Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: HTS 1443 / 39
M.  Jumapili, 05 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuongezwa Muda wa Ujumbe wa UNITAMS kwa Mwaka Mwengine

Kunatokana na Usimamizi wa Dhahiri wa Nchi za Kikoloni juu ya Sudan
(Imetafsiriwa)

Mnamo Siku ya Ijumaa, tarehe 03/06/2022, Baraza la Usalama lilipitisha Azimio nambari 2636, la kuongeza muda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kusaidia Awamu ya Mpito nchini Sudan (UNITAMS) kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi 06/03/2023, kwa kauli moja ya wajumbe wa Baraza la Usalama.

Kuongezwa muda wa ujumbe wa UNITAMES kunamaanisha mwaka mwingine wa usimamizi wa wazi wa dola za kikoloni juu ya nchi hii, na kwamba kuongezwa kwa muda wa UNITAMS na kuiongezea ala za kikanda za Kafiri mkoloni; Umoja wa Afrika, IGAD, na chini ya bendera ya utaratibu wa pande tatu wa kuunda upya nchi hii kwa misingi ya ukafiri, na kuondoa mgongano kati ya ala mbili za ukoloni wa kimataifa; jeshi linaloungwa mkono na ukoloni mamboleo; Amerika, na miongoni mwa raia wasekula wanaonasibishwa na ukoloni mkongwe; Uingereza, yote haya yanakataliwa na Hizb ut Tahrir, na watu wa Sudan.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na mbele ya uongezaji muda huu tunathibitisha mambo yafuatayo, na kunukuu kutoka katika Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah:

Kwanza: Uislamu unaharamisha makafiri kuwa na njia juu ya waumini, na ujumbe wa UNITAMS unafanya kazi ya kuchunga mambo, na kwa hiyo una mamlaka juu ya Waislamu wa Sudan, na hilo limeharamishwa kwa mujibu wa Shariah,

kama asemavyo Mwenyezi Mungu:  [وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً] “wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini." [An-Nisa: 141].

Pili: Mashirika ambayo hayana msingi wa Uislamu, au yanayotabikisha hukmu zisizokuwa za Uislamu, dola haipaswi kushiriki, kwa mfano katika mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), na Benki ya Dunia. Na asasi za kieneo kama vile Jumuiya ya Waarabu, Muungano wa Afrika, IGAD na nyinginezo, kwa sababu misingi ambayo juu yake jumuiya hizo ziliasisiwa imeharamishwa na Sharia, kwa sababu zimeegemezwa kwenye msingi wa kirasilimali ambao umejikita juu ya msingi wa usekula; yaani itikadi ya kutenganisha dini na maisha, pamoja na kuwa ni chombo mikononi mwa nchi kubwa, hasa Amerika.

Tatu: Kamwe hairuhusiwi kwa mtu binafsi, chama, kambi au kikundi chochote kuwa na uhusiano wowote na nchi yoyote ya kigeni. Uhusiano na dola nyengine umefungwa kwa serikali pekee, kwa sababu hiyo pekee ndiyo yenye haki ya kuchunga mambo ya Umma kivitendo. Na umma na kambi lazima ziihisabu dola kwa uhusiano huu wa nje, kwa sababu ya kauli yake (saw): «الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imamu ni mchungaji na yeye ni ndiye mwenye kuulizwa kuhusu raia wake.” [Imepokewa na al-Bukhari]. Shari’ah ilimpa mtawala njia ya kivitendo ya kuchunga mambo, uangalizi wa faradhi kwa yeye peke yake, na hairuhusiwi kwa mtu mwengine yeyote kufanya hivyo.

Kwa kumalizia, dola hizi za kitaifa zinazofanya kazi, ambazo zilianzishwa na makafiri wanaozikoloni nchi za Waislamu, na kituo hiki kikaragosi cha kisiasa, hazitauendeleza Ummah wetu, wala hazitarudisha heshima na hadhi yake. Bali mwenye kufanya hivi ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume itakayowakata Makafiri, kung'oa ushawishi wao, kusimamisha uadilifu, na kuchunga mambo ya Ummah kwa hukmu za Mola Mlezi wa walimwengu wote, ili watu wahakikishiwe maisha ya utu hapa duniani, na wapate radhi za Mwenyezi Mungu Akhera.

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum 4-5]

 Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu