Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Magharibi iliyo sheheni Ulafi Yaitupia Macho Maovu Bangladesh yenye Utajiri wa Petroli

(Imetafsiriwa)

Habari:

Bangladesh yakabiliwa na miaka mingine mitatu ya kukatwa kwa umeme huku taifa hilo linaloendelea likitatizika kupata mahitaji ya muda mrefu ya gesi asilia na bei yake iko nje ya soko la hapo kwa hapo. Nchi hii ya Asia Kusini iliacha kununua shehena za gesi asilia iliyoyeyushwa za hapo kwa hapo mwezi Juni kwa sababu ya bei tete, na inafikiria kutafuta mahitaji zaidi ya muda mrefu, Nasrul Hamid, waziri wa umeme, nishati na rasilimali za madini, alisema katika mahojiano…. Wizara ya Fedha ya Bangladesh iliidhinisha mpango wa kutoa taka bilioni 20 (dolari milioni 211) kwa shirika linaoendeshwa na serikali la Petrobangla ili kuagiza LNG, Financial Express iliripoti Alhamisi. (Bloomberg.com, August 1, 2022).

Maoni:

Kutokana na uhaba wa kawi, haswa gesi, kuendesha mitambo ya uzalishaji umeme, watu wa Bangladesh wamekuwa wakikabiliwa na umwagaji mkubwa wa shehena. Sekta zote zikiwemo familia, kilimo na viwanda zimekuwa zikiteseka sambamba kutokana na mgogoro huu wa ‘kutengenezwa’. Kwa jina la kuhitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati, serikali ya Hasina tayari imeamua kuingia katika Mkataba wa Kimataifa wa Nishati (IECT) ili kusalimisha ubwana wetu wa nishati. Lakini ukweli ni kwamba, Bangladesh ni moja ya eneo lenye utajiri wa gesi duniani kwa sababu ya eneo lake la kijiografia na sifa za kijiolojia. Hadi sasa, ni theluthi moja tu ya eneo lake la ufuoni ambalo limegunduliwa na futi za ujazo trilioni 28 (Tcf) za hifadhi ya gesi iliyothibitishwa. Sehemu iliyosalia ya theluthi mbili ya nchi kavu na eneo lote la pwani bado haijagunduliwa. Takriban Tcf 18 za gesi zimetolewa na kutumiwa kufikia sasa, na kuacha hifadhi ya gesi iliyothibitishwa ya Tcf 10 (The Daily Star, Mei 21, 2021). Kando na hilo, utafiti wa pamoja wa miaka miwili wa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS) na Petrobangla ulionyesha kuwa Bangladesh una gesi asilia ambayo haijagunduliwa takriban Tcf 32. Katika utafiti wa baadaye, kwa ushirikiano na Kitengo cha Hydrocarbon cha GoB (HCU) chini ya wizara ya nishati na kawi, Kurugenzi ya Petroli ya Norway (NDP) ilionyesha kuwa Bangladesh ina Tcf 42 za gesi ambayo haijagunduliwa (The Financial Express, Julai 21, 2022).

Lakini cha kushangaza, bila kuvinjari na kuchimba visima vipya vya gesi, serikali inatumia fedha kutoka kwa mfuko wa kuvinjari gesi kwa ajili ya kuagiza LNG kutoka soko la kimataifa, ambapo ni ghali mara 24 kuliko gesi inayozalishwa nchini (Tk. 20 bilioni zilizo kusudiwa kwa ajili ya kuvinjari gesi lakini Petrobangla ilizitumia kwa ajili ya uagizaji, The Daily Star, Agosti 3, 2022). Kulingana na kiwango cha sasa cha bei ya eneo la Henry Hub (USD 8.32 kwa kila futi za ujazo elfu moja za gesi asilia), Tcf 52 za ​​gesi asilia zenye thamani ya karibu dolari bilioni 430 (linganisha hili na mkopo wa dolari bilioni 4.5 ambao umetafutwa kutoka IMF!). Mataifa malafi ya Kimagharibi yalimshawishi Hasina kumbakisha madarakani kwa badali ya kukabidhi hifadhi hii kubwa ya gesi. Na anafungua njia kwa ajili ya uporaji huu mkubwa sana kwa kuwafanya watu wanyimwe rasilimali zao wenyewe. Watu wa Bangladesh hawana budi ila kuunga mkono ulinganizi wa Khilafah ili waondoke katika hali yao mbaya. Ni Dola ya Khilafah (Rashida) kwa njia ya Utume pekee ndiyo inayoweza kuikomboa Bangladesh kutokana na ushawishi wa dola za kikoloni ya Kikafiri na kutumia rasilimali zake kubwa kuifanya kuwa dola yenye nguvu ili kubeba Da'wah ya Uislamu hadi kote ulimwenguni. Mwenyezi Mungu (swt) anatuamrisha,

[وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنْسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِنْ كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ]

“Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.” [Al-Qasas: 77].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Risat Ahmed
Mwanachama wa Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.