- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi “Nusra kwa Al-Aqsa na Wafungwa”
Mnamo siku ya Ijumaa, 3 Aprili 2026, matembezi yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia, mji mkuu wa Tunisia, yalianza kutoka Msikiti wa Al-Fath baada ya swala ya Ijumaa. Matembezi hayo, yaliyofanyika kwa ajili ya kuunusuru Msikiti wa Al-Aqsa na wafungwa wa Palestina, yalikuwa na kichwa:
“Kuhamasisha majeshi, kupindua viti vya watawala, na kutangaza jihad ndiyo njia pekee ya kuwaokoa wafungwa na kuikomboa Masra.”
Matembezi hayo, yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wakaazi, yalianza kwa miito ya “Tunakuitikia Tunakuitikia, Tunakuitikia Ewe Al-Aqsa!” na “Ewe Al-Aqsa, tunajibu wito wako, watu wote wa Tunisia wako pamoja nawe!” Mabango yaliinuliwa, moja likiwa na kichwa cha matembezi na jengine likisomeka, “Enyi Waislamu: Nani atasimama kwa ajili ya wafungwa wakati mti wa kunyongea utakapowekwa kwa ajili yao?” Katika matembezi yote, yaliyopita katika barabara za mji mkuu, washiriki waliimba kaulimbiu zinazowahimiza jamii ya Waislamu na watu wake waaminifu wenye nguvu kuchukua hatua, kama vile: “Al-Aqsa inawaita Waislamu... Ghera iko wapi? Dini iko wapi?”, “Aibu, aibu... Kunyongwa kwa wafungwa Wallahi ni aibu!”, “Enyi Maafisa na viongozi... Al-Aqsa inawaita jihadi!”, na “Al-Aqsa inawaita watu huru... Nani ataivunja MzingirO huu,” “Enyi majeshi, Enyi watu huru... nani anayewajali wafungwa?” “Enyi majeshi ya Waislamu... wafungwa ni ndugu zenu katika imani,” “Enyi majeshi ya Waislamu... jihad huko Palestina,” “Enyi majeshi ya jihad... Mola wa viumbe vyote atawapa ushindi,” “Hakuna ukombozi, Enyi majeshi... isipokuwa kwa kupindua viti vya watawala.” Matembezi hayo yalimalizika katika Barabara ya Al-Thawra mbele ya Ukumbi wa Manispaa kwa mkutano ambapo mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir - Wilayah ya Tunisia - alitoa hotuba ambapo alielezea kwamba wajibu wa Umma wa Kiislamu leo ni sawa na jana; Lazima ufanye kazi, si tu kwa kuhukumu na kushutumu, bali pia kuwasha katika majeshi yake ari ya imani, kuwasha harara ya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kupindua viti vya enzi vya watawala wake, wakielekea Msikiti wa Al-Aqsa, wakiukomboa na huku wakibiga takbira: ﴿وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً﴾ “na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” Kitendo chochote kisichohusiana na wajibu huu ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, mahali pa Safari ya Usiku(Masra) ya Mtume (saw), na damu ya watu wa Palestina na wafungwa wao.
Umbile la Kizayuni na wahalifu wake waovu zaidi ni duni sana kuweza kuumiliki Msikiti wa Al-Aqsa. Mwenyezi Mungu ameamuru, ﴿وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ﴾ “na wamepigwa na unyonge na fedheha.” na ameamuru, ﴿لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ﴾ “Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.”, na ameamuru, ﴿وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَى حَيَاةٍ﴾ “Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu wote kwa pupa ya kuishi.”
Hii ni kazi ya Hizb ut Tahrir katika nchi ya Zaituna; huu ni wajibu wake kwa Umma wake na watu wake wenye nguvu: kuwaamsha, kufafanua hukmu za Kiislamu zilizo juu yao, na kuondoa pazia la ujinga ili waweze kuzitambua na kuzikumbatia, kuinuka kama kitu kimoja, kusimamisha dola ya Kiislamu, kuwakomboa wafungwa na maeneo matakatifu, kung'oa umbile la Kizayuni, na kueneza ujumbe wa Uislamu kama mwongozo na nuru kote ulimwenguni.
﴿وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴾.
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.”
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Ijumaa, 16 Shawwal 1447 H – 03 Aprili 2026 M

https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/5322.html?print=1&tmpl=component#sigProId7b63dc12d1

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Gazeti la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Gazeti la Tahrir
