Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nyumba ya Al-Sabah, Watawala wa Kuwait

Habari:

Sheikh Sabah Al Ahmad Al Sabah, mtawala wa Kuwait alifariki tarehe 29 Septemba 2020 akiwa na umri wa miaka 91 wakati akipatiwa matibabu nchini Amerika. Kifo chake kilipokelewa na rambirambi kutoka kwa viongozi kote ulimwenguni ikiwemo Amerika na Israeli. Alijulikana maarufu kama "mtu mwenye busara eneo hilo" na watawala wenzake wa Kiarabu. [1] [2]

Maoni:

Nyumba ya Al-Sabah imekuwa ndio watawala wa Kuwait tangu karne ya 18. Waingereza kabla ya Vita vya Kwanza vya Ulimwengu walitia saini Mkataba wa Anglo-Ottoman mnamo 1913 kulegeza nguvu ya Khilafah Uthmani juu ya eneo la Kuwait ambayo mwishowe ilisababisha kuundwa kwa dola ya kitaifa ya Kuwait. Itifaki ya Uqair (1922) iliyowekwa na Percy Cox, Kamishna Mkuu wa Uingereza chini Iraq, na kufafanua mipaka ya Kuwait ya kisasa na kumaliza mizozo ya mpaka kati ya nchi jirani za Iraq na Najd. Nyumba ya Al-Sabah imekuwa ikihudumia maslahi ya Uingereza tangu kuundwa kwa dola ya Kuwait. Wakati Amerika ilipoibuka kama dola kuu ya baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ilijaribu kulishawishi eneo hilo na kupata mwanya wa mafuta ya Iraq. Vita vya Ghuba (1991) ambavyo Kuwait ilitishiwa kuunganishwa na Saddam Hussein ilitumika kama kisingizio kwa Amerika kupata udhibiti wa eneo hili kutoka Uingereza chini ya pazia la ukombozi wa Kuwait.

Kwa kuzingatia muktadha huo hapo juu, dori ya Nyumba ya Al-Sabah na muungano wake na maadui wa Uislamu inaweza kueleweka. Sheikh Sabah alitumikia maslahi na sera za dola za kigeni. Haishangazi kwamba Sheikh Sabah, wiki moja tu kabla ya kifo chake, alipewa Tuzo la Heshima na Donald Trump kwa kutambua dori yake aliyoicheza Mashariki ya Kati na ulimwenguni [3]. Uaminifu huu wa Sheikh Sabah na Nyumba ya Al-Sabah ndio uliomfanya Trump atoe maoni hivi majuzi kwamba Kuwait itafuata Bahrain katika kusawazisha mahusiano na 'Israeli'.

Nyumba ya Al-Sabah pamoja na madhalimu wa sasa wa Kiarabu ni washirika katika uhalifu wa khiyana dhidi ya Ummah.

Walishirikiana na Waingereza dhidi ya Khilafah Uthmani na kushirikiana nao kuwaua na kuwapiga mabomu Waislamu wasio na hatia wa Iraq, Yemen na Syria. Enyi Waislamu! Hekima iko katika kushikamana na Shariah na kuachana na muungano wa maadui wa Uislamu, hivyo ndugu wapenzi, wakataeni wasaliti na muwaunge mkono wale wenye busara na ikhlasi ambao wanalingania kusimamisha Hukm ya Mwenyezi Mungu (swt) ardhini kupitia kusimamisha Khilafah Rashida! Mmoja wa Tabi'een wakubwa, Ibrahim Nakhai (rah), alipopokea habari za kifo cha Hajjaj bin Yusuf, alilia kwa furaha. Hajjaj bin Yusuf hakutabikisha sheria za kikafiri, wala hakushirikiana na makafiri. Ikiwa hilo ndilo lililokuwa jibu kwa kifo cha Hajjaj la vizazi bora, basi jibu litakuwa ni lipi kwa yule aliyeshirikiana na makafiri na kutabikisha sheria za Taghut.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ)

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Maida: 51]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Fattaah ibn Farooq

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.