Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Madini ni Mali ya Umma: Ni Umma Pekee Ndio Unaopaswa Kunufaika Sio Kampuni za Ufyonzaji za Kirasilimali

Habari:

Mnamo tarehe 13/10/2020, Shirika la madini la Twiga Minerals Corporation, ambalo linasemekana kuwa ubia kati ya serikali ya Tanzania na shirika la dhahabu la Barrick Gold Corporation (NYS: GOLD) (TSX: ABX), limelipa mgao wa pesa taslimu wa $250 milioni kulingana na kujitolea kwa Barrick katika ushirika huo.

Maoni:

Barrick iliimiliki kampuni ya zamani ya Madini ya Acacia nchini Tanzania kufuatia mizozo kati ya Acacia na serikali ya Tanzania. Imesema kuwa ililipa takriban $205 milioni kwa serikali kama kodi, mrabaha na migao chini ya makubaliano ya pande hizo mbili ya kumaliza mizozo ya kabla ya Barrick.

Mgao huu mdogo ambao serikali iliuchukua kwa ajili ya ushindi sio chochote isipokuwa kofi kwa watu. Ikumbukwe kwamba mnamo 2017 serikali ya Tanzania iliunda kamati maalum ya kuchunguza juu ya uwekezaji wa sekta ya madini, wakati huo iligundua kwamba Acacia ambayo iliendesha migodi mitatu nchini Tanzania: huko Bulyanhulu, Buzwagi, na Mara Kaskazini ilikuwa na kodi ambayo haijalipwa ya $40 bilioni na zaidi ya $150 bilioni ya faini na riba inayodaiwa kukifanya kiwango jumla kiwe $190 bilioni.

Hii inaonyesha jinsi kampuni za Kirasilimali zinavyo endesha shughuli zake katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, chini ya jina la biashara huru na ubinafsishaji, Wakoloni wa kirasilimali kupitia kampuni zao hutumia rasilimali za nchi masikini pasi na aibu. Acacia ililazimika kulipa kodi ya $190, badala ya kuilipa Barrick ambayo inamiliki asilimia 64 ya hisa za Acacia ilimiliki hisa zilizobaki mnamo 2019 na kuunda pamoja na serikali kampuni mpya, Twiga Minerals ikiacha kodi ya $190 bilioni bila kulipwa.

Huku kampuni tajiri za Warasilimali kama hizi zikiwatumia wanasiasa walafi katika nchi zinazoendelea kufyonza rasilimali kwa njia huru, watu masikini katika nchi hizi wanalemewa na mzigo wa kodi katika biashara zao ndogo ndogo za kuku mchumia mdomo. Ikiwa huu sio ufisadi vipi serikali inawe kukubali wizi wa $190 bilioni kutoweka hewani!

Uhusiano wa bwana na mtumwa kati ya nchi masikini na za kikoloni unaelezewa vyema katika hali hii, huku nchi masikini kama Tanzania kiuhalisa zikiwa hazina la kusema juu ya uwekezaji wa wakoloni, kampuni za kimataifa za kimagharibi sio tu zinapora rasilimali bali zaidi zinaamua kila kitu kwa maslahi yao. Ni hali ya kusikitisha kwamba wakati umma unachukua hatua dhidi ya uwekezaji huu na kampuni hizi za ufyonzaji za kimagharibi, viongozi wa kisiasa husimama kufanya chochote ili kupoza hasira zao.

Ni chini tu ya nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu pekee inayotabikishwa na dola ya Kiislamu (Khilafah Rashidah) ndipo Umma utakaponufaika na rasilimali zake nyingi kwani rasilimali zote za umma kama madini huzingatiwa kuwa mali ya umma ambayo kamwe haitabinafsishwa kunufaisha wachache.                                                                                    

Mtume (saw) amesema:

«المسلمون شركاء في ثلاث: في الماء، والكلأ، والنار»

“Waislamu na washirika katika vitu vitatu: katika maji, malisho na moto”. (Sunan Abu Dawud)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 18 Oktoba 2020 21:30
Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.