Afisi ya Habari
Amerika
| H. 3 Rajab 1447 | Na: 07 / 1447 H |
| M. Jumanne, 23 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kifo cha Imam Fouad Saeed Abdulkadir: Pindi Hifadhi Inapogeuka Kuwa Mkasa
(Imetafsiriwa)
Idara ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE) imethibitisha kifo cha Fouad Saeed Abdulkadir, raia wa Eritrea mwenye umri wa miaka 46, ambaye alifariki tarehe 14 Disemba akiwa kizuizini mwa ICE katika Kituo cha Ushughulikiaji cha Moshannon Valley huko Pennsylvania. Kulingana na ICE, Imam Abdulkadir anaripotiwa kupata maumivu ya kifua na kupokea uangalizi kutoka kwa wafanyikazi wa matibabu na huduma za matibabu za dharura. Kifo chake, mojawapo ya vifo kadhaa vilivyoripotiwa katika vituo vya ICE, bado kinachunguzwa na kimeongeza uchunguzi wa hali za uzuizi na upatikanaji wa huduma za afya za kutosha kwa wafungwa.
Jumuiya ya Waislamu inaomboleza kufariki kwa Imam Fouad Saeed Abdulkadir, ndugu anayeheshimika ambaye kifo chake kimesababisha huzuni kubwa miongoni mwa familia yake, wapendwa wake, na Ummah kwa jumla. Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia yake na tunaomba kwamba Mwenyezi Mungu ampe rehema na kuinua daraja yake.
Kinachoumiza vievile ni dhurufu zinazozunguka kuzuiwa kwake. Imam Abdulkadir inaripotiwa alitumia siku 215 kizuizini akisubiri kusikilizwa kwa kesi, na kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu uzuizi wa muda mrefu bila suluhisho. Ripoti za huduma duni za kimatibabu na hali ngumu za kifungo zinaonyesha kufeli kwa serikali kunakowaweka wafungwa katika hatari kubwa. Hali hizi, pamoja na kutokuwa na hatima kwa muda mrefu, zinaripotiwa kuchangia dhiki kubwa ya kimatibabu na hatimaye kifo chake.
Zaidi ya mkasa huu wa kibinafsi, kesi hiyo inaonyesha ukweli mpana na mchungu mno unaowakabili Waislamu kote duniani. Katika maeneo mengi, Waislamu huvumilia mateso, kuwekwa kizuizini kiholela, na ukandamizaji mikononi mwa serikali na watekelezaji wao kwa kukataa kutii amri zisizo za haki za kisiasa na kijamii. Matokeo yake, watu wengi wanalazimika kukimbia nchi zao kutafuta usalama, utu, na uhuru wa kuishi kulingana na imani zao.
Cha kusikitisha, wengi wanaotafuta hifadhi hukutana na dhulma zaidi katika nchi walizoamini zingetoa ulinzi. Kifo cha Imam Abdulkadir kinasimama kama ukumbusho mkali kwamba kuhama hakuhakikishi usalama, na kwamba dhulma ya kimfumo inaendelea kuwafuata walio dhaifu kuvuka mipaka.
Hili sio tukio la pekee, bali ni kielelezo cha hali iliyosambaratika ya Ummah ambao umetawanyika, umefichuliwa, na kunyimwa mamlaka yenye mshikamano yanayoweza kulinda maisha na hadhi ya Waislamu. Bila mfumo wa ulinzi unaohakikisha haki, uwakilishi, na uwajibikaji, Waislamu wanabaki dhaifu popote wanapoishi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu Imam Fouad Saeed Abdulkadir, awape uvumilivu na nguvu familia yake, na kuunganisha na kuulinda Ummah. Mwenyezi Mungu (swt) aurudishie Ummah huu ngao inayounga mkono utakatifu wa maisha ya Muislamu, kuwaunganisha watu wake, na kutoa usalama, hadhi, na haki kwa Waislamu kote ulimwenguni.
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Amerika
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |