Jibu la Swali: Mkakati wa Amerika na Suluhisho la Dola Mbili
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tunajua kwamba mkakati wa Marekani wa kuasisi umbile la Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu, kwa sehemu kubwa, umeegemezwa kwenye suluhisho la dola mbili. Hata hivyo, chini ya Trump, mkakati huu umeanza kuatelekezwa, au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo limezua maswali. Kwa mfano, Trump alisema, "Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, 'Israel' ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa mno. Kwa hakika nilisema: 'Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo..." (Sky News, 19/8/2024). Je, hii inamaanisha kuwa mradi wa suluhisho la dola mbili wa Amerika umekufa na kukamilika, au bado ungali hai?