Afisi ya Habari
Amerika
| H. 1 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: 16 / 1447 H |
| M. Jumatatu, 18 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mashahidi Watatu Jijini San Diego: Matunda ya Chiki dhidi ya Uislamu
[إِنَّا لِلَّٰهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutaregea.”
(Imetafsiriwa)
Nyoyo zetu zimejaa huzuni kufuatia mauaji ya kusikitisha ya Waislamu watatu katika msikiti mmoja jijini San Diego wakati wa siku takatifu za kwanza za Dhul Hijjah, miongoni mwa siku takatifu zaidi katika kalenda ya Kiislamu. Familia na jamii zinapojiandaa kwa Idd al-Adha, wakati wa ibada, kujitolea muhanga, na umoja, waumini wasio na hatia badala yake walikutana na vurugu na chuki ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu (swt).
Hizb ut Tahrir inatoa rambirambi zake za dhati kwa familia za waathiriwa na kwa jamii nzima ya Waislamu iliyotikiswa na kitendo hiki cha kutisha. Hakuna muumini anayepaswa kuhofia maisha yake ndani ya utakatifu wa msikiti. Muhimu zaidi, hakuna muumini anayepaswa kujihisi hana ulinzi na dhaifu kabisa.
Msiba huu haukujitokeza wa kipeke yake. Unaonyesha miaka mingi ya maneno ya kupinga Waislamu, kudhalilisha binadamu, na simulizi ambazo zimesawazisha tuhuma na uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu. Maonyesho ya mara kwa mara yanayowalinganisha Waislamu na ugaidi, pamoja na utumiaji vibaya siasa wa hofu na vita dhidi ya Waislamu, yamechangia mazingira ambapo chuki isiyo na msingi inaweza kustawi. Haya ndiyo matokeo pindi vyombo vya habari na serikali vinaposhirikiana kuwatusi Waislamu ili kuunda mazingira ya hofu na chuki ili kuhalalisha unyenyekeshaji wao Waislamu ndani na nje ya nchi.
Katika wakati huu wenye uchungu, tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt) awaruzuku Shuhada (mashahidi) wetu rehema zake, awape Jannatul Firdaus na awape subira na nguvu wapendwa wao. Tunamuomba (swt) auunganishe Ummah juu ya Uislamu, nyuma ya ngao ya Khalifa, na awalinde watu wote kutokana na chuki, dhulma, na ghasia.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Amerika
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |