- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hotuba ya Mwanachuoni na Amiri wa Hizb ut Tahrir Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah (Mwenyezi Mungu amlinde)
Katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake, na wale wanaomfuata.
Kwa Ummah wa Kiislamu, Ummah wa Jihad, uadilifu, na ukarimu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu—Ummah bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu—Mwenyezi Mungu aupe ushindi na tamkini.
Kwa wabebaji ulinganizi wa kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida - na tunawachukulia, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kuwa wachamungu, wasafi, watukufu, na waliobarikiwa.
* Katika siku hizi kama hizi, miaka 105 iliyopita, mwishoni mwa Rajab 1342 H, sambamba na mapema Machi 1924 M, wakoloni makafiri, wakiongozwa na Uingereza wakati huo, kwa ushirikiano na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, waliweza kuivunja Khilafah. Mhalifu wa zama hizo, Mustafa Kemal, alitangaza ukafiri wa wazi kwa kuifuta Khilafah, kumzingira Khalifa jijini Istanbul, na kumfukuza alfajiri siku hiyo hiyo. Hivyo, tetemeko baya la ardhi lilizikumba ardhi za Waislamu kwa kuvunjwa Khilafah, chimbuko la izza yao na radhi ya Mola wao Mlezi. Ilikuwa ni juu ya Umma kumpiga kwa upanga, kama ilivyoelezwa katika Hadith iliyopokewa na Bukhari na Muslim ya Mtume (saw) kutoka kwa Ubada ibn al-Samit, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, ambaye alisema,
«وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ»“Na tusizozane na mamlaka ya wenye mamlaka isipokuwa mukiona ukafiri ulio wazi ambao nyinyi mna dalili kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Lakini Ummah ulipungukiwa katika hili, na haukufanya kile ambacho kingemzuia mhalifu huyo na wafuasi wake na kumshinda yeye na wafuasi wake. Bali tetemeko la kupotea kwa Khilafah liliendelea. Kisha ushawishi wa wakoloni makafiri ukaenea katika ardhi za Waislamu, kwa hivyo waligawanya ardhi hizo na kuzichana vipande vipande vilivyofikia vipande 55!
* Kisha, watawala wa Ruwaybidha (wajinga wasio na maana) katika ardhi za Waislamu waliongeza tetemeko jengine kwenye hili, wakishindwa kuwazuia Mayahudi kuivamia Ardhi Iliyobarikiwa, mahali pa Israa wal Miraj (Safari ya Usiku na Kupaa) ya Mtume. Kisha walizama chini zaidi, wakikimbilia kwenye uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi bila kujiondoa kutoka kwa chochote! Baadhi walitenda uhalifu wa uhalalishaji mahusiano faraghani, huku wengine wakifanya hivyo hadharani, mchana na usiku! Kwa hivyo, wote wanaharakisha kuelekea uhalifu huu, bila kujali udhalilifu unaowazunguka kuanzia kichwani hadi vidoleni.
[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]
“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An’am: 124].
* Hivi ndivyo mlivyo kuwa nyinyi Waislamu baada ya kuvuliwa Khilafah kutoka kwenu, na kutawaliwa na watawala wa Ruwaybidha ambao leo wanachukua amri kutoka kwa Trump dhalimu, hata katika Gaza (ya Hashim) na Ardhi yote iliyobarikiwa. Mnamo Septemba 2025, Trump aliongoza mkutano uliojumuisha Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia, na Pakistan, kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akiuelezea kama mkutano muhimu zaidi. Kisha akawasilisha, au tuseme, akalazimisha mpango wa nukta 20 juu yake. Nukta za mpango wake zilizungumzia mengi kuhusu kupotea kwa Gaza, kutiishwa kwake, na kukoloniwa kwake kuwa uwanja wa nyuma wa kufurahia kwa Trump na umbile la Kiyahudi! Baada ya hapo, Sisi alifanya sherehe nchini Misri (al-Kinanah) kwa ajili ya Trump na mpango wake muovu. Huu ulikuwa utangulizi wa Azimio la Baraza la Usalama nambari 2803, ambalo linalazimisha baraza la udhamini au ukoloni kusimamia Gaza (ya Hashim), ambalo analiita Baraza la Amani! Kisha Trump anatangaza kwamba atatangaza wanachama wa baraza linaloongozwa naye huko Gaza mwanzoni mwa mwaka huu, 2026. Al Jazeera pia ilimnukuu ikisema kwamba Trump anaweza kumteua jenerali wa Marekani kuongoza kikosi cha utulivu katika Ukanda wa Gaza. (Al Jazeera, 11/12/2025). Kwa maana nyengine, Trump anadhibiti baraza la usimamizi na vikosi vya usalama huko Gaza! Kisha, mjumbe wake, Witkoff, anakutana na nchi “za upatanishi”—Uturuki, Misri, na Qatar—huko Miami mnamo 19/12/2025, ili kuendeleza awamu ya pili ya majadiliano kuhusu jinsi ya kupeleka vikosi vya utulivu na kupokonya silaha Hamas, pamoja na kujadili hatua za kivitendo za kutekeleza hili! Kisha, Trump alikutana na Netanyahu huko Florida na kusema: [“Mkutano ulikuwa na natija sana.” Anaongeza kwa waandishi wa habari: “Mazungumzo yalishughulikia suala la kupokonya silaha Hamas, akisisitiza kwamba wanapaswa kupokonywa silaha ndani ya muda mfupi, na kisha (Hamas) watalipia gharama kubwa mno.” (BBC, 30/12/2025)]. Trump anasema hivi huku akilipa umbile la Kiyahudi kila silaha, nzito na nzito zaidi, katika vita vya kikatili dhidi ya Gaza vinavyowadhuru watu, miti, na mawe. Trump anasema na kufanya hivi mbele ya watawala katika nchi za Waislamu ambao wameisaliti Ardhi Iliyobarikiwa kwa kukaa kimya kuhusu ukombozi wake, na hata kumpigia makofi Trump kwa mpango wake wa nukta 20!
* Palestina sio pekee ambayo watawala hawa wamesaliti, pia walisaliti nchi walizozitawala, wakifanya kazi kwa niaba ya na kwa amri ya wakoloni makafiri, haswa Amerika. Sudan Kusini ilitenganishwa na Kaskazini, na Darfur sasa iko kwenye njia hiyo hiyo. Libya pia imeingia katika mzozo na kugawanywa katika dola mbili. Yemen imegawanywa katika Kaskazini na Kusini, na Kusini hata inagawanyika! Syria mpya imejitupa mikononi mwa Amerika, ikiwaachilia huru wasaidizi na majambazi wa utawala wa dhalimu wa zamani huku ikiwaweka kizuizini wanachama wa Hizb ut Tahrir, wanaolingania Khilafah, wakiwafunga na kuwahukumu kwa hadi miaka kumi. Watawala hawa Ruwaybidha (wajinga wasio na maana) hawakuridhika na hili; walisalimisha au kukabidhi sehemu zengine za ardhi ya Uislamu. Kashmir iliunganishwa na washirikina wa Kibaniani. Urusi iliunganisha Chechnya na ardhi zengine za Waislamu katika Asia ya Kati. Timor Mashariki ilichukuliwa kutoka Indonesia. Kupro, ngome ya Waislamu kwa miaka mingi, sasa inadhibitiwa zaidi na Ugiriki. Waislamu wa Rohingya wanauawa nchini Myanmar, na wakitafuta hifadhi nchini Bangladesh, utawala unawakandamiza na kushindwa kuwanusuru kupitia kupigana na adui yao! Kisha kuna Turkestan Mashariki, ambayo China inaishambulia kikatili, kwa ukatili ambao hata wanyama wangeuepuka. Na dola zilizopo katika ardhi za Waislamu ziko kimya mithili ya makaburi; na endapo zitazungumza, zinasema kwamba ukandamizaji wa China kwa Waislamu ni jambo la ndani!
[كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً]
“Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu.” [Al-Kahf: 5]
Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu: Je, hamwezi kufuata nyayo za wale waliokuja kabla yenu katika askari wa Uislamu, na kutimiza faradhi ya Mwenyezi Mungu Al Qawi Al Aziz, kwa kuikomboa Palestina na Gaza (ya Hashim) kupitia jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, kilele cha Uislamu? Na kisha kurudisha kila shubiri ya ardhi ya Waislamu ambayo imekatwa kutoka asili yake au kunyakuliwa na wakoloni makafiri mashariki na magharibi mwa dunia, na kuwafukuza hadi kwenye nchi zao? Je, hamuwezi? Ndiyo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hakika mnao uwezo:
* Nyinyi ni wana wa Umma wa Kiislamu, Umma wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Umma wa Muhajirina na Answar (Wahamiaji na Wasaidizi), Umma wa Khulafaa’ ar-Rashidoon (Makhalifa Waongofu) na wale waliowafuata, kizazi cha Harun al-Rashid, ambao walijibu kuvunja kwa mfalme wa Byzantine mkataba wake na Waislamu na uvamizi wake dhidi yao: “Jibu ni kile mnachokiona, si kile mnachosikia!” na ndivyo ilivyokuwa. Nyinyi ni kizazi cha al-Mu'tasim, ambaye aliongoza jeshi kubwa kumsaidia mwanamke aliyedhulumiwa na mwanamume wa Kirumi, ambaye alipiga kelele, “Ewe Mu'tasim!” Nanyi ni kizazi cha Salahudin, mshindi dhidi ya Makruseda na mkombozi wa al-Aqsa kutokana na unajisi wao mnamo tarehe 27 Rajab 583 H (Oktoba 2, 1187 M).
* Nyinyi ni kizazi cha Muhammad al-Fatih, Amir kijana ambaye Mwenyezi Mungu alimtukuza kwa sifa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kuwa mkombozi wa Konstantinopoli:
«فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا، وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ» “Amir bora zaidi ni Amir wake, na jeshi bora ni jeshi lake!” Ilifunguliwa na yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu na ambariki, mwaka 857 H (1453 M). Ninyi ni kizazi cha Sultani Selim III, ambaye wakati wa utawala wake Marekani ililipa kodi ya kila mwaka kwa gavana wake nchini Algeria kiasi cha dolari 642,000 za dhahabu, pamoja na lira 12,000 za dhahabu za Uthmani, kwa badali ya kuachiliwa huru kwa wafungwa wake walioshikiliwa nchini Algeria na ruhusa ya kupita katika Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania bila kuingilia kati kutoka kwa jeshi la wanamaji la Uthmani. Na kwa mara ya kwanza, Amerika ililazimishwa kusaini mkataba si kwa lugha yake, bali kwa lugha ya Dola ya Uthmani, mnamo tarehe 21 Safar 1210 H (Septemba 5, 1795 M).
* Nyinyi ni kizazi cha Khalifa Abdul Hamid, ambaye alimwita balozi wa Ufaransa jijini Istanbul na kukutana naye kimakusudi akiwa amevaa sare za kijeshi, kisha akamtishia kusimamisha tamthili iliyomtukana Mtume Muhammad (saw), akisema, “Mimi ni Khalifa wa Waislamu... Nitageuza dunia chini juu chini vichwani vyenu msipokomesha tamthilia hiyo.” Ufaransa ilitii na kuipiga marufuku mwaka 1307 H (1890 M). Nyinyi ni kizazi cha Khalifa huyu ambaye hakushawishiwa na mamilioni ya sarafu za dhahabu zilizotolewa na Mayahudi kwa Hazina ya Dola (Bayt ul-Mal), wala hakuogopeshwa na shinikizo la kimataifa waliloliandaa dhidi yake ili kuwaruhusu waishi Palestina. Alisema maneno maarufu, “Ni rahisi kwangu kukatwa vipande vipande mwili wangu kuliko kuona Palestina ikikatwa kutoka Khilafah.” Alikuwa na mtazamo wa mbele, akiongeza, “...Waacheni Mayahudi wabaki na mamilioni yao... Iwapo Khilafah itachanika, basi wanaweza kuichukua Palestina bure.” Na hivyo ndivyo hasa ilivyotokea!
Enyi Waislamu! Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu! Endapo Khilafah itarudi, mtarudi kwenye izza ya mababu zenu, kwani matendo yao yanazungumzia nguvu zao na radhi kubwa ya Mwenyezi Mungu. Walisimamisha Khilafah na kuihifadhi, kwa hivyo waliheshimiwa na kushinda na kupata radhi ya Mola wao Mlezi. Nyinyi ni kizazi chao, kwa hivyo njooni kwenye haki waliyoifuata na muifuate, na kwenye izza waliyoileta na muilete. Regesheni Khilafah na muihifadhi. Hizb ut Tahrir iko miongoni mwenu, kwa hivyo inusuruni kwani inafanya kazi mchana na usiku kuregesha mtindo wa maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida. Inaongoza Ummah na kuupa uongofu kwenye kazi hii kubwa, na inawakosesha usingizi wakoloni makafiri kwa ulinganizi wake wa Khilafah. Kwa hivyo, nini kitatokea Khilafah itakaposimamishwa na kuondoa mipaka na vizuizi vilivyowekwa na wakoloni makafiri kutoka kingo za Bahari ya Pasifiki, ambapo Indonesia na Malaysia zipo, hadi fuo za Atlantiki, ambapo Morocco na Andalusia zipo?! Kisha Waislamu watarudi kuwa Umma mmoja chini ya dola moja, Khilafah Rashida ambayo itakirimu Uislamu na Waislamu, na kudhalilisha ukafiri na makafiri. Itaregesha ardhi za Uislamu na Waislamu kutoka mikononi mwa makafiri wanaowakoloni, kuwaandama hadi kwenye kina cha ardhi zao wenyewe, na kuuangaza upya ulimwengu. Siku hiyo, haki itatawala na batili itaangamia.
[وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً]
“Na sema: Haki imefika, na batili imetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!” [Al-Isra: 81].
* Inaweza kuulizwa, “Je, Khilafah inatimiza haya yote? Je, itapata ushindi na kurudisha nyuma kushindwa?” Je, itazikomboa ardhi za Waislamu kutoka kwa makafiri wanaotawala na hata kuwaandama hadi kwenye ardhi zao wenyewe?” Tunasema, “Ndiyo, Mola wetu Mlezi, Aliyetukuka, anasema hivi
[إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].” Ushindi wa kweli wa Mwenyezi Mungu unaweza kupatikana tu kupitia kusimamishwa kwa dola ya Uislamu inayotabikisha Sheria Zake. Pindi inapoasimamishwa, Mwenyezi Mungu (swt) huipa ushindi, na inakuwa imara na yenye nguvu, ili washirika wake waiheshimu na maadui zake waiogope. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema hivi: «الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam ni ngao ambayo watu wanapigana nyuma yake na watu wanalindwa kwaye.” Khalifa na Khilafah ni ngao, yaani, ulinzi. Na yeyote mwenye ulinzi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, atashinda mwishowe; ardhi yake haitapotea, na maadui zake hawatamkaribia. Historia ya Khilafah inashuhudia hili. Byzantium iko wapi na fimbo yake ya ufalme? Ctesiphon na Khosroes ziko wapi? Na ni nani mwengine isipokuwa Dola ya Kiislamu, askari wa Uislamu, na uadilifu wa Uislamu waliopaza wito wa Takbir katika nchi hizo kubwa zinazoenea kutoka bahari hadi bahari? Lau Khilafah ingezijua ardhi zilizo ng'ambo ya bahari mbili, mashariki na magharibi, ingevuka vina vyake, ikilingania kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Uwezo Wote, Mwenye Nguvu Zote, Mwenye Hekima Zote.
* Inaweza pia kusemwa kwamba Hizb ut Tahrir haina bidhaa nyengine isipokuwa Khilafah; popote inapokwenda, inazungumzia Khilafah pekee, haijui chengine chochote, na haitambui chengine chochote. Tunasema, ndio, Khilafah kwa kweli ni bidhaa yake na mradi wake; ni izza yake na nguvu yake; ni mlinzi wa Dini na maisha ya kidunia; ni msingi na dhati. Kupitia hiyo, hukmu husimamishwa, mipaka hufafanuliwa, ufunguzi hufikiwa, na vichwa huinuliwa katika haki. Hayo ndiyo Waislamu walivyoanza nayo kabla ya kuanza kumuandaa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na mazishi yake, rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, licha ya umuhimu na ukubwa wa hilo, na yote hayo yalitokana na ukubwa na umuhimu wa Khilafah, kwani Maswahaba wakubwa waliona kwamba kushughulika nayo ni muhimu zaidi kuliko wajibu huo mkubwa: kuandaa mazishi ya Mtume (saw).
Enyi Waislamu! Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu: Kusimamishwa kwa Khilafah ni suala nyeti la Waislamu. Tuna uhakika katika ushindi wa Mwenyezi Mungu, katika izza ya Uislamu na Waislamu, katika kurudi kwa Khilafah Rashida, katika kuangamizwa umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu Palestina, na katika kufunguliwa kwa Roma kama ilivyofunguliwa Konstantinopoli na Istanbul zikawa makaazi ya Uislamu (Dar al-Islam). Sisi tuna uhakika nayo, hata kama makafiri na wanafiki watasema kinyume chake,
[إِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ]
“Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya.” [Al-Anfal: 49]. Ushindi huu wote kwa Waislamu ni katika ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt).
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi” [An-Noor: 55]. Na bishara njema ya Mtume Wake (saw) baada ya utawala huu wa kidhalimu ambao tunaishi ndani yake:
«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَت»
“Kisha kutakuwa na utawala dhalimu, na utadumu kwa muda wote ambao Mwenyezi Mungu atautaka udumu. Kisha atauondoa atakapotaka kuuondoa. Kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha akanyamaza. (Musnad Ahmad). Kwa hivyo Khilafah bila shaka itarudi, Mwenyezi Mungu akipenda. Hata hivyo, inahitaji kazi nzito na ya bidii ili kuisimamisha. Kwani sunnah ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye Hekima, ameamuru kwamba Hatawatuma malaika kutoka mbinguni kuisimamisha Khilafah kwa ajili yetu na kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Aliyetukuka, na bishara njema ya Mtume Wake (saw) huku tukikaa tu bila kufanya kazi. Badala yake, Atawatuma malaika kutusaidia tunapofanya kazi kwa kujitolea, kwa bidii, kwa ukweli, na kwa dhati. Kisha Mwenyezi Mungu (swt) atatupa ushindi na mafanikio katika ulimwengu huu na akhera, na huo ndio ushindi mkuu. Hizb ut Tahrir inafanya kazi kwa bidii kwa ajili yake, inatarajia kusimama kwake hivi karibu. Kwa hivyo, harakisheni, enyi Waislamu! Harakisheni, enyi watu wenye nguvu! Jiunge na ulinganizi na muunusuru, na muharakishe kusimamisha Khilafah pamoja na hizb, sio kushuhudia tu kutoka kwao. Kwani ushindi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, uko karibu.
[إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]
“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq:3]
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].
Dua yetu ya mwisho ni kusema sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Walimwengu.
Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh.
Ndugu Yenu Mpendwa,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Rajab 1447 H
Januari 2026 M