Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 28 Jumada I 1447 | Na: H 1447 / 029 |
| M. Jumatano, 19 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ukosefu wa Masuluhisho ya Kudumu kwa Mgogoro wa Rohingya
(Imetafsiriwa)
Gazeti la ‘South China Morning Post’ liliripoti mnamo tarehe 10 Novemba kwamba Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Kusini-mashariki mwa Asia kuna hatari ya “janga jengine la kibinadamu” ikiwa uvukaji wa bahari wa wakimbizi waliokata tamaa utaendelea bila kudhibitiwa. Vifo vya watu wasiopungua 21, wakiwemo watoto kadhaa, katika ajali ya boti karibu na pwani ya Malaysia vimeibua hofu ya kuongezeka tena kwa uvukaji hatari wa bahari wa wakimbizi wanaokimbia mzozo nchini Myanmar na hali mbaya katika nchi jirani ya Bangladesh. Kulikuwa na miili 12 iliyopatikana nchini Malaysia na tisa katika nchi jirani ya Thailand – kulingana na mkuu wa eneo wa shirika la bahari la Malaysia, Romli Mustafa.
Makundi ya haki za binadamu na mashirika ya kimataifa yanaonya kwamba janga hilo ni ishara ya kile kinachoweza kuwa mbele katika miezi ijayo, huku njia tulivu za bahari na zinazoweza kusafirika zaidi zikikaribia (baada ya Mvua ya Monsoon, kila mwaka kipindi cha Oktoba hadi Disemba) kutoka Rakhine na Cox's Bazar ya Bangladesh, ambapo mamia ya maelfu ya Warohingya hukusanyika katika moja ya kambi kubwa zaidi za wakimbizi duniani.
Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, linakadiria kwamba takriban Warohingya 7,800 walijaribu kuvuka baharini kutoka Myanmar na Bangladesh mwaka wa 2024, huku zaidi ya 650 wakiripotiwa kufariki au kutoweka – idadi kubwa zaidi tangu 2015. “Uhaba wa chakula, vikwazo vya usafiri, na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama kumefanya maisha kuwa magumu. Wengi wanaona bahari kama njia yao ya mwisho ya kutorokea,” Mtandao wa Utetezi wa Haki za Warohingya uliambia ‘This Week’ huko Asia, na kuongeza kuwa walanguzi sasa wanatoza hadi dolari 3,000 za Marekani kwa kila mtu kwa ajili ya kupita hadi Malaysia au Indonesia.
Migogoro hii inayoingiliana – mateso nchini Myanmar, kukata tamaa katika kambi na ukosefu wa masuluhisho ya kudumu kutoka nchi za ASEAN kama utaratibu wa kikanda – inawalazimisha watu kuchukua tena safari hatari za baharini na wengi kamwe hawafiki wanakokwenda.
Kwa karibu miongo miwili, utaratibu wa sasa hauna suluhisho endelevu kwa mgogoro wa Rakhine, badala yake unaruhusu mateso ya Warohingya kudhibitiwa na mvua za monsoon zinazojirudia. Suluhisho hili lisilo endelevu linatokea kwa sababu mamlaka (ikiwemo nchi za Waislamu za ASEAN, ASEAN, na UN) hutoa masuluhisho yasiyo na nia moja tu, zikitaja ukosefu wa uwajibikaji, kama vile mipaka ya mamlaka yao, usalama wa kitaifa, au maslahi yao ya kiuchumi. Zinachagua kubaki katika eneo salama la mfumo wa zamani, yaani ubepari wa kisekula ambao unajumuisha dhana potofu ya utaifa.
Zaidi ya hayo, watawala hawa wanapuuza masuluhisho badali endelevu, kwa sababu hakuna hata mmoja wa watawala hawa aliye tayari kutabanni muundo wa Uislamu, kwa sababu wamepoteza dhamira, malengo na matarajio yao ya Kiislamu kama Umma bora kulingana na mwongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwa kweli, ni wazi kabisa kwamba Uislamu una suluhisho bora na endelevu, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu Ta'ala:
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ] “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal: 72].
Uislamu unawaamuru watawala wa Waislamu wa Indonesia, Malaysia na Bangladesh kuchukua hatua za dharura mara moja kwa wakimbizi wa Rohingya. Hatua hizi ni pamoja na:
(1) kufungua mipaka ya nchi kwa wakimbizi wa Rohingya,
(2) kutuma misheni za uokoaji kwa wale ambao bado wanaelea baharini,
(3) kulinda na kushughulikia mahitaji yao yote,
(4) kutoa shinikizo la kisiasa kwa utawala dhalimu wa Myanmar ili kukomesha dhulma na ukatili wao wote dhidi ya Waislamu wa Rohingya na
(5) hatua ya mwisho ni ikiwa shinikizo la kisiasa litapuuzwa, basi uhamasishaji wa vikosi vya jeshi lazima ufanyike ili kudumisha heshima ya Uislamu na Waislamu!
Hata hivyo, hatua hizi zote zinaweza kuwa na ufanisi ikiwa watawala wa Waislamu watatoka katika eneo lao la starehe, yaani, kuondoka kutoka kwa mfumo wa kibepari wa kisekula kuelekea mfumo wa Kiislamu ambao umeonekana kwa muda mrefu kama tishio kwa mfumo uliozeeka. Mfumo huu utaongozwa na serikali ya Khilafah ambayo itatumia ala na njia zake zote, kuhamasisha juhudi zake zote, kisiasa, kiuchumi, na kijeshi, kuwalinda Waislamu kutokana na ukandamizaji, na kutetea damu na heshima yao; bila kujali mahali walipo na gharama yoyote. Hii ni kwa sababu Khilafah ni dola yenye kanuni, inayoegemea juu ya maadili mema ya Uislamu ambayo huweka heshima ya maisha ya mwanadamu mahali pa juu, ambayo inalazimika kulinda damu ya Waislamu, badala ya kutenda tu kwa kutegemea maslahi ya kitaifa au faida ya kiuchumi, kama Mtume (saw) alivyosema.
إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»» “Hakika, imam (kiongozi) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na kujihami kwaye” (Muslim)
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |