ikiishi katika hali ya machafuko, hofu, na wasiwasi, na katika kunyang'anywa ubwana unaodaiwa kutokana na uingiliaji kati wa Amerika na vitisho vyake vya kuzuia kupigia kura Sheria ya Uhamasishaji wa Watu iliyopitishwa na vikosi vya Muundo wa Uratibu, ambavyo havikusubutu kuipitisha hadi sasa, na vinajaribu kutupa mpira katika mahakama ya vyama vinavyopingana vikitumia hisia za wafuasi wao, ingawa vinaweza kuipitisha kwa sababu vina idadi ya wengi bungeni. Vyanzo vya habari vilichapisha taarifa ya Mbunge Hadi Al-Salami kwamba kuondolewa kwa rasimu ya sheria ya Mamlaka ya Uhamasishaji wa Watu kulikuja baada ya mkutano wa Muundo wa Uratibu, ikionyesha kwamba Waziri Mkuu alitekeleza uamuzi wa mkutano bila kuwasilisha tena sheria hiyo hadi sasa, na akaonyesha kutokuwepo kwa nia ya wazi miongoni mwa viongozi wa Muundo huo wa kupitisha sheria hiyo licha ya kukamilika kwa usomaji wa kwanza na wa pili, akidai kwamba sababu ya hilo ni kutokana na mzozo juu ya nyadhifa.

Enyi Waislamu nchini Iraq: Serikali zote mtawalia zilizotawala Iraq tangu ilipokaliwa kimabavu mwaka wa 2003 zimetelekeza ubwana na uchungaji, na zikawa zimejishughulisha na kumtumikia mvamizi, kupigania kupata madaraka, na kukimbilia kunyakua rasilimali na utajiri wa nchi kwa njia zote duni na za ovu. Kwa hivyo, hakuna heshima kwetu na hakuna wokovu isipokuwa kwa kung'oa uchafu huu na kutakasa nchi hii kutoka nao, na kubadilisha mfumo huu mbovu uliowekwa na mvamizi Marekani, na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume juu ya magofu yake.

Ni kwa heshima hii na maisha haya ya hadhi ambayo Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakulinganieni. Hivyo itikieni amri ya Mola wenu Mlezi:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.