- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Historia Inawalingania Wanajeshi wa Pakistan – Wakati Umewadia wa Uongozi wa Kweli wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Shambulizi la Pahalgam mnamo Aprili 2025, ambapo washambuliaji wenye silaha waliua raia 26 na kujeruhi wengine kadhaa, kwa mara nyingine tena limeitupa Kashmir katikati ya hali ngumu ya kisiasa na kiitikadi. Ingawa mamlaka mara moja zilielekeza kidole cha lawama kwa makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Pakistan kuwa yanahusika, tukio hilo liliingizwa siasa haraka na kuingizwa katika masimulizi mapana ambayo yameunda utawala wa Narendra Modi kwa zaidi ya muongo mmoja: mapambano kati ya dola ya kitaifa ya Kibaniani na wanaodaiwa kuwa maadui zake—wa ndani pamoja na nje.
Maoni:
Makabiliano ya hivi punde ya kijeshi kati ya Pakistan na India kwenye Mstari wa Udhibiti (LoC) huko Kashmir pia yameangazia mizani ya siasa za kieneo inayozidi kuwa dhaifu. Mashambulizi ya India yaliyofeli na mashambulizi ya kisasa ya kijibu ya Pakistan yalifichua udhaifu katika uwezo wa kijeshi wa India, na kusababisha India kutafuta usitishaji mapigano. Hii haiashirii tu ushindi wa mbinu kwa Pakistan lakini pia fursa ya kimkakati inayowezekana. Kwa miongo kadhaa, Pakistan imewekeza katika teknolojia ya kisasa ya kijeshi na kuendeleza uwezo wake kwa msaada wa, miongoni mwa wengine, China.
Kinyume chake, India imeegemea teknolojia ya zamani, ingawa hivi karibuni imepokea maboresho kutoka kwa washirika wa Magharibi kama vile Ufaransa, 'Israel' na Marekani. Shambulizi hilo linaingia moja kwa moja kwenye simulizi ambayo Chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP) kimekuza katika miaka yake ya uongozi. Kwa serikali ya Modi, wahalifu hawakuwa magaidi tu bali nembo za adui mkubwa—yaani Uislamu na Waislamu. Bila kungoja uchunguzi kamili, mamlaka za India zililaumu vikundi vilivyoko Pakistan, vinavyoitwa Lashkar-e-Taiba na shirika linalodaiwa kuwa mbele yake, The Resistance Front (TRF). Ingawa TRF ilikanusha kuhusika na ushahidi wa kuaminika kukosekana, simulizi tayari ilikuwa imeimarishwa. BJP, ambayo ni mahiri kwa muda mrefu katika kugeuza migogoro ya kitaifa kuwa mizozo mikuu ya kisiasa, iliunganisha mauaji ya Pahalgam katika maono yake ya kisiasa ya Hindu Rashtra.
Uzinduzi wa Hekalu la Ram huko Ayodhya ulikuwa kilele cha miongo kadhaa ya siasa za kimadhehebu. Ilikuwa pia ishara wazi: katika India ya Modi, Ubaniani umeidhinishwa na serikali, huku dini zengine zinatazamwa kwa tashwishi. Tangu kufutwa kwa Kifungu cha 370 mnamo 2019, Kashmir imepokonywa uhuru wake na kuwekewa udhibiti mkubwa wa kiutawala na kijeshi na serikali ya India.
Lile ambalo hapo awali lilikuwa eneo linalotawaliwa na haki na huruma ya Kiislamu sasa kimekuwa eneo la kijeshi, linalotawaliwa kutoka New Delhi na kuundwa na matamanio ya utaifa. Miradi ya miundombinu kama vile daraja jipya la reli inayounganisha Kashmir na India Bara inawasilishwa kama ishara za maendeleo. Lakini kwa kweli, maendeleo haya yanawakilisha ukaliaji wa kimabavu-sio uwiano. Kukamatwa kiholela, kuzimwa kwa mtandao wa intaneti, kunyakua ardhi kwa lazima, na ukandamizaji wa kisheria vimekuwa zana za kawaida za utawala katika eneo hilo. Usalama unafuatiliwa kwa gharama ya uaminifu, na kila tukio jipya linakuwa uhalali wa ukandamizaji zaidi na ishara ya kutofaa kwake. Hii inaakisi kwa karibu mbinu zinazotumiwa na jeshi la Wazayuni kwa miongo kadhaa dhidi ya Wapalestina.
Madhara ya shambulizi hilo pia yanafikia zaidi ya Kashmir. Takriban mara moja, serikali ya Modi ilichukua hatua ya kusimamisha sehemu ya kati ya Mkataba wa Maji wa Indus – kitovu cha diplomasia ya India na Pakistan tangu 1960. Tishio la kuzuia mtiririko wa maji kwenda Pakistan ni la kiishara na la kimkakati. Haiashirii tu kulipiza kisasi bali pia nia ya kutumia rasilimali shirika kama silaha katika michezo ya kisiasa.
Watawala wa Pakistan wanaendelea kuiona Marekani kama mshirika asiye na budi, lakini uhalisia umeonyesha kuwa Marekani inazidi kuweka kamari kwa India kama mshirika wake mkuu wa kimkakati barani Asia. Hii sio tu kwa sababu ya mazingatio ya kiuchumi na kijeshi lakini pia dori ya India katika mkakati wa Amerika kuidhibiti China. Pakistan inaonekana imenaswa kati ya maslahi ya dola kuu duniani—kutafuta uungwaji mkono wa Marekani kwa upande mmoja, na kuongezeka kwa ushirikiano wa China kupitia CPEC na uhusiano wa kijeshi kwa upande mwingine. Pakistan inasimama kwenye njia panda ya kihistoria: kuendelea kama kibaraka katika mikakati ya dola kuu – au kukamata udhibiti wa hatima yake na kuuinua Umma wa Kiislamu. Ukombozi wa Kashmir na kujitenga kutokana na utegemezi kwa Marekani ni muhimu kwa mabadiliko haya ya kimkakati na kimfumo.
Msukosuko wa sasa wa kimataifa si tishio tu—bali ni fursa nzuri kwa uongozi wa Kiislamu na mabadiliko. Pakistan haipaswi kutafuta hali halisi au kusitisha mapigano, lakini badala yake ichukue hatua ya kihistoria kwa kukomboa Kashmir yote, kupata udhibiti wa rasilimali zake muhimu, na hivyo kuchukua uongozi katika mabadiliko ya mfumo wa ulimwengu. Hii inafungua njia kwa enzi mpya ambayo Pakistan inacheza dori kuu katika kusimamisha Khilafah Rashida. Haya ndio ruwaza ya kina kimfumo ambayo inahitaji si tu nguvu za kijeshi na uongozi wa kisiasa bali utashi wa kisiasa wa kupambana na mfumo wa dunia uliopo.
Wakati umefika sasa kwa Pakistan kukomesha maono ya Modi ya Hindu Rashtra kwa kuungana na nchi za Asia ya Kati, kuikomboa Kashmir yote, na kusimamisha Khilafah Rashida juu ya magofu ya Hekalu la Ram na maono ya Hindu Rashtra.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohib Abdullah