Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Rambirambi za Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na Wafanyikazi wake wote

((وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُواْ إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ))

“Na wabashirie wanao subiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Baqara: 156-7]

G en

Tumepokea habari za kifo cha dada mwema Gamze Gürsoy / Zahra Malik (mwanachama wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari); kwani Mwenyezi Mungu alimchukua asubuhi ya leo, Ijumaa, 09 Shawwal 1447 H, sambamba na 27/03/2026 M. Tunamwomba Mwenyezi Mungu, Mwenye rehema na Msamaha, amfunike katika rehema zake kubwa, amjalie radhi na msamaha wake, na amjalie makaazi katika Peponi Yake kubwa pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, na wema, na  wanandani wema walioje hao. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awape familia yake na wapendwa wake subira na faraja, na asiwanyime ujira wake, wala kuwajaribu baada yake, Amin.

Alijitolea maisha yake kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu hapa duniani na alikuwa msukumo kwa wengi kwa maneno yake na kujitolea kwake kwa Dawah. Hakudhoofika kamwe katika ulinganizi huu licha ya changamoto na matatizo mengi aliyokabiliana nayo maishani. Mwenyezi Mungu amjalie thawabu na nafasi ya juu zaidi huko Jannah. Amin

إنا لله وإنا إليه راجعون

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Baqara: 156-7]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ijumaa, 09 Shawwal 1447 M sawia na 27/03/2026 M

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.