Jumamosi, 26 Ramadan 1442 | 2021/05/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 SHERIA IMECHINJWA TENA, WAZO LA KHILAFAH LINAONEKANA KUWA NI UHALIFU

(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa, 02/04/2021, sheria ilichinjwa tena kwa kesi ambayo ilianzishwa kwa sababu ya Kongamano la Khilafah nchini Uturuki mnamo 2017 lakini haikufanyika kwa sababu ya kuzuiwa na utawala.

Mahakama Kuu ya Jinai ya 30 ya ISTANBUL imewahukumu wazungumzaji hao wanne kwa kifungo cha gerezani cha miaka 31 na miezi 3.

Kongamano hilo lililopewa anwani "Kwa nini Ulimwengu Unahitaji Khilafah?" lililopangwa kufanywa na Jarida la Koklu Degisim lilizuiwa bila ya sababu yoyote ya msingi, na mchakato wa uamuzi ulianzishwa kuhusiana na

Kwenye usikilizwaji wa uamuzi uliofanyika Ijumaa tarehe 02/04/2021 wa kesi hiyo iliyofanywa na Mahakama Kuu ya Jinai ya 30 ya Istanbul, mzungumzaji wa kongamano Mahmut KAR alihukumiwa miaka 12.5, Abdullah Imamoglu, Musa Bayoglu na Osman Yildiz miaka 6 na miezi 3 kila mmoja. Kwa kuongezea, uamuzi ulitolewa wa kuwapiga marufuku watu wote kutoka kwenda nje ya nchi. Uamuzi huo ulitolewa na jaji kutoka kwa jopo la mahakama kwa maoni ya upinzani, yaani, kura  za wengi.

Kufuatia hukmu hiyo, Mahmoud Kar, Abdullah Imamoglu, Musa Bayoglu na Osman Yildiz walisambaza ujumbe wa video.

Upande wa mashtaka haukuweza kufichua uhalifu wowote wa kihakika unaohusiana na washtakiwa

Katika kikao cha usikilizaji wa hukumu, Mahmut Kar, mwandishi wa theolojia Abdullah Imamoglu, Musa Bayoglu na Osman Yildiz walifanya utetezi ambao ulikanusha madai yaliyotolewa kwa maoni ya upande wa mashtaka mmoja mmoja. Walielezea wazi kwamba Hizb ut Tahrir inapinga nguvu na vurugu, na haisemi neno lolote la kushajiisha ugaidi, pia walisisitiza kwamba mtu hawezi kudai adhabu kali kutokana tu na kongamano ambalo halijafanywa na adhabu hizi nzito haziko sambamba na sheria na maadili. Tena, walitangaza kuwa Sheria ya Kupambana na Ugaidi inayotekelezwa iko wazi, kwamba vitendo na shughuli zao hazihusishi vurugu na ugaidi haziwezi kuzingatiwa kama uhalifu, kwa hivyo madai ya upande wa mashtaka hayana mashiko.

Mawakili wa washtakiwa Kaya Kartal, Ahmet Sait Öner na Mehmet Alagöz walitoa utetezi wa kina kwa jopo la mahakama. “Shirika la kigaidi ni aina ya shirika lenye nia ya kisiasa ambalo hutenda kupitia shinikizo, vitisho, ugaidi, ukandamizaji au tishio kwa kutumia nguvu na vurugu. Hizb ut Tahrir sio shirika katika muktadha huu.” Dhihirisho rahisi zaidi la kupingana na kutokubaliana kwa serikali na mahakama kuhusu Hizb ut Tahrir ni kwamba watu walio na ukaribu na shirika hili waliadhibiwa kama wanachama wa "shirika haramu" na kisha "shirika la kigaidi lisilo na silaha" na, hivi karibuni, "shirika la kigaidi lenye silaha". Katika kipindi chote cha kesi, njia ya utendakazi ya Hizb ut Tahrir ni ile ile. Japokuwa njia ya utendaji ya Hizb ut Tahrir ilikuwa ni ile ile na sheria zilibadilika wakati huu, mahakama daima ilipata njia na adhabu ziliendelea na viwango vya faini viliongezwa."

Raisi wa Mahakama Alisoma Hukumu, akisema, "Faili Hii Haina Ubishi!"

Baada ya jopo la Mahakama Kuu ya Jinai ya 30 kuchukua utetezi na mapumziko na kuelezea uamuzi huo: "tulizungumza, tukatathmini kwamba Hizb ut Tahrir ilikuwa shirika la kigaidi." Mkuu wa mahakama, ambaye hakutoa uthibitisho wa maana kwamba Hizb ut Tahrir ni shirika la kigaidi, alitangaza uamuzi huo, akisema: "Faili hii haina ubishi."

Sheria Imechinjwa kwa Mara Nyengine Tena!

Katika kesi hii, ambayo ilianza mnamo 2017 na bado ingali inaendelea, Idara ya Kuadhibu nambari 9 ya Mahakama ya Upeo, imekosolewa waziwazi kwa mara nyengine tena na AYM, ikisisitiza maamuzi haramu ya kesi ya sheria iliyofanya juu ya Hizb ut Tahrir mnamo 2004 na 2008 na upande wa mashtaka, ambao unategemea sheria hizi za kesi zenye kuzingatiwa, haukuulizwa uthibitisho wa kisawa sawa. Upande wa mashtaka vilevile, haukuzingatia maoni ya upinzani ya Mustafa Kurtulan ambaye ni mwanachama wa Mahakama ya Upeo. Huku mahakama ikitegemea maamuzi ya Mahakama ya Upeo dhidi ya kanuni na sheria, haikuzingatia jumla ya maamuzi 8 tofauti ya ukiukaji yaliyotolewa na Mahakama Upeo ya kuegemea kwa Hizb ut Tahrir, ambayo yalikosoa maamuzi haya haramu ya sheria ya kesi.

Kwamba mmoja wa wanachama wa mahakama aliwasilisha upinzani wake na uamuzi huo ukachukuliwa na wengi inaonyesha wazi hukmu hizi zisizo halali zaidi ya hayo utata na hali ya ghafla dhidi ya Hizb ut Tahrir. Lakini, katika faili zingine za Nzito za Mahakama ya Jinai ya Istanbul, Ankara na Sanliurfa, inajulikana kuwa maamuzi ya kuachilia huru yalitolewa kwa kutangaza kwamba Hizb ut Tahrir sio shirika la kigaidi bali muundo wa kiraia.

#YargıZulmüneDurDe

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Uturuki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu