- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ubepari kama Chanzo Kikuu cha Maafa ya Mafuriko huko Sumatra
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kimbunga Senyar kilikuwa kichocheo tu; kiwango cha uharibifu nchini Indonesia kinaonyesha miongo kadhaa ya usimamizi mbaya wa ikolojia. Sumatra imepoteza mamilioni ya hekta za misitu, ikidhoofisha maeneo ya maji huko Aceh, Sumatra Kaskazini, na Sumatra Magharibi. Maeneo ya tambarare yalikaushwa maji kwa ajili ya mashamba makubwa, na kusababisha kupungua kwa ardhi na kugeuza vizuizi vya maji asilia kuwa mabonde ya mafuriko. Makaazi ya haraka katika maeneo tambarare ya mafuriko, pamoja na usimamizi dhaifu wa matumizi ya ardhi, yaliongeza athari. Mvua kali ilipofika, mandhari haikuwa na uwezo uliobaki wa kuhimili. Maafa yanaonyesha kwamba muundo wa maendeleo wa Indonesia—unaoendeshwa na uchimbaji na usimamizi duni wa mazingira—umefanya hali mbaya ya hewa kuwa hatari zaidi kuliko inavyopaswa kuwa. (news.mongabay)
Maoni:
Mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya mamia ya watu huko Aceh, Sumatra Kaskazini, na Sumatra Magharibi hayakuwa majanga ya kimaumbile tu, bali yalikuwa ushahidi dhahiri wa kufeli kimfumo—kushindwa kwa mfumo mlafi wa kibepari na demokrasia isiyo na nguvu kulinda nafasi ya kuishi ya raia wake.
Ubepari unakuuza mantiki ya “ukuaji usio na mwisho,” ambayo hatimaye huhalalisha unyakuzi wa misitu, upanuzi wa mafuta ya nazi, shughuli za uchimbaji madini, na miradi ya nishati katikati ya mfumo wa ikolojia wa Bukit Barisan huko Sumatra. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, hekta milioni 1.4 za misitu zimepotea katika mikoa hii mitatu. Ukataji huu mkubwa wa misitu si ajali; ni matokeo ya moja kwa moja ya sera za serikali zinazotii maslahi ya soko na wawekezaji. Misitu inapokatwa, mito inakuwa hafifu, na milima inaondolewa hifadhi, je, bado tunaweza kuyaita mafuriko haya majanga ya kimaumbile?
Wakati huo huo, demokrasia—inayodhaniwa kuwa utaratibu wa usimamizi wa umma—imefeli kuzuia ongezeko la makubaliano, vibali vya utumizi mbaya, na sera zinazopuuza uwezo wa kubeba mazingira. Ushiriki wa umma unakuwa utaratibu rasmi tu, huku maamuzi ya kimkakati yakifanywa katika maeneo yaliyo mbali na sauti ya watu na mara nyingi yakiwa mazuri zaidi kwa wamiliki wa mitaji. Kivitendo, demokrasia huzalisha dola iliyo changamfu katika kujenga na kuharibu maumbile, ilhali haijali usalama wa binadamu.
Pindi majanga yanapotokea, dola hujibu kana kwamba matukio haya hayawezi kuepukika. Kiuhalisia, chanzo kikuu kiko katika machaguo ya kisiasa na kiuchumi ya muda mrefu yanayofanywa kwa kutabanni mfumo wa kibepari wa kisekula.
Janga hili huko Sumatra linatoa funzo muhimu kwa Waislamu: majanga hayatokani na mambo ya kimaumbile pekee, bali kutoka kwa mfumo wa kisiasa na mfumo uliochaguliwa na taifa. Pindi nchi inapokumbatia mfumo wa kisiasa wa kisekula wa kibepari, inakuwa mtumishi wa wamiliki wa rasilimali. Matokeo yake, migogoro mbalimbali huibuka—umaskini, muozo wa kijamii, na majanga ya kimazingira yanayotokana na unyonyaji wa kupita kiasi.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar