Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika Yaosha Dhambi Zake Juu ya Mgogoro wa Hali ya Hewa kwa Kuzihonga Nchi za Kiislamu za Kusini Mashariki mwa Asia

(Imetafsiriwa)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Retno Marsudi alisema Amerika imejitolea kutoa msaada wa dolari za Amerika milioni 102 (IDR trilioni 1.44) kwa nchi za ASEAN katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Kauli hiyo ilitolewa na Retno baada ya kuhudhuria Mkutano wa mtandaoni wa kati ya Amerika na ASEAN mnamo Jumatano (27/10/2021). "Kupanua ushirikiano na ASEAN, haswa katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, na kutangaza usaidizi wenye thamani ya dolari milioni 102 (sawa na IDR trilioni 1.44) kwa ajili ya mipango mipya," Retno alisema katika mkutano wa waandishi wa habari kupitia YouTube. Amerika itatoa msaada katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa kabla ya Kongamano la Mabadiliko ya Hali ya Hewa la COP26 jijini Glasgow, Uingereza, kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 12. Amerika ni miongoni mwa nchi 35 tajiri ambazo zimeahidi kutoa dolari za Kiamerika bilioni 100 (IDR 1,432 trilioni) kwa Nchi zinazoendelea.

Hatupaswi kusahau kwamba Amerika ni nchi ya pili kwa ukubwa duniani kutoa kaboni baada ya China, hivyo ni mojawapo ya wachangiaji wakubwa wa uharibifu wa mazingira kote duniani. Mfuko wa usaidizi si chochote zaidi ya jitihada za kuosha dhambi zake kwa kuzilipa nchi za tropiki ambazo ni kama mapafu ya dunia.

Zaidi ya hayo, Amerika ilitoa msaada huu katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa kabla ya Mkutano wa COP26 wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa huko Glasgow, Uingereza. Inaonekana kuna hisia kali kwamba Amerika inasita kulaumiwa kwa kubeba mzigo wa uharibifu wa hali ya hewa duniani kote. Ni kwa sababu, hadi leo, Amerika imekuwa ikisita kuidhinisha Itifaki ya Kyoto kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa hivyo, hatua hii iliyochukuliwa na Amerika ni wazi kuokoa tu sura yake mbaya.

Ni wazi kwamba Amerika haiko tayari kujitolea kukabiliana na mgogoro wa hali ya hewa, na wakati huo huo, inasita kulaumiwa. Wakati huo huo, uharibifu wa hali ya hewa ya kimataifa ni matokeo ya utabikishaji wa Urasilimali ambao unatanguliza maslahi ya uchumi wa viwanda kuliko maslahi ya wanadamu na mazingira. Nchi zilizoendelea za kiviwanda zinaonekana kusita kuwajibika, ingawa ndizo zinazotoa hewa nyingi zaidi za CO2 duniani.

Nchi za Kiislamu hazipaswi kukubali usaidizi wowote kutoka kwa nchi za makafiri na zisipofushwe na dolari kutoka Amerika, kwa sababu si chochote zaidi ya 'hongo' ili kuimarisha msimamo wa Amerika. Kama nchi ya Kiislamu, tunapaswa kuchukua mafunzo makubwa kutokana na ujinga, kiburi, na kutowajibika yaliyoonyeshwa na nchi hizi za viwanda zisizo na soni. Hao si chochote zaidi ya mafisadi duniani wanaoendelea kubishana kwamba wanaleta maendeleo na usasa, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الأرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَكِنْ لَا يَشْعُرُونَ]

“Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui." [Al-Baqarah [2]:11-12].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.