Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  11 Jumada II 1441 Na: 1441 H / 01
M.  Jumatano, 05 Februari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Pompeo akutana na Mawaziri wa Kigeni wa Nchi za Asia ya Kati
(Imetafsiriwa)

Katibu wa Serikali ya Amerika Mike Pompeo alifanya mkutano huko Tashkent mnamo tarehe 3/2/2020 na mawaziri wa kigeni wa Nchi za Asia ya Kati. Kabla ya mkutano rasmi wa P5 + 1, alikutana na Rais wa Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Uzbekistan na kuwahimiza wao kuizuia Uchina kutokamana na kupanuka ndani ya Turkistan Mashariki na Nchi za Asia ya Kati. Pia aliwahimiza wao kusaidia mkakati wa Amerika unaolenga kudhoofisha ushawishi wa Urusi katika nchi hizi, na kuunga mkono juhudi za Uzbekistan nchini Afghanistan. Alitoa dola milioni 1 kukuza biashara na Afghanistan, na aliishukuru Kazakhstan kwa kutowakabidhi Waislamu wengi wa Wachina kwa serikali ya Uchina.

Kwa hivyo, Amerika inalenga kuzielekeza nchi za Asia ya Kati dhidi ya Uchina, na pia kuutoa Mkoa kutoka kwa Udhibiti wa Urusi kiuchumi na kisiasa kwa kuanzisha amani nchini Afghanistan.

Pompeo hakuzuru Kyrgyzstan. Wanasiasa na wachambuzi wa kisiasa wamelitafsiri hili kwa njia kadhaa. Amerika imeweka vizuizi kwa watu wa Kyrgyz. Mnamo tarehe 3/2/2020, Tovuti ya Sputnik iliripoti kwamba takriban dola milioni 60 ziliingizwa Kyrgyzstan kutoka uwanja wa ndege kwa pepe ya kidiplomasia. Mkutano unaofuata wa P5 + 1, uzinduzi wa chama kipya cha Wamagharibi kinachoitwa Liberal Democratic Party kinachoongozwa na Janar Akayev, na dola milioni 60 pesa taslimu ambazo zilidaiwa kufanywa kuunga mkono vikosi vya Wamagharibi kabla ya kura, yote yalitokea kwa siku moja.

Mtazamo wa Amerika kuielekea Kyrgyzstan umebadilika vibaya, na hili linaweza kuelezewa na kutoridhika kwake na viongozi wa Kyrgyz, kwa sababu wanaziba mapengo ya kisiasa na kiuchumi ambayo yamezuka kwa sababu ya udhaifu wa Urusi katika mkoa huo kupitia Uchina. Kwa hivyo, inaweza kusemwa kuwa Amerika imeanzisha mkakati mpya wa kisiasa wa Kyrgyzstan.

Katika miaka ya hivi karibuni, nguvu ya kiitikadi ya Kimagharibi imeongezeka nchini Kyrgyzstan, na inaonekana kuwa viongozi na mduara wa kisiasa wamedhoofika na kuunda hali nzuri kwa kuanguka kwa nguvu mpya ifuatayo. Lakini kuanguka kwa nguvu inayotarajiwa inatofautiana kikamilifu na kesi za nyuma kulingana na mtazamo mpya wa Kimagharibi. Mapenduzi ya awali yalifanikisha mabadiliko ya madaraka ndani ya mduara wa kisiasa wa mrengo wa Urusi, na mabadiliko yaliyotarajiwa yatakuwa kwa kuzuka kwa mahodari wa kisiasa kama vile toleo la Ukraine na kuondolewa kwa ile ya zamani.

Kwa hivyo, Mkakati wa Amerika katika Asia ya Kati ulijengwa kwa misingi ya kuzuia Ujumuishaji wa Uchina katika mkoa na kuzuia ukoloni wake, Wakati Urusi inadhoofika na kuanguka (na kuondolewa) katika siasa za kimataifa. Amerika pia ilitaka kuchukua fursa zote za kimikakati katika mkoa dhidi ya Uchina na Urusi kwa maslahi yake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.