Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  8 Jumada II 1443 Na: HTY- 1443 / 04
M.  Jumanne, 11 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mahouthi Wawalazimisha Wafungwa Wao Kuachana na Ukinaifu wao wa Kifikra kwa Badali ya Kuachiliwa kwao Huru!

 (Imetafsiriwa)

Karibu mwaka mmoja baada ya kukamatwa kwa Ndugu Mohsen Muhammad al-Jadabi, mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Yemen, bila kosa lolote isipokuwa kufanya kazi ya kuregesha hukmu za Uislamu zitekelezwe katika uhalisia wa maisha ya watu, ili kupata furaha duniani na akhera, licha ya hayo, na baada ya ufuatiliaji wa mamlaka rasmi za kundi hilo, zinazowakilishwa katika Baraza lake Kuu la Kisiasa, ili kutoa risala kwa Mwendesha Mashtaka wa Umma na kuielekeza kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo ilisema kuwa wafungwa miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir walikuwa wameachiliwa huru kwa badali ya dhamana za kibiashara - kama dhamana za uhudhuriaji. Kisha kutenguliwa kwa dhamana ya kibiashara kwa dhamana ya mtu mwenye akili timamu katika kitongoji cha Ndugu Mohsen al-Jadabi, na baada ya kutimizwa ombi lao la kuleta dhamana inayotakiwa, na wakaikubali, wakamtaka kuahidi kuachana na kazi ya Hizb ut Tahrir, lakini akakataa ombi hili na matokeo yake wakamrudisha gerezani!

Ombi la Mahouthi kutoka kwa wafungwa miongoni wa wafanyakazi wa Hizb ut Tahrir kuacha kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ni ombi la haramu na lililo kinyume na sheria. Bali ni aina ya vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw), na ukaidi dhidi ya wabebaji da’wah. Vyenginevyo watawafungaje wale wanaofanya kazi ya kusimamisha dola inayotekeleza Uislamu na kuondoa mipaka iliyowekwa na ukoloni miongoni mwa Waislamu?! Je, kitendo hiki ni jinai inayoadhibiwa kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir?! Mnahukumu vipi?! Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 (وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ)  “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Aali-Imran: 103]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

 (وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ) “Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao.” [Al-Ma‘idah: 49].

Bali, wanapaswa waelekeze mishale yao kwa Magharibi Kafiri, ambayo inafanya kazi asubuhi na usiku kuwagawanya Waislamu, kuwasambaratisha, kuchochea ugomvi wa kimadhehebu baina yao, na kupora mali zao. Je, haitoshi kwa Waislamu kutokana na yale wanayopata kutoka kwa Magharibi Kafiri kuongeza dhuluma zaidi kwa tawala zilizopo katika nchi za Kiislamu?!

Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, hataanguka katika majaribio ya kukata tamaa yanayofanywa na wengine kuwafikia wafanyakazi wake. Hizb ut Tahrir, kama inavyojulikana kwa Ummah, ni chama cha kisiasa kinachoendesha shughuli zake katika zaidi ya nchi 40 kote duniani. Uislamu ndio mfumo wake, na siasa (kuchunga mambo) ndio kazi yake. Na njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yake, ndio njia yake ya kusimamisha utawala katika Uislamu.

Mahouthi na wengineo na wajue kwamba kazi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume inayotabikisha Uislamu ni faradhi juu yao kabla ya kuingia madarakani na baada ya kuyafikia. Ni lazima watabikishe Uislamu na wao ndio wanaodai njia ya Qur'an, na Hizb ut Tahrir itaendelea kufanya kazi kikamilifu maadamu Uislamu haupo kwenye utawala na hakuna dola yenye kuutekeleza nchi Yemen na nchi nyengine za Waislamu, mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu ajaalie Nusra yake na tamkini yake kupitia mja wake mwema kwa kutimiza ahadi yake na bishara ya Mtume wake (saw).

Hizb ut Tahrir imechukua hatua ya kusimamisha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, kama kadhia nyeti ambayo itasababisha kifo na uhai, na ambayo inawezekani kufikiwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

 (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao.” [An-Nur: 55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.