Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  18 Jumada II 1444 Na: 1444/12
M.  Jumatano, 11 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wito kutoka kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia kwa Watu wetu nchini Tunisia
(Imetafsiriwa)

Enyi Waislamu katika Ardhi ya Al-Zeytuna:

Mumeshuhudia jinsi demokrasia ilivyo fisidi maisha yenu, na kuifanya ardhi yenu kuwa mahali pazuri kwa matamanio ya nguvu zinazodhibiti jamii kwa pesa na ushawishi kwa jina la watu na kinyume na matakwa yao, na mukashuhudia usaliti wa kituo kizima cha kisiasa na shauku yao ya kuzitii serikali za kikoloni za Magharibi hadi zikaiingiza Tunisia chini ya usimamizi wa ukoloni na taasisi zake za kifedha, na juu yazo ni Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, chombo hatari cha wakoloni.

Mlikuwa kinara wa Umma wa Kiislamu katika kuwaasi madikteta na madhalimu, na mlikuwa kinara wa Waislamu katika kutaka mabadiliko ya mfumo wa kisekula ulioanzishwa na wakoloni katika nchi zote za Kiislamu, na mkafanikiwa kumfurusha dhalimu Ben Ali. Je, munakubali kuongozwa na wanyonge na vibaraka walioyageuza mapinduzi yenu na kuyapotoa kutoka kwenye njia yake kukupelekeni kuirudisha Tunisia na nyinyi kwenye zizi la utegemezi na udhalilifu?! Na je, mnakubali kuwa watumwa na wategemezi wa Makafiri, na hali nyinyi ni Waislamu ambao Mwenyezi Mungu amewakirimu kwa Uislamu?!

Enyi Waislamu katika ardhi ya Al-Zeytuna, nchi ya Mujahidina mashujaa:

Nyinyi ni Waislamu kutoka katika kizazi cha mujahidina, wafunguzi Tariq bin Ziyad na Uqba bin Nafeh, na tumewajua nyinyi tu kama wanaume msionyamaza kimya juu ya dhulma na mnakataa utegemezi wote, na tumewajua nyinyi tu kama Waislamu mupendao Dini yenu na Mtume wenu (saw), basi kwa nini mukae kimya juu ya upuuzi huu wa kisekula? Je, miaka kumi na mbili ya ubatili wa kidemokrasia haijatosha?! Mamluki watacheza kwenye majeraha yenu hadi lini huku mukitazama?! Watafanya biashara ya maumivu yenu hadi lini huku mkisubiri?!

Pengine munamsubiri rais, au upinzani, au chama cha wafanyakazi, au mazungumzo baina yao wanayodai ni ya kizalendo, hivi wana kipi zaidi ya kuwa utiifu, kuikabidhi nchi na kuiweka rehani?

Enyi watu wa Tunisia:

Mabadiliko ya utawala muliyoyataka hayakufanyika mwaka wa 2011 kwa uchaguzi, bali kwa kukataa kikanuni na kinaganaga utawala uliopo. Ben Ali na ubabe wake haukutoka kwa njia ya uchaguzi, bali alikimbia kwa kukimbia pindi mulipompigia kelele “Ondoka...” na walioko madarakani wakakuungeni mkono, lakini kukosekana kwa uongozi mbadala na wa dhati na busara ndiko kulikokosa fursa kwa ajili yenu, hivyo utawala wa kikoloni wa Magharibi ulirudi kupitia dirishani, bali kupitia mlangoni.

Vivyo hivyo leo, ushawishi wa ukoloni na vibaraka wake hautaondolewa, isipokuwa musimame kwa umoja na kusema neno lenu la mwisho "tuondokeeni". Tofauti wakati huu:

1- Kuna uongozi wenye fahamu miongoni mwenu, ambao ni Hizb ut Tahrir, ambao Mashababu wake wanajulikana na ukakamavu wao katika ulinganizi wa haki.

2- Badali iko wazi na salama, kwani ni mfumo wa Uislamu ambao munauamini.

3- Kwamba mfumo wa Uislamu haunyanyui kauli mbiu ya umma isiyo eleweka, lakini Hizb ut Tahrir inawasilisha pendekezo la kisiasa ambalo liko tayari kwa utekelezaji wa haraka. Na hakuna kinachobakia ila kusimama pamoja nasi, kwa hakika nyinyi musimame pamoja na nafsi zenu na Dini yenu kama nusra kwa Mola wenu Mlezi aliye kuahidini ahadi ya kweli, na Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake.

Enyi watu wa Tunisia, tunawahutubieni leo, hasa watu wenye nguvu na ulinzi miongoni mwenu:

Hakuna kazi yoyote leo ambayo mtajiokoa kwayo katika dunia hii na Akhera, isipokuwa kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu ndani ya dola ambayo siasa zake ziko kwenye njia  ya Mtume wenu (saw), na ambayo iko karibu kuliko kufungia macho ikiwa azam iko sahihi. Hakuna kitu baina yetu na ukombozi kamili isipokuwa msimamo kukatikiwa, mithili ya msimamo muliochukua mwaka wa 2011, kuwafukuza vibaraka wote, kukataa usekula, urasilimali, na kila fikra iliyobuniwa na mwanadamu, na kutokubali Uislamu kama badali. Tunakukumbusheni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ)

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka?” [Al-Hadid: 16].

Je, wakati haujawadia wa nyinyi kuuona ukweli na kujua kwamba njia ya ukombozi na mabadiliko iko kwenye Dini yenu, Uislamu wenu?!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.