Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Bajeti ya kila Mwaka ya Serikali: Utumwa wa Kudumu wa Kikoloni

(Imetafsiriwa)

Habari:

Dola za kiliberali za kirasilimali zimeundwa kupitia mpango wa kifedha wa kila mwaka wa uendeshaji wa mapato na matumizi ya serikali. Sera hii ya kifedha ambayo inashirikisha nchi za ulimwengu wa tatu katika shinikizo kubwa la kuweka usawa kati ya usimamizi wa serikali wa mambo ya watu na utawala wa kikoloni. Sera ya fedha ya kimataifa (mfumo wa fedha zisizo na thamani ya dhati (fiat)) ambazo thamani zake zimeegemezwa kwa dolari kwa Petroli lazima zisawazishe biashara (mahuruji na maduhuli) ili kuelea thamani ya sarafu ya ndani kutokana na kuzama kwenye dimbwi la mporomoko wa kiuchumi.

Maoni:

Kenya haina kinga kutokana na mpango huu muovu wa kikoloni tunaposhuhudia tena mswada wa fedha uliopendekezwa 2025/2026 umepiga rekodi ya juu zaidi katika historia ya taifa hili maskini hadi kufikia shilingi trilioni 4.2 (dolari bilioni 32 za Marekani). Mswada huu unakusudia kukusanya zaidi ya 80% kupitia ushuru wa raia na mengine kupitia kukopa kwa msingi wa mfumo wa riba. Sehemu ya kusikitisha zaidi ya muswada huu ni kwamba zaidi ya 70% ya mapato yametengwa kwa ajili ya malipo ya deni la taifa na theluthi moja kwa ajili ya bili ya mishahara na programu ya maendeleo. Kadiri muda unavyopita, nchi za ulimwengu wa tatu zinazama zaidi katika bahari ya deni la kitaifa. Moja ya athari kubwa za mfumo wa kinyama - muovu ni ufisadi unakuwa ni jambo la kawaida la siku na kuwaacha wananchi wa kawaida wakiteseka katika umaskini.

Sauti za wasiwasi ingawa za chini kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Kiafrika kuhusu mfumo wa kifedha wa kimataifa zinaonyesha hatari na hali mbaya ambayo nchi zimo ndani yake, bila njia nyingine wazi ya kujikomboa kutoka kwa utumwa mamboleo. Uhalisia wa kimsingi hapa ni kwamba, ulimwengu unageuka kila upande kutafuta ukombozi na hili halitakuja iwe BRICS au muundo wowote utakaoundwa kwa msingi wa mfumo huo wa kikoloni. Uislamu ndio fikra pekee ambayo kiuhalisia ilikomboa mataifa kutoka katika utumwa wa serikali hadi kuwa watumwa wa Muumba wa mwanadamu, maisha na ulimwengu, na kuwaongoza wanadamu kutoka kwenye giza la ukafiri hadi kwenye nuru ya tawhid.

Takriban miaka 1,380 iliyopita Rustom, jenerali wa Kifursi akiwa amesimama mbele ya vita kuu vya Al-Qadisiyah, alikabiliwa na jeshi la watu ambao nyoyo zao pekee zingeweza kuhamisha milima. Alimwomba swahaba mtukufu Rabi' b. ´Amir (ra) ili kumjulisha lengo la wale anaowawakilisha (yaani Waislamu). Jibu la Ibn ´Amir lilitoa ufahamu juu ya shajaa ya maswahaba wa Mtume wa Mwisho (saw): إن الله ابتعثنا لنخرج العباد من عبادة العباد إلى عبادة رب العباد، ومن ضيق الدنيا إلى سعة الآخرة، ومن جور الأديان إلى عدل الإسلام  “Mwenyezi Mungu Ametutuma ili tuwatoe waja kutoka kuwaabudu waja hadi kumuamudu Mola wa waja; kutoka kwenye dhiki ya dunia hadi kwenye starehe za ākhirah, na kutoka katika dhulma za dini na mifumo [zilizotungwa na wanadamu au zilizobadilishwa] hadi uadilifu wa Uislamu...”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.