Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 22 Rabi' II 1447 | Na: 1447/18 |
M. Jumanne, 14 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Sharm El-Sheikh Ni Kutangaza Ushindi Juu ya Ummah, Kumakinisha Utiifu, na Kuimarisha Ukaliaji wa Kimabavu
(Imetafsiriwa)
Baada ya Trump kutangaza ushindi yeye na mfuasi wake, umbile la Kiyahudi, walioupata katika hotuba yake mbele ya Knesset. Ushindi huu ulipatikana dhidi ya raia wasio na silaha, wakiwemo wanawake, watoto, na wazee, pamoja na miti na mawe, Muuaji wa Gaza alielekea kwenye kongamano hilo liliopangwa na kibaraka wake nchini Misri, Sisi, ambapo aliwaalika wale wote waliokula njama dhidi ya ardhi iliyobarikiwa. Kongamano hilo lilifanyika mjini Sharm El-Sheikh mnamo tarehe 13/10/2025, chini ya kichwa “Kongamano la Amani la Sharm El-Sheikh.” Zaidi ya nchi ishirini na mashirika ya kimataifa yalihudhuria, wakiongozwa na Rais Trump wa Marekani na Rais Sisi wa Misri, kwa ushiriki mkubwa kutoka kwa viongozi wa Kiarabu na Magharibi, akiwemo mfalme wa Jordan, Amir wa Qatar, rais wa Ufaransa, rais wa Uturuki, Waziri Mkuu wa Pakistan, na Waziri Mkuu wa Indonesia, pamoja na wajumbe wa Ulaya na Asia. Kongamano hili limekuja siku chache tu baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya uvamizi na Hamas, ambayo ni pamoja na kubadilishana wafungwa, kusitishwa kwa uhasama, na kufunguliwa kwa mazungumzo ya usimamizi na ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza.
Licha ya kichwa chenye kung’aa cha kongamano hilo, ambalo linadai kukuza amani, utulivu, na ujenzi mpya, uhalisia wake haugongani wote na kichwa chake. Kiini cha halisi cha kongamano hilo kilikuwa ni sherehe ya Trump ya ushindi unaodaiwa na umbile la Kiyahudi, na kuuwasilisha kama mafanikio makubwa yanayostahiki Tuzo ya Amani ya Nobel—tuzo ambayo haijawahi kutolewa kwa wale wanaowakilisha maadili na kanuni za juu au kwa mafanikio ambayo yanatumikia ubinadamu kikweli. Kupitia kongamano hilo, Trump alitaka kujionyesha kama bwana na mtoa maamuzi pekee katika kuunda na kufinyanga suala la Mashariki ya Kati. Zaidi ya hayo, Trump alitoa wito wazi wazi kwa ruwaibidha (watawala wajinga wasio na maana) wa nchi za Kiislamu wajiunge na Makubaliano ya Abraham, akimaanisha kuitawaza dola inayokalia kwa mabavu kama mfalme wa Mashariki ya Kati mpya anayoitaka.
Misri ilicheza dori muhimu katika kuandaa kongamano hilo na kutoa dhamana ya Waarabu kwa mipango ya Marekani, kama ilivyokuwa katika makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano. Serikali ya Misri imejitolea kwa Makubaliano ya Camp David, ambayo yalidhibiti harakati zake za kijeshi na kuifanya kuwa mlinzi wa mipaka ya umbile la Kiyahudi. Leo hii, inajionyesha kama mpatanishi “asiyependelea upande wowote”, wakati dori yake ya halisi ni kufungua njia kwa nchi zengine za Kiislamu kuhalalisha mahusiano na Mayahudi, katika kutimiza matakwa ya Amerika na kudhamini usalama wa Mayahudi kutokana na tishio lolote kutoka kwa Umma.
Walaji njama hawa waovu huko Sharm El-Sheikh hawawakilishi kadhia ya Palestina, wala wao si katika Umma wa Kiislamu, mmiliki wa kadhia hiyo. Wajibu wa kuikomboa Palestina na kulipiza kisasi kwa mashahidi wake ni jukumu zito ambalo linaweza tu kutekelezwa na wanaume wa wanaume.
[صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ] “walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu.” [Al Ahzab: 23]. Na hawa hawatakuwa ruwaibidha (watawala wajinga wasio na maana). Makubaliano au kongamano lolote linaloegemezwa katika kulitambua umbile la Kiyahudi, kuishi pamoja nalo, na kumakinisha uwepo wake katika shubiri yoyote ya ardhi ya Palestina ni batili kabisa, kwa sababu inagongana na hukmu za kukatikiwa za Kiislamu kwamba Ardhi Iliyobarikiwa lazima ikombolewe, na kwamba ni haramu kukiacha kipande chochote chake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ]
“Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” [Al-Anfal: 39]. Mwenyezi Mungu (swt) asema: [وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ] “Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa” [An-Nisa: 75].
Kongamano hili ni sehemu ya mradi mpana zaidi wa Marekani wa kupangilia upya eneo hili, kuoanisha umbile la Kiyahudi ndani yake, na kufilisi kadhia ya Palestina kupitia michakato ya uzushi ya kisiasa baada ya kuwachosha watu wa Gaza kwa vita na vikwazo. Michakato hii inalenga kuanzisha kikosi cha kimataifa cha ufuatiliaji ili kusimamia mipango ya usalama na kuhakikisha usalama wa Mayahudi, kwa msaada wa serikali za Kiarabu, zinazoongozwa na serikali ya Misri. Kucheza dori hii ni uhalifu wa uhaini, kwani hautokani na maslahi ya Ummah, bali utumwa kwa bwana Marekani na utekelezaji wa mipango yake.
Wajibu kwa Gaza sio kufanya makongamano au kusubiri maazimio ya kimataifa, bali ni kuhamasisha majeshi ya Waislamu kukomboa ardhi iliyobarikiwa kutoka baharini hadi mtoni. Majeshi haya yana uwezo wa kuangamiza umbile la Kiyahudi ndani ya saa moja ya siku. Ama watawala wao ndio kikwazo kikubwa zaidi cha harakati za majeshi haya, kwa sababu wao ni wasaliti waliofungamana na makubaliano ya udhalilishaji na vikwazo vya kijeshi (Camp David, Wadi Araba, Oslo, na Makubaliano ya Abraham). Hapa ndipo panapoanzia kazi halisi ya kuikomboa Palestina kwa kuzing’oa serikali hizi na kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo hukusanya majeshi na kuyasukuma kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) amewawajibisha kuyafanya na kutabanni jihad ili kuikomboa ardhi hiyo na kuunganisha Ummah.
Enyi Wanajeshi wa Kinanah (Misri): Nyinyi si wanajeshi wa Marekani wala si ala za kutekeleza mipango yake. Bali nyinyi ni sehemu ya Umma wa Muhammad (saw) wenye kuwajibika kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu ya kuwanusuru wanaodhulumiwa na kuinua juu neno la Mwenyezi Mungu. Kinachotokea katika Sharm El-Sheikh, chini ya usikivu wenu, macho na ulinzi wenu, si ushindi kwa Gaza, bali ni uimarishaji wa kuzingirwa kwake na udhibiti wa adui juu ya hatima yake, kuwapa Mayahudi kile ambacho wasingeweza kupata licha ya kila kitu walichofanya kwa Gaza na watu wake. Jibu la lazima la Kiislamu ni kupinga makongamano kama haya, kufichua malengo yake, na kuelekea kwenye ukombozi wa kweli, na sio “amani ya kirongo”.
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na Watoto” [An-Nisa: 75]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |