Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 17 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 033 |
| M. Jumatatu, 08 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vita vya Amerika dhidi ya Uislamu
(Imetafsiriwa)
Utawala wa Marekani na watoaji maamuzi ndani yake hawaachi kuonyesha uadui wao dhidi ya Uislamu na kufichua vita vyao vinavyoendelea na anuwai dhidi yake. Katika kila tukio na bila ya tukio, utamsikia afisa wa Marekani akipaza sauti yake kuushambulia Uislamu, akiuelezea kwa maelezo yanayofichua ukubwa wa chuki yao dhidi yake na kuashiria ukubwa wa utisho unaojaza nyoyo zao kutokana na Uislamu.
Na inajulikana kwamba baada ya kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti mwanzoni mwa muongo wa mwisho wa karne iliyopita, Amerika iliuchukua Uislamu kama adui yake wa kimfumo na ikakusanya kwa ajili ya kupigana nao majeshi ya askari, vibaraka, fedha, makubaliano na mikataba, ambayo si wa mwisho ulikuwa ni Mkataba wa Abraham, wala wa kwanza ambao ulikuwa ukiuita Uislamu kuwa ni mapinduzi, itikadi kali na ugaidi.
Katika siku za hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alionekana pamoja na Sean Hannity kwenye The Onyesho la Sean Hannity kwenye Fox News akieleza, “Uislamu wenye msimamo mkali umeonyesha kwamba nia yao sio tu kuchukua sehemu moja ya dunia na kufurahishwa na Khilafah yao mdogo, wanataka kupanuka. Ni wa kimapinduzi katika maumbile yake. Unatafuta kupanua na kudhibiti maeneo zaidi na watu zaidi...” Na Rubio alipuuza kwamba kile anachoutuhumiwa kwacho Uislamu zaidi ndicho kile kile Marekani inachofanya—isipokuwa kwa tofauti kubwa: Amerika inatafuta udhibiti juu ya ulimwengu ili kupora rasilimali na utajiri wake, na kwa ajili hiyo inaua mamilioni ya wanadamu, inaunguza kilicho kibichi na kikavu, na kuacha nyuma uharibifu na kifo; na vita vya Somalia, Iraq na Afghanistan haviko mbali nasi. Ama Uislamu, uliwatoa watu kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru, kutoka kwenye taabu hadi kwenye furaha, na kutoka kwenye utumwa kwa wanadamu na sheria zao hadi kwenye utumwa kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Na kabla yake, rais wake mwenyewe alitaka kulazimisha Mkataba wa Abraham juu ya ardhi za Waislamu ili kuyeyusha Uislamu na kuufanya kuwa ni mila za kikuhani kama dini nyenginezo, na kuondoa kipengee cha kisiasa cha Uislamu kwenye akili za watu. Pia alithibitisha sera ya Marekani kuhusu Uislamu na Waislamu katika kile alichokiita Mkakati wa Usalama wa Kitaifa wa 2025, akisema: “Tunataka kuzuia nguvu ya adui kutawala Mashariki ya Kati, usambazaji wake wa mafuta na gesi, na vinyongo ambavyo kwavyo wanapitia.” Na alisema mahali pengine: “Marekani daima itakuwa na maslahi ya msingi katika kuhakikisha kwamba nishati ya Ghuba haianguki mikononi mwa adui wa moja kwa moja, kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz ubaki wazi, kwamba Bahari Nyekundu ibakie kupitika, kwamba eneo hilo lisiwe kiota au msafirishaji wa ugaidi dhidi ya maslahi ya Marekani au nchi ya Marekani, na kwamba ‘Israel’ ibaki salama. Tunaweza na ni lazima tuzungumzie tishio hili la kimfumo na kijeshi bila ya miongo ya vita tasa vya “kujenga taifa”. Pia tuna hamu ya wazi ya kupanua Makubaliano ya Abraham kwa mataifa zaidi katika eneo hili na kwa nchi zengine katika ulimwengu wa Kiislamu.”
Pia alisema: “Washirika wa Mashariki ya Kati wanaonyesha dhamira yao ya kupambana na itikadi kali, sera ya Amerika inapaswa kuendelea kushajiisha.” na akasema: “Na ni lazima tuwe na tahadhari dhidi ya vitendo vya kigaidi vinavyoibuka upya katika sehemu za Afrika…” Na unamuona katika hotuba yake yote kuhusu Uislamu na uainishaji wake wa Waislamu kwa kutumia istilahi iliyobuniwa na watangulizi wake miongoni mwa marais wa Marekani; kwani waliwagawanya Waislamu kwa watu wenye msimamo wa wastani na wenye itikadi kali, na wakawataja wao na Uislamu kuwa ni ugaidi, wakichukulia hilo kuwa ni kisingizio cha kupigana nao.
Nguvu ya kifikra katika Uislamu, ukubwa wa ardhi za Waislamu, na hofu ya kurejea Khilafah katika ardhi za Kiislamu ni chanzo cha hofu kwa ukafiri na dola zake, hususan dola zenye nguvu kubwa zinazoona katika Uislamu hatari inayotishia maslahi yao na hata kutishia kuwepo kwao. Hivyo, hawaachi kueleza wasiwasi huu mara kwa mara, licha ya kile wanachomiliki katika nguvu za kimada na licha ya kuwepo kwa watawala vibaraka watiifu kwao katika ardhi za Kiislamu.
Lakini tunawapa bishara njema kwamba wanachokihofia kitakuja bila ya kuepukika licha ya mipango yao, nguvu zao, na vibaraka wao; kwani dola ya Khilafah inaregea upesi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kuujaza ulimwengu kwa uadilifu kama walivyoujaza dhulma na utumwa. Kwani Umma wa Kiislamu ni Ummah ulio hai ambao haufi kamwe, hata kama utaghafilika kwa muda fulani; utaregea kubeba ujumbe wa Uislamu—ujumbe wa nuru, mwongozo, na uadilifu—kwa watu wote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ndani ya Umma wa Kiislamu kuna Hizb ut Tahrir, kiongozi wa kweli asiyewadanganya watu wake, inayobeba mradi wa mwamko wake sahihi kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Na kesho iko karibu sana kwa yule anayengoja.
[يُرِيدُونَ لِيُطْفِؤُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. * Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawbah: 32–33]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |