Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  23 Rabi' II 1447 Na: H 1447 / 018
M.  Jumatano, 15 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wanawake wa Kashmiri Walibakwa na Kuteswa na Uvamizi wa Dola ya India Tangu 1947

(Imetafsiriwa)

Wakati wa Kikao cha 60 cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) mwaka huu, Kikao cha Kimataifa kisicho cha Kiserikali kilifanyika kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni za Wanawake, kilichoandaliwa na OCAPROCE International chini ya kichwa, “Wanawake kwa ajili ya Kukuuza na Kulinda Turathi ya Kitamaduni na Ujenzi wa Amani Endelevu ifikapo 2030,” ambapo mwakilishi wa wanawake wa Kashmir Dkt. Shugufta, aliangazia masaibu ya wanawake wa Kashmir mikononi mwa gaidi amvamizi, vikosi vya jeshi la India. Alisema, “Ninasimama mbele yenu leo ​​kwa sauti inayobeba maumivu ya wanawake wengi walionyamazishwa kutoka bonde la Jammu na Kashmir Inayokaliwa Kimabavu Kinyume cha Sheria. Vilio vyao vimezidiwa na milio ya risasi, heshima yao iliyoharibiwa na uvamizi ambao unatumia sio tu risasi, bali pia miili ya wanawake, kama silaha za vita.” Alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kukomesha unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake wa Kashmir, na kuwawajibisha wahusika.

Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yametembelea Kashmir kunakili kesi za unyanyasaji na ubakaji dhidi ya raia na kile ambacho wameripoti kinashangaza katika hali yake ya kutisha. Wanajeshi wa India, Jeshi Kuu la Polisi wa Akiba, na Vikosi vya Usalama vya Mipakani wote wanahusika katika unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake wa Kiislamu huko Kashmir ambao unakusudiwa kuwadhalilisha na kuwaadhibu na vile vile njia ya kuwalazimisha wanaume wa Kiislamu wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo kujisalimisha. Wanawake pia wanakabiliwa na mauwaji kinyume na sheria, wakifanywa vipofu kimakusudi, na nyumba zao, biashara, na vijiji vizima vikichomwa chini ya kisingizio cha kukomesha ugaidi. Kwa kuongezea, mashini ya propaganda ya India inawaonyesha wanawake wa Kiislamu wa Kashmiri kama vyombo vya haki, vyenye urembo vinavyosubiri wanaume wa Kibaniani kuwaowa na kuwafanya wahindi. Vitendo hivi vyote ni mipango iliyofikiriwa kwa uangalifu na serikali ya India kama njia ya kupanua zaidi ajenda ya wakoloni walowezi ya Dola ya Hindutva huko Kashmir kwa kuwatenga na kuwatia hofu Waislamu wanati.

Kashmir ni ardhi nyengine ya Uislamu inayokaliwa kwa mabavu ambayo wakati fulani ilitawaliwa na Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt) na ilisifiwa kama, “Jannah (Pepo) ya Duniani.” Hata hivyo, tangu Waingereza waingie India kwa mara ya kwanza mwaka wa 1608 kwa utawala wao wa moja kwa moja juu ya bara hilo dogo karibu miaka 150 baadaye, ikawa ardhi ya njaa, umaskini, ukosefu wa usalama, na migawanyiko. Utawala huu mbovu wa kikoloni ulibadilishwa na serikali iliyoratibiwa na nchi za Magharibi chini ya kivuli cha Uhuru mwaka 1947, na kukaliwa kwa mabavu na dola ya Hindutva, kama vile Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inavyokaliwa kwa mabavu na umbile la Kiyahudi, na imekuwa isiyovumilika kwa Waislamu.

Walakini, mnamo 2025, baada ya kushuhudia matamshi yasiyokuwa na vitendo ya taasisi za kimataifa kuhusu mauaji ya halaiki yanayotokea Gaza mikononi mwa Mayahudi, wengi wanaendelea kutazama taasisi zile zile, kama vile UN, ambazo ziliundwa ili kuhakikisha utawala wa Amerika na ambazo ndio hasa zilizoruhusu ukaliaji wa kimabavu kuchukua na kudumisha umiliki wa ardhi zetu kutatua tatizo la ghasia huko Kashmir.

Baada ya miongo kadhaa ya dunia kuwatazama wanawake wa Kashmiri wakidhalilishwa, kutengwa, na kulazimishwa, kwa hakika, tunaweza kuona kwamba taasisi hizi za kimataifa pamoja na serikali za Magharibi hazitakomesha uvunjifu wa heshima kwa dada zetu. Bali, ni kupitia tu kusimamishwa kwa dola ambayo inatawala kwa Uislamu peke yake na hivyo inaelewa umuhimu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu (swt) anautoa wa kulinda heshima na ustawi wa mwanamke wa Kiislamu, ndipo unyanyasaji dhidi ya dada zetu huko Kashmir, Palestina, Turkestan Mashariki na kwengineko utakwisha. Dola hii ni Khilafah kwa njia juu ya Utume ambayo itakusanya jeshi lake kutetea heshima ya dada zetu, bila kujali wanaishi ardhi gani, kama vile Jenerali mtukufu wa Kiislamu, Muhammad ibn Qasim, alitumwa na jeshi imara na Khalifah al-Walid bin Abdul Malik chini ya utawala wa Bani Ummayya ili kuwaokoa baadhi ya wanawake waliokamatwa na kufungwa na Mfalme dhalimu wa Kibaniani wa India, Raja Dahir, ingawa mji mkuu wa Khilafah ulikuwa Damascus wakati huo. Sisi vivyo hivyo tunahitaji kuelekeza juhudi zetu kamili na umakini kwenye usimamishaji wa haraka wa Khilafah. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[[اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ

“Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka.” [Al-A’raf: 3]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.