Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  25 Safar 1444 Na: 1444 / 08
M.  Jumatano, 21 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala Hawajali huku Mamilioni Wakiteseka katika Mafuriko

Enyi Watu wenye Nguvu! Waondoeni Watawala hawa Wasiojali, Wenye Moyo Baridi na Simamisheni Tena Khilafah Mahali Pao

(Imetafsiriwa)

Theluthi moja ya Pakistan ilikabiliwa na mafuriko. Zaidi ya watu 1500 walipoteza maisha. Nyumba milioni moja ziliharibiwa. Watu milioni thelathini na tano waliathiriwa na mafuriko, wakiwemo watoto milioni kumi na sita. Walakini, kwa uongozi wa kidemokrasia wa Pakistan, kifo na uharibifu ulikuwa fursa ya kupiga picha. Walijifanya kuwahurumia watu, kwa kulowesha nguo kwa maji ya mafuriko, kusambaza kiasi kidogo cha chakula na kufanya uchunguzi wa angani wa watu waliokwama na wanyonge, kana kwamba hii iliwaondolea jukumu lao.

Badala ya kujishughulisha kikamilifu na misaada ya mafuriko, uongozi wa kisiasa unashughulika na uteuzi wa mkuu mpya wa jeshi na mchezo wa uchaguzi, huku uongozi wa kijeshi ukinaswa katika mapambano dhidi ya mkuu wa jeshi anayekuja. Waziri Mkuu, Shehbaz Sharif, alikwenda London kumzika Malkia Elizabeth II, kana kwamba mazishi hayo hayangefanyika bila yeye. Vile vile, chama cha upinzani cha PTI kinajishughulisha na mikutano yake ya hadhara, matukio ya kujinadi, kampeni za mitandao ya kijamii, mikutano ya siri na mawasiliano ya mlango wa nyuma. Serikali za mkoa wa PTI wa Punjab na Khyber Pakhtunkhwa zinashughulika kutafuta maslahi ya kisiasa na ya kibinafsi. Haya yote ni huku waathiriwa wa mafuriko wakililia chakula na mahitaji ya kimsingi, chini ya anga wazi, bila paa. Hivi sasa pia wako hoi dhidi ya magonjwa yanayosambazwa na maji kama vile kipindupindu, dengue na malaria.

Kulingana na makadirio, chanzo kilichoharibiwa na mafuriko kimegharimu zaidi ya dolari bilioni thelathini. Mazao yaliyokuwepo yaliharibiwa. Mamilioni ya ng'ombe waliathiriwa na mafuriko. Katika hali mbaya kama hiyo, vyombo vyote vya serikali, watawala, urasimu, jeshi, polisi, ulinzi wa raia, mawaziri, wawakilishi wa umma na wafanyikazi wa matibabu wa serikali, lazima wahamasishwe. Walakini, hakuna kitu kama hicho kilionekana. Serikali haikufungua hata maghala yake na hazina. Badala yake, mdomo wa hazina hufunguka kwa ajili ya kufanya malipo ya riba pekee, si kwa ajili ya watu, huku vipaumbele vya watawala vikiwa ni kuomboleza kifo cha Malkia wa kikoloni wa Uingereza, na sio kushiriki maumivu ya watu.

Khilafah Rashidah ilionyesha jinsi ya kukabiliana na majanga kama vile baa la njaa na mafuriko. Wakati baa la njaa lilipoikumba Hijaz mnamo 18 Hijri, vyombo vyote vya dola vilihamasishwa ili kumaliza janga hilo, huku uongozi mzima ulikuwa ukijishughulisha kikamilifu katika kutoa misaada. Msaada mkubwa, ikiwemo chakula na mavazi, ulitumwa kutoka wilaya za Misri na Ash-Sham. Khalifa Umar (ra) binafsi alikuwa akijishughulisha na juhudi kubwa za usaidizi, huku akila kiwango cha chini kabisa, bila bughudha. Huu ulikuwa ni mwitikio mkubwa na mpana kwa Ummah wa Khilafah katika kukabiliana na majanga ya kimaumbile. Ni tofauti kabisa na Demokrasia, ambapo Shahbaz Sharif anasimulia utafiti kuhusu ongezeko la joto duniani, huku akiomba fedha.

Kupuuzwa wakati wa mafuriko kumedhihirisha wazi kuwa ni wakati wa kuizika Demokrasia ya kisekula. Hakuna hata mmoja wa watawala hawa aliye na hisia yoyote ya kuwajibika kabla ya mafuriko, kwa hiyo vipi hivi sasa siku zijazo? Huu ndio wakati wa kuwapindua, kuwaondoa na kusimamisha tena Khilafah.

Enyi Maafisa wa Vikosi vya jeshi la Pakistan! Munahitaji sababu gani zaidi ya kuhamasika? Katika Sindh na Balochistan, kutokuwepo kwa vyombo vya dola, rasilimali na tahadhari ni dhahiri. Chama tawala na upinzani vinashughulika katika mzozo wa kuwania madaraka katika jimbo la Punjab, wakati kura za Sindh na Baluchistan hazihesabiki katika mzozo huu. Maisha na mustakbali wa mamilioni ya watu unategemea uamuzi wenu, msimamo na hatua yenu. Toeni Nusrah sasa ili kusimamisha tena Khilafah na kuwakomboa watu wenu kutokana na mfumo huu katili na watawala walio na roho mbaya. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنْصَارَ اللَّه)

“Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu” [As-Saff, 61:14].

 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.