Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kila Mmoja ni Lazima Atazame Ameandaa Nini Kesho, Wewe Pia Erdogan!

Habari:

Rais Erdogan, ambaye amehudhuria mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani Mast Yilmaz, alisema: “Kwa maombi, rais wetu amefariki kwenda katika uzima wa milele. Mwenyezi Mungu amsamehe mapungufu yake. Kila nafsi hai itakufa siku moja… Tunahitaji kujiandaa kwa ajili Akhera. Kama ambavyo tuko hapa kwa mazishi ya Bwana Mesut, sisi pia tutafikwa na mwisho huu huu. Mwenyezi Mungu atujaaliye tuwe tayari kwa mapumziko haya ya jeneza.”

Maoni:

Ukumbusho wa Rais Erdogan kuhusu Akhera hakika ni haki. Lakini sio mtazamo sahihi kutoa maoni kwamba yote anayoyasema Erdogan na kuyafanya ni haki, ingawa maneno haya upande mmoja ni sahihi. Maneno yaliyotajwa yanaweza kuchukuliwa kama "ukweli" ambao unaweza kupatikana katika kila dosari au kosa.

Ni wajibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kujitahidi kwa ajili ya Rehema Yake na kufanya kazi hapa duniani kwa ajili ya Akhera.

]يَٓا اَيُّهَا الَّذ۪ينَ اٰمَنُوا اتَّقُوا اللّٰهَ وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللّٰهَ اِنَّ اللّٰهَ خَبيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ]

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda.  [Surah al-Hashr: 18]

Lakini, Rais Erdogan, ambaye anawakumbusha raia wake juu ya aya hii ya Mwenyezi Mungu, ni wazi anaongea kana kwamba amejisahau na hajui alichofanya. Jinsi gani hali ya Erdogan ilivyo sawa na ukumbusho wa Mwenyezi Mungu katika Aya Yake:

]اَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنْسَوْنَ اَنْفُسَكُمْ وَاَنْتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ اَفَلَا تَعْقِلُونَ]

“Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii?” [al-Baqarah: 44].

Na Erdogan anayetoa wito kwa wenzake kufanya kazi kwa ajili ya Akhera, umejiandaa vipi kwa ajili yake?

Je! Sio wewe na uongozi wako ambao mumeikomboa zinaa chini ya utiifu wa sheria za Ulaya na kuweka msingi wa kuwafanya watu wako kutenda dhambi kwa urahisi?

Je! Sio wewe uliyekaidi vifungu vya Mwenyezi Mungu kwa kuruhusu maelfu ya madanguro kuendeshwa?

Je! Sio wewe na uongozi wako mulioyachukulia maslahi kuwa kama jambo la lazima na halali?

Vijana, wakiwa katika umri muhimu wa maisha yao, wanashuka kutoka kwa rehema za Mwenyezi Mungu siku hadi siku kutokana na fikra ya usasa na uhuru, ambazo ni zao chungu la Magharibi.

Je! Sio wewe na uongozi wako mliotoa njia ya kuvunjika kwa familia, iliopelekea vijana kuburuzwa katika ukahaba mchafu? Kwa kuongezea, sio wewe na uongozi wako ambao mumetunga Mkataba wa Istanbul, ambao unahakikisha haki za mashoga kuheshimiwa kikamilifu?

Je! Sio wewe na uongozi wako mliotabikisha bahati nasibu na kamari kupitia utekelezaji wa dola ambayo yameharamishwa na Mwenyezi Mungu? Je! Sio nyinyi mliotangaza na kuuza vitu hivi viovu kupitia mwanamke aliyefinikwa vizuri?                           

Je! Sio wewe na uongozi wako ambao mumetengeneza njia ya unywaji mamilioni ya pombe katika nchi zetu?

Je! Sio wewe ambaye umebadilisha amri za Mwenyezi Mungu kwa zile sheria za wanadamu na kuwa mtendaji wa Demokrasia?

Ewe Bwana Erdogan! Huwezi kufanya maandalizi kwa ajili ya Akhera kwa kueneza liwati kwa kutetea haki zao kupitia Mkataba wa Istanbul.

Hakuna njia ya kujiandaa kwa Akhera kwa kuwa wewe ni mtekelezaji wa demokrasia ambayo imegeuza ulimwengu wetu kuwa wenye dhambi kwa kutunga sheria ya kila lililo haramishwa na Mwenyezi Mungu (swt).

Walakini, ungelikuwa umefanya maandalizi ya kisawasawa Akhira (Akhera ikiwa tu utaasisi maisha ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) anaridhika nayo!

Ungekuwa umefanya maandalizi ya kisawa sawa kwa ajili ya Akhira (Akhera) ambayo Mwenyezi Mungu anayakubali ikiwa utamaliza utawala wa Urasilimali na kuasisi utawala wa Uislamu kote ulimwenguni endapo tu utakataa chochote kisichokuwa cha Uislamu kama demokrasia, uhuru, ubaguzi nk...

Njia hii ndiyo inayopendelea maisha yako hapa duniani na Akhera…

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah İmamoğlu

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.