Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  24 Jumada I 1447 Na: 1447 / 05
M.  Jumamosi, 15 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Masanduku ya Kura katika Mfumo Fisadi Ndio Udanganyifu Mkubwa Zaidi kwa Mabadiliko
(Imetafsiriwa)

Tangu Marekani ilipovamia mwaka wa 2003 hadi sasa, Iraq imekuwa ikizama katika matatizo, na hali yake inazidi kuwa mbaya. Yote hayo ni matokeo ya ramani ya kisiasa ambayo mvamizi Marekani aliiunda na kuilazimisha. Ndiyo iliyoweka misingi ya mfumo huo na kuchora ramani ya kisiasa ya nchi hii, ikiudanganya umma wa Iraq kuamini kwamba suluhisho la matatizo yanayozalishswa na mfumo huu ni masanduku ya kura.

Kwa hivyo, haishangazi kwamba mjumbe wa Marekani nchini Iraq, Mark Savaya, aliwapongeza Wairaqi kwa mafanikio ya uchaguzi wa bunge, akithibitisha “kwamba watu wa Iraq wameonyesha tena kujitolea kwao kwa uhuru, utawala wa sheria, na taasisi imara za serikali”! Na hivyo Wairaqi walianguka katika mtego wa udanganyifu na kuendelea kubadilisha baadhi ya nyuso bila kuzingatia shina la ugonjwa na asili ya fitina iliyosababisha matatizo haya yote. Kwa hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya, na watu wa Iraq walibaki katika meli ya kutangatanga, wakirushwa rushwa na mawimbi ya mkanganyiko na wasiwasi.

Baada ya zaidi ya miaka 22, na baada ya kukamilika kwa upigaji kura kwa ajili ya raundi ya sita ya uchaguzi mnamo Jumanne, 11/11/2025, bado tunashuhudia watu wengi wa Iraq waking’atwa kutoka kwenye shimo lile lile tena na tena. Licha ya kukata tamaa kwao kutoka kwa vyama vyote na kambi za kisiasa ambazo zimeiba nchi na kuwadhalilisha waja, bado wanaenda kwenye shimo lile lile na wanang’atwa nalo kwa mara nyengine tena, wakiendeshwa kwa misingi ya kimadhehebu, kijamii, na kikabila, ila tu kurudi baadaye wakilaani saa waliyokwenda kwenye uchaguzi!

Enyi watu wa Iraq: Tumefafanua mara kwa mara, katika kila mzunguko kabla yake na baada yake, kwamba matatizo yenu yanasababishwa na mfumo fisadi, na kwamba suluhisho lake haliwezi kutoka ndani yake. Tumeelezea zaidi kwamba kitendo hiki—kugombea nafasi na kupiga kura—ni haramu, kwa sababu Baraza la Wawakilishi ni baraza la kutunga sheria, na hivyo ni taghut inayotunga sheria bila ya Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo taghut ile Mwenyezi Mungu Mwenyezi aliyotuamuru kuikufuru. Kisha baada ya kila mzunguko uliofeli munadai kwamba munajuta na kwamba hamkutaka chochote isipokuwa mageuzi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anakujibuni kwa maneno yake:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيداً * وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْاْ إِلَى مَا أَنزَلَ اللّهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُوداً * فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَآؤُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللّهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلاَّ إِحْسَاناً وَتَوْفِيقاً * أُولَـئِكَ الَّذِينَ يَعْلَمُ اللّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِي أَنفُسِهِمْ قَوْلاً بَلِيغاً]

“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali. * Na wanapo ambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, na njooni kwa Mtume; utawaona wanaafiki wanakukwepa kwa upinzani. * Basi inakuwaje unapo wasibu msiba kwa sababu ya yale iliyo tanguliza mikono yao? Hapo tena hukujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hatukutaka ila wema na mapatano. * Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.” [An-Nisa:60–63].

Na isisemwe hapa kwamba hakuna chaguo ila kuwachagua wale tunaowaona kuwa wema ili wafisadi wasihodhi madaraka. Hapana, hili halipaswi kusemwa; kwani ni kosa lililo mbali na uhalisia. Kumchagua mtu mwema ndani ya mfumo fisadi humfisidi mtu badala ya kurekebisha mfumo. Na wema aina gani huu, wakati mtu anagombea baraza linalompinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa kutunga sheria bila ya Mwenyezi Mungu na kujisalimisha kwa katiba ya ukafiri iliyolazimishwa na mvamizi Marekani?!

Enyi watu wa Iraq kwa jumla, na Enyi watu wenye Nguvu na Ushawishi hasa: Suluhisho thabiti na suluhisho halali ni kazi nzito ya kung'oa mfumo huu fisadi na kusimamisha Sharia ya Mwenyezi Mungu ndani ya Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Kwa hivyo kusanyeni azma yenu na musimame pamoja na wenye ikhlasi miongoni mwa Ummah wenu wanaofanya kazi ya kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Kwa kheri hii kubwa Hizb ut Tahrir hii inakulinganieni, ili muondoe udhalilifu shingoni mwenu na mrudi kama Ummah bora, kama wema wenu waliokutangulieni walivyokuwa.

[هَٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ]

“Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.” [Ibrahim:52]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.