Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  8 Ramadan 1441 Na: H.T.L 1441 / 08
M.  Ijumaa, 01 Mei 2020

Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon
Huisheni Faradhi ya Ijumaa Mnamo Tarehe Nane Ramadhan Mjini Sidon
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon katika mji wa Sidon imetoa wito wa swala za Ijumaa kufanyika katika uwanja wa wazi mjini humo, miezi kadhaa baada ya kukatizwa kwa swala za Ijumaa, kutokana na hatua za ufungaji zilizo chukuliwa na utawala huu hususan baada ya tawala hizi kutangaza mwanzo wa kuondoa marufuku ya kufungwa (misikiti) na kuhafifisha uzuiaji matembezi ya watu, lakini wakaziweka sehemu za kuabudu katika awamu za mwisho za kuondoa marufuku hiyo, baada ya casino, maduka makubwa, shule na vyuo vikuu, ambazo ndizo zenye umati mkubwa na mawasiliano ya muda mrefu baina ya watu.  

Waandazi walikuwa makini kuchukua hatua muhimu za kuhifadhi usalama wa watu, huku wanaohudhuria wakilazimishwa kuvaa barakoa, na kuja na miswala yao, pamoja na kupimwa joto la mwili kwa wale wote wanaoingia sehemu hiyo ya swala.

Mkurugenzi wa afisi ya Hizb ut Tahrir mjini Sidon, Hajj Hassan Nahhas, alitoa Hotuba ya Ijumaa na kuwaongoza watu katika swala, ambapo katika hotuba yake aliashiria sababu ya swala kuswaliwa sehemu hii. Kisha akageukia janga baya la kiuchumi wanalopitia watu nchini humu, akifafanua kwamba sababu kuu ni ufisadi wa wanasiasa na kuamiliana na Riba. Alitaja kuwa suluhisho ni kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu nchini Lebanon na ulimwenguni kupitia kusimamisha dola ya Uislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, akitamatisha kwa dua kwa Mwenyezi Mungu awaondolee Waislamu janga hili, na kwamba swala katika siku zijazo ziswaliwe ndani ya misikiti ya mji huo.

Swala hiyo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu ambao nyoyo zao zilitamani swala ya Ijumaa, hususan wakati huu wa mwezi wa Ramadhan ambao mwaka huu umekuja katika hali  zisizo za kawaida kote ulimwenguni, ambazo zinamulika mshikamano wa watu na dini yao na ibada zao, licha ya kampeni zote za kuwatenga na kuwaweka mbali na dini yao, zikiongozwa na dola, makundi na mashirika.

Kuhusiana na hili, tunawasihi wahusika wote, mjini Sidon na Lebanon, kufanya kazi pasi na kuchoka ili Waislamu warudi katika ibada zao, na kuzitia shinikizo tawala kutoiweka misikiti mwishoni mwa orodha ya kuondolewa marufuku ya kufungwa pasi na udhuru wa kisayansi au wa kivitendo, wala hata udhuru wa Kisheria. Na kwa mara nyengine tena tunawakumbusha watu wetu utafiti (Jibu la Swali, na Majibu ya Maswali kuhusu Jibu la Swali) lililotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, juu ya mada ya swala kuambatana na athari za janga la virusi vya Korona.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu auondolee uzito Ummah huu, na atuweke katika msafara wa wale wanaohuisha tena faradhi za Mwenyezi Mungu katika ardhi Yake, na aifanye hii iwe ndio kazi yetu, na matendo yetu yote yawe na ikhlasi kwa ajili Yake, Subhanahu, na kwamba dhurufu hizi zilizo katika Ummah huu na ulimwenguni ziwe ni zenye kuwabainikia kuwa ni ukweli, uliyo sadikishwa na maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ)

“Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?” [Fussilat: 53]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.