Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
| H. 10 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: 1447 / 13 |
| M. Jumatano, 27 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Salamu za Idd
Idd ni Wakati Ambapo Furaha na Huzuni Zinaunganishwa!
(Imetafsiriwa)
Siku hizi Idd al-Adha inafika, ambapo furaha na huzuni zimechanganyika. Furaha katika mwitikio wa waumini kwa wito wa Mwenyezi Mungu wa Hijja, wakiitikia wito wake katika mkusanyiko unaowaunganisha kutoka pembe zote za dunia, pamoja na makabila na rangi zao mbalimbali, kwa kutii amri ya Mwenyezi Mungu na kupata radhi Zake. Na huzuni kubwa inawakumba nyoyo zao kwa masaibu yao tangu kupoteza nguvu yao na kuvunjwa kwa dola yao mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Ni Idd ya aina gani huku Gaza ikiendelea kutokwa na damu?! Idd ya aina gani huku kambi na meli za kivita za maadui wa Umma zikiwa katikati ya ardhi zake?! Idd ya aina gani huku wanawake huru wa Waislamu wakidhalilishwa huko Palestina, Turkestan Mashariki, Myanmar, na India?!
Enyi Waislamu: Je, inafaa kwa Umma mtukufu, unaozidi watu bilioni 1.5, uliobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa imani kubwa na uliojaa utajiri na maeneo ya kimkakati, kuwa chini ya mataifa?! Je, si haifai zaidi kwa Ummah, kwa faida hizo, kuwa kiongozi asiye na ubishi?!
Hii ni hali ya kuhuzunisha ya Ummah, na sababu yake ni wazi na dhahiri: kuvunjwa kwa dola yake na kugawanyika kwake kuwa dola sitini. Tiba yake iko wazi vile vile: kuregeshwa kwa mamlaka yake na kusimamishwa kwa dola yake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Enyi Waislamu: Kama vile Mwenyezi Mungu (swt) alivyofaradhisha Hijja juu yenu, pia amewajibisha juu yenu faradhi kubwa, hakika taji la faradhi zote. Kwani utabikishaji wa sheria za Mwenyezi Mungu miongoni mwenu unategemea hilo. Faradhi hii ni juhudi za dhati za kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kusimamisha Khilafah, ili muweze kurudi kuwa Ummah wa heshima na hadhi, na kuziokoa nafsi zenu na wanadamu wote kutokana na utawala wa dhulma na ufisadi wa ubepari na taabu na uharibifu ambao umesababisha kwa watu na riziki zao.
Je, alfajiri ya Khilafah haijafika, na muozo wa ubepari kutoweka, huku tukifurahia maneno ya Mola Mtukufu:
[وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً]
“Na sema: Haki imefika, na batili imetoweka. Hakika batili lazima utoweke!” [Al-Isra 17:81].
Kwa kumalizia, tunawapongeza Ummah wa Kiislamu kwa Idd al-Adha iliyobarikiwa, na hasa tunawapongeza wabebaji wa ulinganizi, wa kwanza miongoni mwao Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde na ampe ushindi na uwezo kupitia yeye, tukimwomba Mwenyezi Mungu airudishe kwa Ummah wa Kiislamu kwa usalama, amani na Uislamu, na kuifanya kuwa Idd ya kheri, baraka, ushindi na tamkini.
Idd Mubarak, muwe karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na muwe imara zaidi katika kumtii Yeye.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Iraq |
Address & Website Tel: |
E-Mail: hutiraq@yahoo.com |