Majibu ya Aibu ya Tawala katika Nchi za Waislamu kwa Uvamizi wa Umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Yeyote anayetazama miitikio ya tawala zilizopo katika ardhi za Waislamu kwa mashambulizi ya umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran atahisi huzuni kubwa na masikitiko kwa hali ya sasa ya Waislamu. Wengine wamelaani na kushutumu pekee; wengine wameonyesha hofu ya machafuko katika eneo hilo kutokana na mashambulizi haya. Baadhi walieleza kuwa ni ongezeko la hatari; wengine walielezea wasiwasi wao juu ya athari zake kwa kadhia ya Palestina. Wengine hata walitangaza kuwa tayari kufanya upatanishi kati ya Iran na umbile la Kiyahudi. Walio bora zaidi walionyesha nia ya kuiunga mkono Iran katika majukwaa ya kimataifa, huku baadhi ya nchi hizo hizo zikifungua anga zao kwa ndege za umbile la Kiyahudi kuruka juu, kuipiga Iran kwa mabomu, kuua na kuharibu, na kisha kuregea bila hata risasi moja kufyatuliwa kwao! Wengine walinasa makombora na droni za Iran zilizolenga kushambulia umbile la Kiyahudi, na hivyo kuwaepusha na kupigwa!