Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 17 Rabi' II 1447 | Na: H 1447 / 015 |
M. Alhamisi, 09 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Chukueni Hatua na Msiache Masuala Yenu Yawe Mikononi mwa Maadui Zenu
(Imetafsiriwa)
Mazungumzo ya awamu ya kwanza ya mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kusimamisha vita dhidi ya Gaza yalianza mjini Sharm El-Sheikh nchini Misri, kwa kuhudhuriwa na wajumbe wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner, Waziri Mkuu wa Qatar, na wakuu wa kijasusi wa Uturuki na Misri.
Ilikuwa wazi kutokana na mpango huo kwamba ulilenga kufikia maslahi binafsi kwa Rais wa Marekani, kuwasilisha mafanikio yake katika kusimamisha vita dhidi ya Gaza kama sehemu ya faili lake la kupata Tuzo ya Amani ya Nobel, na kufikia maslahi ya kisiasa na kiuchumi kwa Marekani; kwani inauweka utawala wa Ukanda huo mikononi mwa kamati ya kimataifa inayoongozwa naye, na nyuma yake Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, ikijulikana kwamba Marekani na Uingereza ni maadui wawili wakubwa wa Uislamu na Waislamu, na walinzi wa umbile la Kiyahudi! Ilikuwa wazi pia kutokana na mpango wa Trump kwamba ulizingatia maslahi ya umbile la Kiyahudi, kulipa nguvu juu ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na kuzuia hatari yoyote ambayo inalitishia.
Kabla ya Trump kuwasilisha mpango wake huo, aliongoza mkutano uliojumuisha Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia na Pakistan, kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mnamo Jumanne, 23/9/2025, akiusifu kuwa “mkutano muhimu zaidi.” Kisha akawasilisha, au akaweka, juu yao mpango wenye nukta 21, mashuhuri zaidi kati yazo ni: kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa Kiyahudi waliokuwa wakishikiliwa na Hamas, usitishaji wa kudumu wa mapigano, na kuondolewa hatua kwa hatua kwa jeshi la Kiyahudi. Trump aliweka bayana lengo lake la kuwakusanya, ambalo lilikuwa ni kuwaachilia huru wafungwa wa Kiyahudi, alipokuwa akiwahutubia akisema: “kwamba utawala wake unataka kuregesha mateka 20 na miili 38 kutoka Gaza...” Kisha akaweka bayana uondokaji wa hatua kwa hatua, ambao ni neno lililosheheni kumaliza uondokaji huo wa hatua kwa hatua, na kisha umbile la Kiyahudi kubakia kudhibiti kudumu kwa usitishaji vita huo!
Kwa hivyo, haishangazi kusikia ukaribishaji wa watawala Ruwaybidhat (wajinga wasio na maana) wa Waislamu wa mpango wa Trump, na haishangazi kuona kila mmoja wao akingojea zamu yake ya khiyana katika mpango huu; baadhi yao walianza zamu yao katika mazungumzo ya awamu ya kwanza, kwani tuliona Waziri Mkuu wa Qatar akishiriki ndani yake, pamoja na wakuu wa ujasusi wa Uturuki na Misri, na wengine wanasubiri zamu yao. Hakika hayo wanayo yafanya ni maovu kabisa!
Enyi Waislamu: Watawala wenu waoga wamekuuzeni kwa bei rahisi na wamekabidhi masuala yenu kwa maadui zenu, ili kuhifadhi viti vyao vibovu vya utawala vinavyokaribia kuanguka. Kunyamaza kwenu juu yao kunawafanya waendelee na upotofu wao na khiyana zao. Hawaoni haya mbele ya Mwenyezi Mungu, wala Mtume wake, wala nyinyi. Wamekula njama dhidi ya Palestina, wakawapa nguvu Mayahudi juu yake, wakakaa kimya juu ya mauaji ya makumi ya maelfu na uharibifu wa nyumba juu ya vichwa vya wakaazi wake huko Gaza, wakatazama kuhamishwa kwa watu wake kutoka kwa makaazi yao, na wakati wote huo walikuwa wakitoa wito wa amani na suluhisho la dola mbili, mradi wa Amerika ambao unafanikisha maslahi ya umbile la Kiyahudi.
Wakati umefika wa kukomesha khiyana za watawala hawa ruwaybidhat, kuwatupilia mbali kama konde za tende, na kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili hadhi yenu na heshima yenu irudi kwenu, na mushikile hatamu za uongozi, muwe nguvu changamfu yenye ushawishi katika kuunga mkono masuala yenu, na kutowaruhusu maadui zenu kusimamia mambo yenu.
[إِن يَنصُرْكُمُ اللّهُ فَلاَ غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللّهِ فَلْيَتَوَكِّلِ الْمُؤْمِنُونَ]
“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aal-i-Imran:160]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |