Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 8 Muharram 1448 | Na: H1448 / 004 |
| M. Jumanne, 23 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Badala yake, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume Itazika Umoja wa Kiarabu na Tawala Zote za Madhara
(Imetafsiriwa)
Rais wa Misri el-Sisi alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mfumo wa hatua za pamoja za Waarabu na kuamsha dori ya Umoja wa Kiarabu kama "mwavuli mkuu na mfumo kamili wa kutetea maslahi ya dola za Kiarabu na Waarabu." Hii ilikuja wakati wa mapokezi yake mnamo Jumapili ya Nabil Fahmy, mgombea wa wadhifa wa Katibu Mkuu wa Umoja huo, na Ahmed Aboul Gheit, Katibu Mkuu wa sasa, ambaye muhula wake unaisha mwishoni mwa mwezi huu. El-Sisi pia alithibitisha "maono ya Misri ambayo yana nia ya kuchukua dori za kujenga ambazo zinakuza masuluhisho ya amani kwa migogoro ya eneo hilo."
Hamu ya El-Sisi ya kuamsha dori ya Umoja wa Kiarabu na kuuweka hai inatokana na hamu yake ya kuubakisha Ummah kuwa dhaifu, uliogawanyika, na chini ya kafiri wa kikoloni. Umoja wa Kiarabu umeasisiwa kwa kujumuisha mgawanyiko miongoni mwa ardhi za Waislamu katika eneo la Kiarabu kwa kisingizio cha kuheshimu uhuru wa mataifa; yaani, kuheshimu kwamba kila dola ina mipaka yake, bendera, na katiba tofauti na nyengine. Jaribio lolote la kubadilisha uhalisia huu linachukuliwa kuwa ni ukiukaji wa ubwana wa dola hizi zinazodaiwa na linachukuliwa kuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Kiarabu.
Hili ni kweli kwa upande wa ufahamu wake na kile ambacho Magharibi ya kikoloni ilikusudia: kwamba inatumika kama badali ya mfumo imara wa umoja ambao Mwenyezi Mungu alikusudia kwa Waislamu, Waarabu na wasio Waarabu vile vile, yaani mfumo wa Khilafah, kwa mujibu wa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ فَاقْتُلُوا الْآخَرَ مِنْهُمَا» “Pindi ahadi ya utiifu inapotolewa kwa makhalifa wawili, muueni wa pili wao.” Na kauli yake (saw):
«مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ فَاقْتُلُوهُ» “Akikujieni mtu na hali mambo yenu yameshikana chini ya mtu mmoja, kwa kutaka kuvunja umoja wenu au kufarikisha umma wenu, muuweni.”
Na kauli yake (saw): «إِنَّهُ سَتَكُونُ هَنَاتٌ وَهَنَاتٌ، فَمَنْ أَرَادَ أَنْ يُفَرِّقَ أَمْرَ هَذِهِ الْأُمَّةِ وَهِيَ جَمِيعٌ فَاضْرِبُوهُ بِالسَّيْفِ كَائِناً مَنْ كَانَ» “Kutakuwa na misukosuko na misukosuko, mwenye kutaka kugawanya mambo ya Umma huu na hali umeshikamana basi mpige kwa upanga, yeyote yule.” Na Hadith nyingine zinazofanya kuwa ni faradhi kwa Ummah kuendelea kushikamana chini ya Khalifa mmoja, bendera moja, na katiba moja: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Wake (saw).
Kuhusu historia yake, imejaa rekodi za uzembe, utelekezaji, na usaliti. Iliuangusha Ummah katika hali yake mbaya zaidi na kuwaacha wanawe, wanawake, na wazee wake kuuawa na kuhamishwa bila kuchukua hatua yoyote ya maana huko Palestina, Syria, Sudan, Libya, Yemen, Iraq, na kwengineko. Haikuokoa Muislamu wala kunusuru nchi, ikiridhika na kauli za kulaani, kupinga, na misemo tupu ambayo haimfukuzi adui wala kuondoa dhulma. Kuhusu kadhia kuu ya Waislamu, Palestina inabaki ikikaliwa kimabavu na Mayahudi, Al-Aqsa inabaki ikinajisiwa na walowezi wao, na Gaza inabaki chini ya mashambulizi ya mabomu, kifo, na uhamishwaji, huku Ligi hiyo ikibaki imetulia tuli. Badala yake, ilikuwa miongoni mwa wa kwanza kutabanni mpango wa usaliti na makubaliano unaojulikana kama Mpango wa Amani wa Kiarabu, ambao uliwezesha umbile la Kiyahudi kubaki katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina.
Ni faradhi kwa Ummah kuizika Jumuiya ya Kiarabu katika bonde refu badala ya kutafuta kuiamsha au kuiboresha. Haijawahi kuwa chochote ila kisu katika moyo wa Ummah, chombo cha kuugawanya, na njia ya Amerika na Magharibi kupitisha miradi yao na kudumisha udhibiti wao wa kikoloni juu ya ardhi zetu. Badala yake, na badala ya serikali zote za madhara katika ardhi za Waislamu, Ummah lazima usimamishe Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itauunganisha na kuuongoza kwenye ushindi na tamkini.
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |